Nasikitika kusema kwamba, Katiba Mpya tunayoitafuta kwa nguvu nyingi haiwezi kutusaidia

Nasikitika kusema kwamba, Katiba Mpya tunayoitafuta kwa nguvu nyingi haiwezi kutusaidia

Kwani katiba inamsaidia nini mtu aliyeko Kijijini zaidi ya wanasiasa kugombania keki ya taifa?
Hili swali inawezekana uliyeuliza ni PhD holder, lkn itoshe kusema tu nchi hii bado ina majitu majinga jinga mengi sana.
 
Jamaa nakuonaga una akili kumbe na wewe ni pimbi tu, haya hata kama sio lissu au mbowe kwanini asishabikie katiba itakayotoa fursa kwa mtz yoyote kupata madaraka kwa njia halali na ya wazi hata kama atakuwa ni yeye mwenyewe au babu yake au Dada yako?
Kumbe ww unataka kugombea urais?
 
Doh!!

Ni kati ya maswali ambayo nimekuwa nikijiuliza kuhusu usimamiaji wa katiba yetu

Majibu umeyaona? Kwa hakika ni muhimu kuelewa vinginevyo unaweza kushangaa kwanini tusijikite kwenye gombesugu.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Haiwezi kwani yanayopiganiwa ni maslahi ya wanasiasa pekee.
Kweli kabisa mkuu, katiba mpya ni takwa na hitaji la wanasiasa. Sisi huku vijijini mahitaji yetu makuu ni, huduma bora za afya, maji, shule, barabara, masoko ya uhakika ya kuuzia mazao yetu, nk. Hayo yote yanawezekana bila katiba mpya!
 
Uwe unasoma comments. Elimu kuhusu katiba na umuhimu wake inakuhusu sana wewe. Soma comments kuna elimu inatolewa humo. (Wewe unakwazika na tume huru ya uchaguzi) . Katiba ni zaidi ya tume huru ya uchaguzi.
Hizo huduma unazozisema kwa katiba hii kiongozi anaweza akaamua asizilete na usiwe na la kumfanya.
Hebu fikiria wakati jiji kama Mbeya linakosa barabara za uhakika jemedari akaenda kujenga airport kijijini kwake, akaweka mpaka traffic lights[emoji3]. Sababu hakuna wa kumcheck kwa mujibu wa katiba.
Soma comments mbalimbali utaelimika.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Ikiwe sisi wanachadema hatuwezi kudai katiba ya CHADEMA inayotoa uenyekiti wa milele kwa Mbowe tunawezaje kupata ujasiri was kudai katiba ya nchi?

Mwamba tuvushe, wala hatutaandamana kukuondoa hakuna kama wewe, MWAMBA TUVUSHE.
 
Chanzo cha huyu spika kutowajibishwa ni Katiba yetu mbovu inayompa rais ufalme.

Kwa muktadha huo basi, kama kuwepo kwa Covid-19 bungeni kungekuwa kunamuudhi rais siku nyingi sana wangekuwa washaondolewa.

Lkn kwa kuwa ni Mungu mtu, na kwa kuwa kuwepo kwa Covid-19 bungeni Kuna mnufaisha yeye na chama chake ndiyo maana wapo hadi leo .

Usiulize ananufaikaje. Kuna ka kipengele ka kutoa misaada ya mrengo wa demokrasia kanataka bunge liwe na wabunge wa upinzani
Kwanini umlaumu spika na usiwalaumu wale wabunge at the first place?
 
Naunga mkono hoja.

Liwe takwa la wananchi na si kikundi cha wakosoaji wa utendaji wa Serikali,wasiwasingizie wananchi wakati hatujawahi kuwaona hata kidogo wakiamdamana au kuhamasishana kutaka hiyo Katiba.

Kazi iendeleee.
 
