Tafuta data za horticulture na top ten producers and exporters wa avocado, macadamia, sugar snaps, green peas, mangetouts, french beans etc haya ni mazao hot soko la ulaya.
Tea, coffee, cotton, mahindi nk ni mazao yasiyo na tija tulishaachana nayo wewe upo dunia ya wapi?
Unaposema wanaolima ni wazungu kumbe bado upo dunia ya kuangalia skin color
Afadhali kidogo hapaumekuwa 'specific', na tunaweza kuanza mjadala wenyewe.
"Horticulture", (French beans, n.k.) ndio ni kweli hii sehemu imeinukia na kuchangia kwa kiasi kikubwa katika pato la taifa hilo, nadhani inaweza kuwa namba 3 hivi nyuma ya utalii na sekta nyingine; lakini huwezi kamwe kusema chai kwa Kenya ni zao la zamani. Ukiondoa chai uchumi unaporomoka.
Tunarudi hapo hapo, ni wazungu/wawekezaji wa nje zaidi wanaojihusisha na sehemu kubwa ya haya.
Sio swala la "kuangalia 'skin color'"; hata kama wawekezaji hao wangekuwa weusi toka nje ya nchi na kubeba faida kubwa na kuipeleka kwao na kuwaacha wananchi wa hapo wakishikilia masalia, bado ningesema hivyo.
Swala hapa ni nani mnufaika mkubwa.
Hapo unaposema "Tea, coffee, cotton, mahindi, n.k.) ni mazao yasiyo na tija", unaelewa maana ya hili neno "TIJA"?
Hiyo "horticulture" kwani ni kitu gani hadi kiwe na 'tija' kuliko mazao hayo unayoyadharau?
Mwisho: hata kwa hiyo 'horticulture' unayoipapatikia, Kenya haina uwezo wa kuzizidi nchi nyingine katika uzalishaji wake. Kwanza sehemu ya mazao hayo huyakusanya toka nje ya Kenya na kuyafunganisha kama yanatokea Kenya. Sasa Kenya wanapata taabu sana walaji wa mazao hayo wanaposisitiza vyanzo vyake vijulikane.
Na hapa ni swala la muda tu, miaka miwili mitatu Kenya hawana tena tambo juu ya hiyo 'horticulture', kwa sababu nchi nyingine zenye hali bora zaidi watakuwa wazalishaji wakubwa zaidi.