Hiyo zamani ina mapungufu. Rais yuko juu ya katiba. Haimgusi kabisa rais.Ya zamani imetushinda kuwajibisha viongozi wakikosea. Mpya tutaweza kweli?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hiyo zamani ina mapungufu. Rais yuko juu ya katiba. Haimgusi kabisa rais.Ya zamani imetushinda kuwajibisha viongozi wakikosea. Mpya tutaweza kweli?
Mwisho wa siku solution bado ni moja. Elimu bado ni jambo la msingi. Kwa sababu. Imagine watanzania wote million 55 wakawa na uelewa wa intelijensia ya siasa na elimu ya juu. Hivi nani ataweza kumdamganya nani. Hapa ndo utashuhudia mabadiliko makubwa. Ila kwa style iliyopo. Wajinga bado ni mtaji mkubwa wa wanasiasa. Wakiisha wajinga kila mtu anarudi kwenye umaskini. Kwa sababu hakuna mtu anae elimika anakubali kufanywa mtumwa " educated mind cant be enslaved"Ya zamani imetushinda kuwajibisha viongozi wakikosea. Mpya tutaweza kweli? Cha msingi issue sio katiba. Issue ni tutaweka mfumo gani ambao utafanya kila mtu awajibike na sheria. Lakini mwisho wa siku hata kama tukipata hiyo katiba. Bado kuna swala moja ambalo ni gumu kutatulika "rushwa" kiongozi anaweza kucheza faulo. Lakini marefa( bunge na mahakama) wakapewa rushwa na wakavunga hawajaiona faulo, hata kama wananchi wakiona faulo. Bado kiongozi na timu yake ya jeshi na mahakama wanalindwa na jeshi. So mwisho wa siku wananchi mtabaki kulia tu.
Ndo maana nasema. Cha msingi hii kitu inahitaji ma genius na wana falsafa kuijadili na kutengeneza mfumo utakao kua permanent
Umewasilisha mawazo yangu kwa namna ingine kabisa yani kama ulikuepo akilini mwangu.Ndiyo na ni ukweli kabisa, Katiba tunayojaribu kuitafuta kwa jasho jingi na Energy nyingi, nasikitika kusema, haitatusaidia popote kama nchi.
Kama kuna mtu anapingana na mimi, Embu atusaidie kujibu maswali haya
Ni kweli tumekuwa na katiba isiyokidhi matakwa yetu hususani katika mizania ya kisiasa, kwa maana, katiba iliyopo, ilitungwa chini ya Chama kimoja, hivyo kuvifanya vyama vingine kukosa uhalali wa kulindwa na katiba hii tuliyonayo
Kingine, Katiba hii iliyopo, inamfanya Rais wetu kuwa mfalme, ni kama yeye ni mtu wa kwanza na wa mwisho, kwa lugha ys kiyunani, ni Alfa na Omega, n.k
Sasa basi, Ukisikiliza kwa umakini, wengi wa wanaharakati wetu kwenye majukwaa ya kisiasa na majumkwaa mbalimbali mbali, Utasikia wakisema, Tunataka katiba itakayotuwezesha kuwaajibisha wote wanaovunja katiba
Ni jambo jema, maana mtu yeyote anayediriki kuvunja makubaliano yetu na katiba yetu , ni sawa na matusi kwa watu woote kama taifa
Tumeshuhudia katiba yetu ikivunjwa waziwazi na baadhi ya viongozi wetu,
Bahati mbaya ni kwamba, kuna waliovunja katiba hata kwa wale ambao, katiba hailindi ouvu wao kama ilivyo kwa Maraisi wa nchi, lakini wanapovunja, Hasira zetu tunazielekeza kwa kiongozi mkuu, tunamsagia meno, Wakati huohuo, Katiba yetu mbovu tuliyonayo, ni kumlinda Raisi wa nchi na maovu yote kipindi awapo madarakani, na kwamba Hawezi kushitakiwa kwa kosa lolote awapo madarakani
Na bila shaka, shida yetu inaanzia hapo
Okay, Achilia mbali makosa ya Rais kwa mjibu wa katiba mbovu tuliyonayo kwamba, hatoshitakiwa kwa makosa yoyote aliyotenda akiwa madarakani, Hili tunaweza kusema, lipo juu ya mamlaka ya kawaida ya mwananchi kumwajibisha Raisi wao kwa kuwa katiba inamlinda
Upande wa pili kwa kosa hilohilo la kikatiba, Tumeshuhudia Bunge lisilo halali, Ni bunge ambalo wabunge wenginewe waliomo humo bungeni si wabunge halali kwa mjibu wa katiba za vyama vyao pia kwa mjibu wa katiba ya nchi, kwamba hawana uhalali wa kuwa wabunge kwa kuwa, hawatambuliki na vyama vyao na katiba haitambui mtu wa aina hiyo kuwa sehemu ya bunge
Sasa basi
Nionyesheni ni wapi ambapo huyo mkuu wa mhimili huu wa Bunge alipohalalishiwa na katiba hii mbovu tuliyonayo kwamba naye hawezi kuwajibishwa,
Je, sasa, ni nani wa kumwajibisha?