Hizi ni fikra mfu na za kipumbavu, akina nyerere wkt wanapgania Uhuru haikuwa ajenda ya watz wote Bali ilikuwa ni kakundi kadogo tu, thanks God kwa ilikuwa ni kwa manufaa ya weusi wote bila kujali idadi ya waliokuwa mstari wa mbele kudai, pia ktk hili la katiba hakuna ubaya tukapata katiba bora hata kama alieishupalia ni lissu pekee, make itakuwa ni kwa faida ya watz wote bila kujali kakundi kadogo
Katiba ambayo wananchi hawawezi kuisimamia unategemea watawala wataifuata kwa hisani yao? Bila sisi wenyewe kuwa na uelewa na atitude ya kuisimamia katiba hata tubadilishe katiba mara mia bado watu wataichezea tu.
Kweli tunataka katiba mpya ila wanasiasa wetu hawa wanaopigia kelele katiba mpya wakati hatujawahi kuwasikia wakipush elimu ya uraia na ujumla wake iboreshwe ni wachumia tumbo wanaotaka katiba ya kuwapa madaraka and nothing else.
 
Napinga uwanzishwaji wa mchakato wa katiba kwa sasa, Ni hadi wananchi watakapofahamu umhimu wa katiba hiyo

Kwani kwa sasa, ni kupoteza fedha za walipa kodi tu na kuwasaidia wanasiasa kuitafuta ikulu kwa manufaa yao

Tunataka kwanza wananchi wajue umhimu na namna bora ya kuilinda katiba na kuhakikisha wataitetea kwa nguvu zote na kwa gharama zote pindi mshenzi mmoja atakapoikanyaga
 
Kwani kipindi JK anafanya harakati za kupatikana kwa katiba mpya kupitia maoni ya wananchi ,wananchi walikuwa na elimu gani ya uraia kuhusu katiba?
 
Napinga uwanzishwaji wa mchakato wa katiba kwa sasa, Ni hadi wananchi watakapofahamu umhimu wa katiba hiyo

Kwani kwa sasa, ni kupoteza fedha za walipa kodi tu na kuwasaidia wanasiasa kuitafuta ikulu kwa manufaa yao

Tunataka kwanza wananchi wajue umhimu na namna bora ya kuilinda katiba na kuhakikisha wataitetea kwa nguvu zote na kwa gharama zote pindi mshenzi mmoja atakapoikanyaga
Hivi mkuu kipindi Tume ya jaji warioba ilitumika kukusanya maoni kwa wananchi kuhusu katiba mpya wananchi walikuwa hawana elimu kuhusu katiba?
 
Kwa mujibu wa katiba rais ni kama tu Mungu wa nchi
Na hiyo imefanya mihimili yote kuwa chini yake
nadhani viongozi wa hii mihimili wanatokana na rais pia kwahiyo mambo Meusi yanayofanyika huko yana baraka za Mungu wa nchi kwa hiyo hilo shtaka utalipitishia wapi

Rais hana hofu ya kuvunja sheria
Anatoa order tu
Maelekezo kutoka juu
Sasa hii inawahakikishia usalama hawa viongozi wa huku chini na wao wakiwa na mambo yao binafsi yanayoenda kinyume na sheria hawana hofu kwa kuwa ni wanafamilia tu wa bwana mkubwa

Nguvu ya kumshtaki mkuu wa wilaya tu utaitoa wapi kwenye mahakama gani kesi hiyo itapita

Yote hii ni katiba tupunguze mamlaka ya rais kupitia katiba hawa viongozi wengine wapatikane kwa njia nyingine isiyo husiana na connection na rais
Na rais ashtakiwe akienda wrong

Mihimili ijitegemee na rais ashtakiwe hii itasaidia, kesi zitakuwa nyingi tu tofauti na unavyofikiri wewe

Lakini lengo la kubadili katiba siyo hili tu la kuwapunguzia madaraka na kushtaki watu hapana
Lakini kumbuka pia lengo la katiba ni kupunguza madaraka ya viongozi wa serikali ambao ni ccm
Ccm wewe na wenzio hamko tayari kwa hilo kwa namna yoyote ile kwa kuwa madaraka yakipungua hamtakuwa na uhakika wa kulindana na kubaki na madaraka ndiyo mana mnakuja na hoja dhaifu kiasi hichi hapa

Hoja yenye mashiko hamna.

