Nasikitishwa na uhusiano wetu na Kenya, unaumiza wakulima na wafanyabiashara

Nasikitishwa na uhusiano wetu na Kenya, unaumiza wakulima na wafanyabiashara

Hii inayoitwa jumuiya ya Afrika mashariki ni uhuni kama uhuni mwingine, maana ni jumuiya ya viongozi na sio ya wananchi, utashi wa viongozi ndio unaofanya kazi na sio kilichoandikwa kwenye mikataba. Ni rahisi sana tofauti za viongozi kuwa ndio misimamo ya nchi, na hili halihitaji degree kulijua.
 
Mtoa mada acha unafiki kwa nchi yako, sawa Magufuli mbaya, Je Mseven pia mbaya kwa Kenya? maana Kenya wame ban mahindi ya Uganda a Tanzania kuingia Kenya , nahisi Kenya ndio wana tatizo kwa hili, unataka kutuambia Kenya ana uhusiano na diplomasia nzuri na nchi ipi majirani?
Siku hizi wapingaji wa serikali wamekuwa wajinga sana. Tangazo limepiga ban mahindi ya Tz na Uganda ila wamekomaa na diplomasia ya Tz. Very stupid. Sisi tuwe positive tuangalie ikiwa kweli yana shida turekebishe. Ikiwa hayana shida tutafute masoko mengine au tuichukulie kama fursa ya kuongeza shughuli zingine za uzalishaji zinazohitaji mahindi. Kama vile ufugaji.
 
kwa hivyo wewe unaona ni sawa wananchi wa pande zote waumie kwa sababu ya UJINGA wa viongozi wao?!.

kumbuka hao maviongozi mshahara na posho zao ziko palepale!.
Ujinga wa viongozi wetu ni upi mkuu. Uganda pia wamefanya ujinga gani? Maana wao pia mahindi yao yamepigwa ban.
 
Nilitamani kuanzisha uzi kuhusu hili suala lakini nashukuru kwa bandiko hili maana limelenga kile nilichotaka kusema.

Binafsi nimekuwa mdau wa kilimo kwa muda mrefu sana, kuanzia kulima mpaka kushiriki makongamano mbalimbali yanayohusiana na sekta ya kilimo na kuna hoja kadhaa ambazo wakulima wamekuwa wakizitoa kwa Serikali lakini kutofanyiwa kazi na hii sasa ndio majibu yake, japo inabidi kutafiti zaidi kama kweli Kenya wanasema ukweli au ndio VITA YA KIUCHUMI.

Hoja kubwa ambayo imekuwa ikitoka mara kadhaa ni kuhusu suala la mbegu, wadau wameshauri mara nyingi turudi kwenye mbegu zetu za asili maana hizi tunazoambiwa za kisasa zina changamoto nyingi sana, mojawapo ni hii ya kushambuliwa na wadudu hali inayopelekea wakulima kutumia madawa mengi sana ili kuweza kulinda mazao yao, na hili nimelishuhudia kwa macho yangu, sasa kwa hali hii tutajiteteaje kwamba mahindi yetu hayana sumu?

Wakulima watanielewa vizuri kwenye hili,

Na hapo nimeongelea madawa kwenye mahindi pekee, rudi kwenye nyanya, matikiti nk, huko ndio usiseme, dawa inayomwaga huko huwezi amini kwamba inaingia tumboni kwa binadamu.

Mimi nashauri wadau wa kilimo wasikilizwe, ianzishwe bank ya mbegu zetu za asili kuliko kutegemea hizi za kisasa tunazoletewa maana wakati mweingine kuzitunza ni ngumu sana kwasababu ya kushambuliwa na wadudu.

Halafu kama hatuwaamini Mabeberu ( Bill Gates) kwenye chanzo za COVID kwa nini tunahamasisha wakulima wetu watumie mbegu zao, Rejea matumizi ya mbegu zilizofanyiwa GMO huku nako kuna madhara mengi zaidi.
Hizo GMO ilikuwa enzi za serikali dhaifu. Sasa hivi zimepigwa ban.
 
