Nasikitishwa na uhusiano wetu na Kenya, unaumiza wakulima na wafanyabiashara

Nasikitishwa na uhusiano wetu na Kenya, unaumiza wakulima na wafanyabiashara

Apple, tende na mazao mengine yaliyopo sokoni ambayo hatupimi Tz, unafikiri ni kwanini? Kilimo ni biashara kama zilivyo biashara nyingine.
nimekuuliza unalima kuuzia wakenya peke yake au?

wao wametoa sababu ya kusitisha ununuzi wa mazao yetu,nikuulize ni kweli mnaweka sumu kwenye mahindi??
 
Kaka unapotoa hoja fikiria maumivu wanayoyapata wakulima na wafanyabiashara, pia tunapaswa kuelewa kuwa Kenya ni soko kubwa la zao letu la mahindi, kwahiyo wewe ni muumini wa kuzalisha kwa matumizi ya nyumbani tu?
 
Mkuu, katika biashara unaanza kumuuzia mteja wa karibu ilimradi kuwe na masilahi. Biashara ya mazao usipouza Africa utauza wapi tena. Masoko nje ya Africa ndio wakulima wakubwa tena kilimo cha kisasa chenye ruzuku ya serikali.

Pia kumbuka Kenya tupo nae kwenye Jumuiya ya Kikanda hivyo masuala ya tariffs hayapo. Ukusema uuze domestically, utamuuzia nani wakati asilimia kubwa ya wananchi ni wakulima?

Serikali ikischa kubalance siasa na uchumi tutaona dunia inatuonea.
 
Kenya wmamefanya maamuzi as a sovereign nation kununua bidhaa Mexico, kwanini tulalamike kama Kenya sio taifa huru lenye maamuzi yake.

Kumbukeni ni mahindi tuu wameagiz a mexico, asilimia kubw a ya matunda , mchele n.k wananunua Bongo hivyo tujiongeze.

Hata sisi Tanzania tunaweza kuamua kuanzia sasa tusinunue sabuni zaona bidhaa zao za viwnandani tukaagiza South Africa , ni maamuzi tuu
 
Kilimanjaro kuna kilimo cha tangawizi na vitunguu, mazao ambayo yana soko Kenya..kwa muda sasa soko la hayo mazao limeyumba kweli..kiwanda chenyewe cha tangawizi huko Miamba kina taralila sio za kitoto. Dahhh!!
Wakulima wasiwe na shaka, serikali ya magufuli itanunua tangawizi zoooote kama ilivyo nunua coroshow za mtwara
 
ww fala kilimo cha tz wateja wetu wakubwa ni kenya
mipaka ikifunguliwa gunia la mahindi linauzwa hadil 120k na sometimes wanalifata hap hapa
tangu wafunge gunia linacheza 30-50k
Tunasema 70% ya watanzania ni wakulima sasa inakuwaje hiyo 70% inashindwa kujilisha yenyewe na hiyo 30% mpaka tuzuie kusafirisha nje?

Kenya wanamasoko makubwa duniani kupitia bilateral agreements kwahiyo hawawezi kukidhi mahitaji na hivyo kulazimika kuja tz kujazia order zao na sisi kunufaika. Uhuru alisaini bonge la dili na china mwaka jana la kupeleka tani laki moja za parachichi china kila mwaka wakati sisi tz wiki iliyopita kontena za parachichi zimetupwa jalalani south africa kwa kutokukidhi matakwa Kati ya nchi 2.

Mwanzoni wazungu walikuwa wananunua kilo 1 ya parachichi kwa mkulima kwa shilingi 400 baada ya wakenya kuingia bei imepanda mpaka sh 2000 kwa kilo na kulazimisha wazungu nao wapandishe bei kwasababu hawapati mzigo tena.
Viazi ilikuwa 28,000 mkenya akiingia bei mpaka 45,000 na kuwalazimu wengine nao kutoa offer ya juu
Maharage debe 28,000 mkenya akifika anatoa mpaka 45
Mahindi, matunda na nafaka nyingine mwendo ni ule ule

Mkenya anafaida kubwa kwa mkulima wa tz kuliko mtz na usishangae siku tukija kuwa na rais mmoja afrika mashariki wakulima wa tz tukamchagua mkenya tukamuacha mtz ili akili ziwakae sawa
 
