Kwa mujibu wa katiba rais ni kama tu Mungu wa nchi
Na hiyo imefanya mihimili yote kuwa chini yake
nadhani viongozi wa hii mihimili wanatokana na rais pia kwahiyo mambo Meusi yanayofanyika huko yana baraka za Mungu wa nchi kwa hiyo hilo shtaka utalipitishia wapi
Rais hana hofu ya kuvunja sheria
Anatoa order tu
Maelekezo kutoka juu
Sasa hii inawahakikishia usalama hawa viongozi wa huku chini na wao wakiwa na mambo yao binafsi yanayoenda kinyume na sheria hawana hofu kwa kuwa ni wanafamilia tu wa bwana mkubwa.
Nguvu ya kumshtaki mkuu wa wilaya tu utaitoa wapi kwenye mahakama gani kesi hiyo itapita.
Yote hii ni katiba tupunguze mamlaka ya rais kupitia katiba hawa viongozi wengine wapatikane kwa njia nyingine isiyohusiana na connection na rais. Na rais ashtakiwe akienda wrong.
Mihimili ijitegemee na rais ashtakiwe hii itasaidia, kesi zitakuwa nyingi tu tofauti na unavyofikiri wewe
Lakini lengo la kubadili katiba siyo hili tu la kuwapunguzia madaraka na kushtaki watu hapana. Lakini kumbuka pia lengo la katiba ni kupunguza madaraka ya viongozi wa serikali ambao ni CCM.
CCM wewe na wenzio hamko tayari kwa hilo kwa namna yoyote ile kwa kuwa madaraka yakipungua hamtakuwa na uhakika wa kulindana na kubaki na madaraka ndiyo mana mnakuja na hoja dhaifu kiasi hichi hapa.
Hoja yenye mashiko hamna.
Jambo dogo tu, tuangalie uchaguzi uliopita ni zao la katiba tulio nayo ndiyo maana tunafikiria kuibadilisha, kuachana na hayo mengine yote hoja na hitaji la katiba mpya ni uchaguzi uliyopita wewe unaongeleaje uchaguzi uliopita ni sahihi kwa kilichotokea?
Sent from my TECNO KC8 using
JamiiForums mobile app