Ni kwa nini tunataka katiba mpya, Je, ni nani atakuwa mbadala wetu wa kusimama na kuwawawjibisha wote wavunja katiba?
Je, katiba hii mbovu ilipokuwa ikivunjwa, ni nani anafahamika ambaye yeye anapaswa kudili na wavunja katiba yetu? Je, alifanya kazi yake?
Na kama alishindwa kuwashughurikia hao waharifu wa kikatiba, Ni kwa vipi anadhani itakuwa rahisi kuwashughurikia kukiwepo katiba mpya?
Ni nani asiyejua kwamba, Watanzania, Watanzania kwao ni wazuri wa kuhamaki mitandaoni pekee ila nje ya hapo ni watu wanafiki na wapole kama maji ya mtungi? na ndiyo maana hata Asiyelindwa na katiba aweza kuvunja katiba na ikawa salama?
Mkinionyesha atakayekuwa zamu ya kuwashughurikia wahalifu wa kikatiba badala yetu, ndipo nitakubali kwamba, Tunataka kweli katiba na tumemaanisha
Katiba haijilimdi, haijipeleki mahakamani, haiandamani na wala haimtishi mvunja katiba, Nionyesheni mlinzi wa katiba
Tanzania hoye?
Ili tume iwe huru inatakiwa iwe na sifa gani ?Angalau basi kuwe na tume huru ya uchaguzi, hilo nalo lina gharimu nini nchi! Kwani Serikali haijui kuwa tume iliyopo sio huru chini ya mfumo wa vyama vingi?!
Mkuu hili suala linabidi lije tena maana vibutu vipo vya kurejea wananchi walisema niniHivi nikisema kwamba draft ya Warioba ilikataliwa na wajumbe utabisha? Kazi ya Bunge la Katiba ni kusema ndioooo au kujadili na Kisha kuamua? Kiufupi draft ilikataliwa na wajumbe ndio maana ikawekwa pembeni
Ndoma huko kwa mswati,watu wanamtoa kwa nguvuWatanzania hawajui kuandamana, hawajui kudai haki yao, wao wanaamini tu kwamba, Mungu ndiyo kila kitu.
Hivi kwa nini kweli tunahangaishana kudai katiba?
Hahaha.Katiba ya sasa inaruhusu maandamano na mikutano ya siasa, si ndiyo jamani?
Mbona mambo yakienda kombo, watu hawaandamani nchini?
Mbona wanasiasa wa upinzani hawafanyi mikutano ya kisiasa ya nje wakati katiba inaruhusu?
Ukipata majibu ya hayo maswali, ndo utagundua, chanzo cha matatizo ya Watanzania ni katiba au hilo jibu la maswali ya hapo juu!
Nadhani hapa, kinachofanya katiba yetu iwe ngumu kupatikana, ni pale inapoonekana inadaiwa na wanasiasa badala ya wanaharakati huru wasioegemea chama chochote
Siasa zetu zimechafuka mno mkuu, Kwa tulipofikia, Ni rahisi kwa jambo mhimu kama hili, CCM na vyama vingine visivyoamini katika Chadema, basi ni rahisi kuona hilo ni jambo la chadema kama ambavyo Chadema hupuuza kila kilichojema kinachoanzishwa na CCM
Kupatikana kwa katiba hii tunayoihitaji sana, ni aidher, Chadema wanyamaze, kuzaliwe makundi mengine kabisa yasiyoshabihiana na chadema wala CCM, naamini ni rahisi kusikilizwa
Ndio hapo tunapofeli kuwa na katiba yetu, Tunataka hata hao wasiokuwa na elimu wajue umhimu wa kuwa na katiba inayogusa maisha yao na wajue kwamba wanawajibu wa kuipigania na kuitetea
Katiba inshitaji makundi yote na siyo mashabiki wa Chadema wala nani
Mimi pia huwa nashangaa jinsi watu wanavyoweka mkazo kwenye katiba mpya zaidi ya ubora wa elimu yetu.