Wakulima Walime, Watanzania tule kwani Kenya tu ndo wanamatumbo peke Yao?.. Viongozi wetu sio wajinga na sisi Watanzania tupunguze uoga, changamoto kidogo tu mshaanza kupost Mabandiko, Kama hawanunui wao tutauza kwingine watakapo hitaji, ikishindikana tuuziane humuhumu Maisha yaendelee mi hua hainingii akilini kununua debe la Mahindi 20,000 wakati mengine yanapelekwa Kenya huko.. hii Ni Vita ya kiuchumi na Kenya wameshaona Kuna uwezekano wakageuka koloni la Tanzania.. Punguzeni Uoga Vijana,. We so bure
 
Wakulima Walime, Watanzania tule kwani Kenya tu ndo wanamatumbo peke Yao?.. Viongozi wetu sio wajinga na sisi Watanzania tupunguze uoga, changamoto kidogo tu mshaanza kupost Mabandiko, Kama hawanunui wao tutauza kwingine watakapo hitaji, ikishindikana tuuziane humuhumu Maisha yaendelee mi hua hainingii akilini kununua debe la Mahindi 20,000 wakati mengine yanapelekwa Kenya huko.. hii Ni Vita ya kiuchumi na Kenya wameshaona Kuna uwezekano wakageuka koloni la Tanzania.. Punguzeni Uoga Vijana, maendeleo hayaji bila changamoto.. Sengwile Makamanda!!
Mawazo kama haya ndio huwa mnamshauri matokeo mambo yanawatokea puani kama korosho

Kenya ina viwanda vingi sana kuliko tanganyika kama hulijui hilo kenya ina connection kubwa sana ya biashara kuliko tanzania ndio maana soko kubwa la nafaka na mazao mengi lipo kenya
 
Wakulima Walime, Watanzania tule kwani Kenya tu ndo wanamatumbo peke Yao?.. Viongozi wetu sio wajinga na sisi Watanzania tupunguze uoga, changamoto kidogo tu mshaanza kupost Mabandiko, Kama hawanunui wao tutauza kwingine watakapo hitaji, ikishindikana tuuziane humuhumu Maisha yaendelee mi hua hainingii akilini kununua debe la Mahindi 20,000 wakati mengine yanapelekwa Kenya huko.. hii Ni Vita ya kiuchumi na Kenya wameshaona Kuna uwezekano wakageuka koloni la Tanzania.. Punguzeni Uoga Vijana,. We so bure
Wewe ni mjinga sana kenya igeuke koloni la tanzania??
 
Wakulima Walime, Watanzania tule kwani Kenya tu ndo wanamatumbo peke Yao?.. Viongozi wetu sio wajinga na sisi Watanzania tupunguze uoga, changamoto kidogo tu mshaanza kupost Mabandiko, Kama hawanunui wao tutauza kwingine watakapo hitaji, ikishindikana tuuziane humuhumu Maisha yaendelee mi hua hainingii akilini kununua debe la Mahindi 20,000 wakati mengine yanapelekwa Kenya huko.. hii Ni Vita ya kiuchumi na Kenya wameshaona Kuna uwezekano wakageuka koloni la Tanzania.. Punguzeni Uoga Vijana,. We so bure
Taifa lina hasara kubwa kuwa na watu wa aina hii. Hivi unajua gharama za kulima wewe? Ulishawahi kujiuliza ni kwanini mkulima wa kenya na nje ni watu wa vipato vya juu na mkulima wa tz anaongoza kwa umasikini
 
Kitu kimoja ambacho wengi hawakielewi sio mazao yote wanayonunua Kenya yanaenda kenya, kiasi kikubwa cha mahindi yanayonunuliwa yanaenda kuuzwa South Sudan.

Kinachotakiwa kufanywa kama nchi ni kufatilia kama sababu walizotoa kenya ni za kweli kama sio za kweli basi waangalie masoko mengine kama Sudani kusini kwani Kenya hajaanza kuifanyia vitko Tanzania leo bahati mbaya wengine kwa kuichukia serikali wapo tayari kuunga kitu chochote ili mradi kinapingana na msimamo wa chakula.

Usalama wa nchi yoyote unaanzia kwanza kwa kujitosheleza kwa chakula ukishakuwa na chakula cha kutosha watu watakuwa na nguvu ya kufanya kazi na watoto watakuwa na akili ya kusoma ndio maana Hashim Rungwe alikuja na sera ya wali na nyama ila kwa uelewa mdogo wa watu wengi waliishia kwenye ushabiki.
 
ninatumain katika Afrika sasa Tanzania ndo nchi inayoongoza kwa watu wasio na furaha na nchi yao.
 
Back
Top Bottom