Wakulima Walime, Watanzania tule kwani Kenya tu ndo wanamatumbo peke Yao?.. Viongozi wetu sio wajinga na sisi Watanzania tupunguze uoga, changamoto kidogo tu mshaanza kupost Mabandiko, Kama hawanunui wao tutauza kwingine watakapo hitaji, ikishindikana tuuziane humuhumu Maisha yaendelee mi hua hainingii akilini kununua debe la Mahindi 20,000 wakati mengine yanapelekwa Kenya huko.. hii Ni Vita ya kiuchumi na Kenya wameshaona Kuna uwezekano wakageuka koloni la Tanzania.. Punguzeni Uoga Vijana, maendeleo hayaji bila changamoto.. Sengwile Makamanda!!
We bwege hivi unafahamu gharama za kilimo wewe?

Unafahamu kwa kiasi gani mkulima anapata hasara kwa kuuza mahindi 5000 debe au 40000 kwa gunia?

Unaijua uchungu na msongo wa mawazo unaowakumba wakulima nchi hii?

Je, unafamu kwamba mbolea hasa DAP imepanda toka 57000 hadi 65000 na ruzuku ilifutwa mara baada ya utawala huu kuingia madarakani?

Unataka wote tuje mjini tuwe machinga wanyonge hapo dar?

Mnatia hasira kweli, jaribu kuongea haya mbele ya mkulima uone.
 
kwani unalima kwa ajiri ya kenya!!!

unafikiri kenya wakianza kulima na wao utamuuzia nani mahindi??
Mkuu, nowadays kizazi kinazidi kuwa soft minded. Kuna soft minds zimejaa mitandaoni humu vichwani hakuna kitu, empty heads.

Hawa wapuuzi wangekuwa wanajua business war baina ya China na US kwenye bidhaa za chakula wasingekuwa wanatuonesha utaahira wao humu. Magu alipowatafutia wakulima wetu hilo soko mwaka jana walikuja na hoja kuwa tusiwalazimishe kununua unga tuwape tu mahindi mazima mazima. Hii ni baada ya naibu waziri Bashe kuwaomba wakenya wakubali mahindi tuwasagie sisi kwenye vinu vya NMC.

Leo badala ya kushukuru hata kwa hilo soko lililotafutwa na hiyo hiyo serikali vinayodai haijui diplomasia vijinga hivi vinakuja na matusi kwa serikali. Hivi vikichanjwa na chanjo ya corona si ndiyo vitakuwa vizombi kabisa.
 
Jifunze diplomasia na elimu ya biashara ndipo utoe challenge,la sivyo,kaa kimya!
Hiyo hiyo diplomasia ndiyo ilipelekea kupatikana hilo soko mwaka jana tu hapo. Yawezekana kweli hayo mahindi yana hiyo sumu kuvu kweli. Mimi kama mkulima najua hilo ni tatizo na ndiyo sababu serikali inajenga vihenge vya kisasa ili kulitatua hilo tatizo. Msifikiri kwamba serikali haijui.
 
Mkuu, nowadays kizazi kinazidi kuwa soft minded. Kuna soft minds zimejaa mitandaoni humu vichwani hakuna kitu, empty heads.

Hawa wapuuzi wangekuwa wanajua business war baina ya China na US kwenye bidhaa za chakula wasingekuwa wanatuonesha utaahira wao humu. Magu alipowatafutia wakulima wetu hilo soko mwaka jana walikuja na hoja kuwa tusiwalazimishe kununua unga tuwape tu mahindi mazima mazima. Hii ni baada ya naibu waziri Bashe kuwaomba wakenya wakubali mahindi tuwasagie sisi kwenye vinu vya NMC.

Leo badala ya kushukuru hata kwa hilo soko lililotafutwa na hiyo hiyo serikali vinayodai haijui diplomasia vijinga hivi vinakuja na matusi kwa serikali. Hivi vikichanjwa na chanjo ya corona si ndiyo vitakuwa vizombi kabisa.
Soko liko wapi? Hivi unafahamu bei ya mahindi kwa Sasa? Kwanza umewahi kulima? Kuna ruzuku yoyote toka serikalini? Unazijua kauli za kisiasa wewe? Kama soko ndio hilo kwa bei hizi basi bora yauzwe mahindi ghafi tusing'ang'ane na unga wakulima wanalia huku, hebu tembelea wakulima kwanza uone kama haya ulioandika hapa yanaleta maana akilini.
 