Tungekuwa na elimu ya viwango stahili suala la katiba lingekuwa agenda ya wananchi karibia wote na sio sasa ambapo wenye shida nayo ni wanasiasa, wanaharakati na wasomi tu.
Tungekuwa na elimu bora watanzania wasingeruhusu kuvunjwa kwa katiba, kuchezewa uchaguzi na mihimili mingine ya serikali kama ilivyokuwa miaka kadhaa iliyopita.
Tunachohitaji haswa na elimu ya bora kwa ujumla na ya uraia ili tusije hata tukipata katiba mpya watu wakaendelea kuivunja maana watu ni walewale na uelewa ni ule ule na tabia zilizile.
Hoja ni nzuri ila kwa mtazamo wangu hakuna katiba yoyote Duniani ambayo hujilinda au kijitete yenyewe. Je katiba ni nini ni mkataba baina ya mtawala na mtawaliwa. Kwa ukweli huu basi mtu yeyote atakaevunja mkataba huu anaweza kuhoji kwa njia mbalimbali. Kwa upande wa serikali itakupeleka mahakamani na utafungwa. Kwa mwananchi njia zipo nyingi ikiwemo ya kwenda mahakamani, kuandamana na kupiga kelele. Na kelele hizi ndizo unazosikia, njia moja ikishindikana wananchi watatafuta njia njingine hadi wafike mwisho hadi kutokutii serikali iliyo madarakani kama Arab springs. Hiki kilio sio cha kufumbia macho au kukitolea utatuzi wenye kebehi kwani wananchi watatufanya nini ni hatari. Majeshi hayataweza kuzuia nguvu ya umma, serikali isitoe kisingizio cha kujenga uchumi this is cheap politics zenye dalili za kudharau mwananchi ni hatari sana.
CCm wanataka katiba hii hii itakayo waacha madarakani? Huu ujinga wa kuona katiba kama nyaraka ya uchaguzi mtauacha lini?Wakina mbowe wanataka katiba mpya itakayo waingiza madarakani.
Shida yetu kuu iko hapo chief, hata tukipata katiba nzuri kiasi gani, kama hatuna ujasiri wa kukabiliana na wavunja katiba, Tunapoteza muda tu
Kwa maswali yako Chief, hapa tatizo siyo katiba, Tatizo ni Sisi watanzaniaKatiba ya sasa inaruhusu maandamano na mikutano ya siasa, si ndiyo jamani?
Mbona mambo yakienda kombo, watu hawaandamani nchini?
Mbona wanasiasa wa upinzani hawafanyi mikutano ya kisiasa ya nje wakati katiba inaruhusu?
Ukipata majibu ya hayo maswali, ndo utagundua, chanzo cha matatizo ya Watanzania ni katiba au hilo jibu la maswali ya hapo juu!
Nadhani pia, utaratibu wa upatika aji wa katiba ukifanikiwa, kuwekwe kipengele kingine kitakachoondoa sauti ya Raisi kwamba, Wananchi watakapoona Katiba yao inamapungufu na wanataka katiba iundwe upya tena, kusihitajike sauti ya Raisi kuamua iandikwe au la, Ni kuachwe kipengele cha kupiga kura kuanzishwa katiba nyingine, wananchi watapiga kura, na hizo kura zikifikia kiwango kitakachoruhusiwa kuandikwa katiba zikitimia, mtu yeyote asiseme eti achwe ajenge sjui nini ndio aone katiba kama itaandikwaNa huu ndo unatakiwa kuwa msimamo wa taifa katiba ni hitaji la nchi sio hisani ya kiongozi fulani kuamua kitu hata nicha kijinga basi Kiko sawa hapana
Nani wa kuwawajibishwa hao wanaivunja katiba sasa?Naunga mkono hili wazo japo bado nataka katiba mpya. Kama tumeshindwa kumuwajibisha kiongozi anaevunja katiba ya zamani basi hata mpya ikija itavunjwa tu na hakuna kitakachotokea
Ukifanikiwa kutenganisha mihimili ya nchi hakuna ujinga utaendelea.Tatizo sio katiba. Hata katiba itungwe na malaika. Viongozi wakiamua kuwa play wanawaplay tu. Cha msingi ni kutafuta njia ya kumbananisha kiongozi akivunja katiba. Hili jambo liko very complicated na linahitaji ufikiriaji wa hali ya juu na kwa kina. Pia linahitaji mwanafalsafa ambaye si mlafi wa hela itakayoweza kumbadilisha mawazo.