Jambo dogo tu, tuangalie uchaguzi uliopita ni zao la katiba tulio nayo ndiyo maana tunafikiria kuibadilisha,
kuachana na hayo mengine yote hoja na hitaji la katiba mpya ni uchaguzi uliyopita wewe unaongeleaje uchaguzi uliopita ni sahihi kwa kilichotokea?

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
Hata katiba ya CHADEMA imemfanya Mbowe mfalme na mungu mtu. Hawezi kuibadili
 
Hahaahaaa haa 😂😂😂😂.

"Nionyesheni ni wapi ambapo huyo mkuu wa mhimili huu wa Bunge alipohalalishiwa na katiba hii mbovu tuliyonayo kwamba naye hawezi kuwajibishwa,"

Kwamba hujui ilishapitishwa kuwa wakuu wa mihimili na manaibu wao hawawezi kushitakiwa kwa makosa yoyote yatokanayo na utekelezaji wa majukumu yao na hii sasa ni sehemu ya sheria kwa mujibu wa katiba?

Pia hutambui kuwa mapungufu ya katiba iliyopo ndiyo yanayoyaleta mikanganyiko unayoiongelea sasa?

Kimsingi kama hufahamu hali nzima ni kama hivi:

1. Katiba iliyopo haiwawajibishi baadhi ya watendaji wakuu kwa kuikiuka, na hii ni kwa mujibu wa katiba yenyewe.
2. kwa katiba iliyopo pana watu hata kama wakiiba, wakipora, wakiuwa, wakidhulumu nk hiyo ni halali kwa mujibu wa katiba yenyewe.
3. katiba iliyopo inawapa baadhi ya watu mamlaka ya kujifanyia lolote bila kuhojiwa au hata kuwajibishwa tu.
4. Katiba iliyopo haitoi haki sawa kwa watu wote ndani ya nchi.
5. Kuna mianya mingi katika katiba hii ambayo inaweza kuifanya mihimili mingine hata kupoteza uhuru wake wa kiutendaji kwa mujibu wa katiba yenyewe.
6. Kuna utitiri wa nafasi za uongozi wasio na tija wala ridhaa ya wananchi ambao pia ni mzigo mkubwa kwa mlipa kodi.
7. Kuna utitiri wa vigogo wenye mapato yasiyoakisi tija, wala kuwa na ridhaa ya wananchi na wasiolipa kodi (stahiki) wanaopata uhalali kwenye katiba hii.
8. Nk nk.

Kwenye mazingira haya asiyewajibishwa kwa mujibu wa katiba atawajibika vipi kwa katiba hiyo?

Hadi hapo bado huoni umuhimu wa katiba muafaka zaidi tena katika hali ya dharura inayowezekana?

Unadhani ni mazingira yapi yalitufikisha tulikofika na awamu ya ile?

Katiba mpya yenye kuyaangazia kikamilifu mapungufu yote yaliyomo ni suluhisho kwa haki, usawa, na uhuru wetu, watoto wetu na hata watoto wa watoto wetu.

Hili ni hitajio sahihi na la msingi ambalo si sawa kupuuzwa.
Nitaaminije bila kuja na vipengele vya hiyo katiba, vifungu ambavyo vinaonyesha eti sipika naye amewekewa zuwio la kushitakiwa akivunja katiba pindi awapo kwenye kiti
 
Katiba inamsaidia nini mwanachi ambaye anahangaika kutafuta mlo mmoja kwa siku!?
Mnajua kabisa umuhimu wa katiba mpya yenye kujenga taasisi imara Ila kwa maksudi mnapinga kwa maslahi yenu na kuzidi kuwapumbaza Watanzania.
 
Back
Top Bottom