Ina maana mnalima ili muwauzie Kenya? Basi nyie mnaolima ni wajinga
wewe ndio hujitambui. Tunalima ili tutumie na nyingine tuuze kwa jirani anayehitaji na mwenye kununua kwa bei kubwa mathalan gunia ya mahindi 90,000 na sio 45,000 tunayouzia hapa tz. wewe hujawahi kulima huelewi chochote. soko likifa lazima tusikitike. KAA KIMYA SISI TUMEPATA PIGO. Nashauri tupate dawa nyingind tofauti za kuhifadhia mahindi ili tuendeled na SOKO la jirani. Kwao tunanunua mpaka colgate ya kupigia mswaki na vitu vingi sana vya viwandani hata soseji za kutokana na ng'ombe zetu tunazouza kule NAROK. Wazuie na hizo tuone kama soseji watauza tena. Cha ajabu bei yao ya kununua mazao yetu kule ni ya juu kuliko hapa ndio kisa cha kuwauzia.
 
ww fala kilimo cha tz wateja wetu wakubwa ni kenya
mipaka ikifunguliwa gunia la mahindi linauzwa hadil 120k na sometimes wanalifata hap hapa
tangu wafunge gunia linacheza 30-50k
Nakuita mjinga, kama unalima ili ukawauzie Kenya endelea kulima
 
Ina maana mnalima ili muwauzie Kenya? Basi nyie mnaolima ni wajinga
Unaandika hivi kwa vile unafaidika na hao unaowatetea, ungekuwa wewe ndie mkulima na umekula hasara kama mwaka huu hakika NAKUAPIA usingeandika hii shombo. Mnatia aibu sana kushabikia kila kitu. Kwanini mnalemaa namna hii mkiwa mnatetea makosa ya wazi ya serikali yenu.
 
We bwege hivi unafahamu gharama za kilimo wewe?

Unafahamu kwa kiasi gani mkulima anapata hasara kwa kuuza mahindi 5000 debe au 40000 kwa gunia?

Unaijua uchungu na msongo wa mawazo unaowakumba wakulima nchi hii?

Je, unafamu kwamba mbolea hasa DAP imepanda toka 57000 hadi 65000 na ruzuku ilifutwa mara baada ya utawala huu kuingia madarakani?

Unataka wote tuje mjini tuwe machinga wanyonge hapo dar?

Mnatia hasira kweli, jaribu kuongea haya mbele ya mkulima uone.
Wewe ni mjinga na bahati mbaya hujijui Kama ni mjinga
 
Unaandika hivi kwa vile unafaidika na hao unaowatetea, ungekuwa wewe ndie mkulima na umekula hasara kama mwaka huu hakika NAKUAPIA usingeandika hii shombo. Mnatia aibu sana kushabikia kila kitu. Kwanini mnalemaa namna hii mkiwa mnatetea makosa ya wazi ya serikali yenu.
Wewe ni mjinga, hakuna jina lingine zuri la kukupa
 
Daah mijadala kama hii ilishapotea kabisa hapa jf ilibaki mijadala ya ccm na wenzao chadema na nani anatembea na nani. safi sana wachangiaji wote. tuendelee kuelimishana kwa nguvu za hoja.
 
Nakumbuka 2012 kulikua na watanzania wengi sana wanaingia Kenya kufungasha biashara mitaa ya wasomali Eastleigh toka 2015 sijaenda tena. Bado wanasafiri tena kweli?
 
Wewe ni mjinga na bahati mbaya hujijui Kama ni mjinga
Unaijua tofauti ya ujinga na upumbavu? Basi wewe ni mpumbavu hakuna lolote unalojua na hutojua kamwe. Upumbavu wako umejidhirisha kwa kushindwa kujibu maswali yangu. Kwa heri endelea kutetea kibarua chako maana bila hivyo mkono hautakwenda kinywani.
 
Back
Top Bottom