Nasikitishwa na uhusiano wetu na Kenya, unaumiza wakulima na wafanyabiashara

Nasikitishwa na uhusiano wetu na Kenya, unaumiza wakulima na wafanyabiashara

Mleta mada hujielewi bunge la kenya limegoma kusaini mkataba kati ya uungereza na Kenya wa kuuza bidhaa za kilimo uingerez unaojulikana kama EPA sababu ni wa kinyonyaji unaumiza wakulima wa kenya.Bunge la uingereza lilisaini lakini kulikwa na kipengele cha kusema bunge la kenya halitakuwa na mamlaka ya kubadilisha huo mkataba au kuridhia

Tanzania huo mkataba wa EPA bunge letu liligoma na nyie michadema kwa ujinga wenu mkatukana sana humu sasa Bunge la kenya limegoma kuridhia

Ni sahihi chadema kuwa mlipigwa chini sio wazalendo kabisa.Bunge la kenya wabunge wa chama tawala na upinzani wamesimama kama kitu kimoja kukataa mkataba Wa EPA wa kibiashara kati ya Kenya na Uingereza wakati sisi mivyama koko kama Chadema haikusimama na wabunge wa CCM kupinga!!!
 
Acha ujinga maana hata tuta la viazi huna. Leo Rukwa na Katavi mahindi gunia 30000 na mengine yanakomaa shambani. Tunapigwa pin ya soko unasema viongozi wako siyo wajinga!? Viongozi gani unaoongelea? Hawa wanaojali posho za vikao kuliko ustawi wa wakulima!?!
Sasa wewe mbona unakuwa mjinga sana?

Kwani huli suala kosa ni la viongozi wa wapi?

Umesikia selikali ya tz au Uganda ikizuia mtu kupeleka mahindi kenya?
 
Kosa la Magufuli kwenye hili ni nini?

Kwamba uhusiano na Kenya siyo mzuri?
Crimea!!! Hata hilo linakupa shaka? Hamkuchoma kuku wao? Mbona before Magufuli haya mambo ya ajabu ajabu hatukuyaona?
 
Crimea!!! Hata hilo linakupa shaka? Hamkuchoma kuku wao? Mbona before Magufuli haya mambo ya ajabu ajabu hatukuyaona?
Wewe, kabla ya Magu wakenya walikuwa wanawatia vidole mnakaa kimya, Magu kasema hapana ndio maana unaona wanavyorusha rusha miguu.
 
Ninachokiona mm Kuna gepu sehemu wazalishaji malighafi, kisha wasomi, kisha wafanyabiashara, kisha serikali inafunga mwisho Sasa kwenye nchi za Africa wasomi ni Kama gepu lakuto kukamilishaa dhumuni. Watu mnajifanya Kama kuwaonea huruma wakulima Kama kigezo cha kuilaumu serikali je serikali inamakosa ? Je wewe kama msomi wa humu jf unamsaidiaje huyu mkulima ukiachana hii kazi ya kutoa report ambayo nikazi ya mfanyabiashara ndo inabidi azitoe kwa serikali.
 
Wakulima Walime, Watanzania tule kwani Kenya tu ndo wanamatumbo peke Yao?.. Viongozi wetu sio wajinga na sisi Watanzania tupunguze uoga, changamoto kidogo tu mshaanza kupost Mabandiko, Kama hawanunui wao tutauza kwingine watakapo hitaji, ikishindikana tuuziane humuhumu Maisha yaendelee mi hua hainingii akilini kununua debe la Mahindi 20,000 wakati mengine yanapelekwa Kenya huko.. hii Ni Vita ya kiuchumi na Kenya wameshaona Kuna uwezekano wakageuka koloni la Tanzania.. Punguzeni Uoga Vijana, maendeleo hayaji bila changamoto.. Sengwile Makamanda!!
Tz ni hatari sana, waweza kuta wew ni graduate
 
nyie mnaoshabikia kila UJINGA wa viongozi wanapoboronga mnatia hasira sana!.

Anyway, ukishaolewa ukaacha utegemezi...akili itakukaa sawa!.
Utegemezi hawezi acha mana atakuwa anamtegemea mume wake
 
Nilitamani kuanzisha uzi kuhusu hili suala lakini nashukuru kwa bandiko hili maana limelenga kile nilichotaka kusema.

Binafsi nimekuwa mdau wa kilimo kwa muda mrefu sana, kuanzia kulima mpaka kushiriki makongamano mbalimbali yanayohusiana na sekta ya kilimo na kuna hoja kadhaa ambazo wakulima wamekuwa wakizitoa kwa Serikali lakini kutofanyiwa kazi na hii sasa ndio majibu yake, japo inabidi kutafiti zaidi kama kweli Kenya wanasema ukweli au ndio VITA YA KIUCHUMI.

Hoja kubwa ambayo imekuwa ikitoka mara kadhaa ni kuhusu suala la mbegu, wadau wameshauri mara nyingi turudi kwenye mbegu zetu za asili maana hizi tunazoambiwa za kisasa zina changamoto nyingi sana, mojawapo ni hii ya kushambuliwa na wadudu hali inayopelekea wakulima kutumia madawa mengi sana ili kuweza kulinda mazao yao, na hili nimelishuhudia kwa macho yangu, sasa kwa hali hii tutajiteteaje kwamba mahindi yetu hayana sumu?

Wakulima watanielewa vizuri kwenye hili,

Na hapo nimeongelea madawa kwenye mahindi pekee, rudi kwenye nyanya, matikiti nk, huko ndio usiseme, dawa inayomwaga huko huwezi amini kwamba inaingia tumboni kwa binadamu.

Mimi nashauri wadau wa kilimo wasikilizwe, ianzishwe bank ya mbegu zetu za asili kuliko kutegemea hizi za kisasa tunazoletewa maana wakati mweingine kuzitunza ni ngumu sana kwasababu ya kushambuliwa na wadudu.

Halafu kama hatuwaamini Mabeberu ( Bill Gates) kwenye chanzo za COVID kwa nini tunahamasisha wakulima wetu watumie mbegu zao, Rejea matumizi ya mbegu zilizofanyiwa GMO huku nako kuna madhara mengi zaidi.

Lakini mbegu za kienyeji hutoa mazao hafifu balaa
 
We unaeandika utumbo huu ni mkulima au umejiskia tuu uandike!!?
Unajua shida tunayoipata sisi mipaka ikifungwa mbeha wewe!!?

Alafu nmekumind kishenzi yaan.

Kwa sababu ya watu kama hao pengine ndio maana nchi yetu ni masikini miaka nenda rudi

Usishangae hapo ni mtumishi wa serikali hana uchungu kabisa na ujasiriamali
 
Labda nikukumbushe tu mwandishi wa hii habari kwamba,''Kenya haijawahi kuwa rafiki wa kweli wa Tanzania,toka enzi na enzi''.Wakati Tanzania ikisadiana na nchi za kusini mwa Africa ,kwenye vita vya ukombozi,Kenya ilikuwa ikifanya biashara na Makaburu wa Afrika Kusini.Makaburu walikuwa ni adui yetu namba moja huko kusini mwa Afrika.Kuna makaburi mengi sana ya ndugu zetu huko Msumbiji na Angola.Ukiondoa ujirani wa mipaka,Tanzania na Kenya ,ni paka na panya.Labda Tanzania na yenyewe ilipe kisasi kwa Kenya kuacha kununua mahindi,sisi nasi tuache kununua bidhaa za wakenya.Sasa hivi ulimwengu ni kama kijiji tunaweza agiza bidhaa nchi za Asia,na tukaachana na hizi za majirani zetu.Kama Mbwai iwe mbwai!
 
Mtu anaefikiria kujikwamua kwenye umasikini hawezi kufikiria kutanguliza chuki au ushabiki shabiki kazini

Kilimo ni kazi
 
Na biashara haina uhusiano na uadui

Japan na China ni maadui tangu na tangu ila kajifunze wanavyouziana vitu vya thamani ya mamia ya matrilioni
 
Kati ya majirani zetu ambao wanapaswa wawe soko letu kubwa la bidhaa za kilimo na biashara nyingine ni Wakenya.

Ila Kati ya watu ambao tumekuwa tukiishi nao Kama maadui kwa miaka sita Sasa ni Kenya.

Nchi inayotaka kuinua wakulima na wafanyabiashara uwekeza kwenye diplomasia ya eneo lilipo soko. Sisi sijui Wataalamu wa mahusiano wanaona Nini huko ofisini Hadi kila siku waibue migogoro na Kenya.

Sasa hivi wenzetu wanaona ni vyema waagize chakula kutoka Brazil na Mataifa mengine ya mbali kuliko kutegemea Tanzania, matamko yamekuwa mengi na yasiyo na tija kwa ustawi wa wakulima wetu.

Na hii imepelekea hata uhusiano wetu na nchi nyingine za Afrika Mashariki uwe na mashaka.... protocol ya free movement of goods and services imebaki kuwa kwenye makaratasi tu. Tubadilike, tukitaka kukua kiuchumi tuwekeze kwenye mahusiano na waliotutangulia kiuchumi, tujifunze kwa china na Marekani.
Uhusiano na Kenya ni mbaya enzi na enzi walishachukua mpaka ndege zetu wakati wa EAC ya mwanzo labda kama hujui historia yetu na Kenya. Saa hizi Kenya wanaumia sana baada ya kuwabana wizi wa madini yetu ya Tanzanite na Dhahabu pia kuwanyima ajira hapa nchini. Tutawanyoosha tu pamoja na nyinyi vibaraka wao mliokuwa mnafaidika na wizi huo hatutarudi nyuma.
 
Wataalam wetu wa kilimo/mifugo vjijijini hawana msaada kwa wakulima/wafugaji. Hawana mpango kazi,hawatusaidii wakulima/wafugaji kwa lolote. Afadhali hivyo vyeo vifutwe,, wengi wamefungua viduka vya pembejeo, lakini ni watumishi wa serikali,wanalipwa mishahara
 
Na biashara haina uhusiano na uadui

Japan na China ni maadui tangu na tangu ila kajifunze wanavyouziana vitu vya thamani ya mamia ya matrilioni
Kama biashara haina uadui mbona Nyerere alipiga marufuku bidhaa za Kenya kuingia Tanzania.Kama kuingia ziliingia kwa magendo?
 
Mtu anaefikiria kujikwamua kwenye umasikini hawezi kufikiria kutanguliza chuki au ushabiki shabiki kazini

Kilimo ni kazi
Kwa hiyo wewe unataka wakenya wafanye wanachotaka wao siyo?? Subiri tunapiga stop bidhaa zao zote kuja TZ tuone nani ataumia zaidi.
 
Wataalam wetu wa kilimo/mifugo vjijijini hawana msaada kwa wakulima/wafugaji. Hawana mpango kazi,hawatusaidii wakulima/wafugaji kwa lolote. Afadhali hivyo vyeo vifutwe,, wengi wamefungua viduka vya pembejeo, lakini ni watumishi wa serikali,wanalipwa mishahara
Wewe siyo mkulima kwenda zao huko.
 
Back
Top Bottom