Nasikitishwa sana na majibu ya dharau ya Rais Magufuli kwa Watanzania

Nasikitishwa sana na majibu ya dharau ya Rais Magufuli kwa Watanzania

""hatuna shida na maiti yake akishakufa tunaweza kumtupa hata baharini samaki wapate chakula."

Nimeipenda tu hii kauli, mtu hudhaminiwa akiwa hai na mali akisha kufa/ kufirisika ata shikamoo hapewi anaitwa kichaaa
 
Kama mnategemea mabadiliko mwafa! Tena awamu ya pili mtakachokipata mtaombapo! Jueni kabisa awamu ya pili ni ya mwisho hana cha kupoteza kwa atakachowafanya ni yeye tu ndiye anajua! Ni wa kupiga chini huyu!

Tz. Iko vizuri na ataipeleka vizuri. Sijui wewe unazungumzia aina gani ya maendeleo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanaounga Raisi Magufuli wako sawa na wale wanaotaka kujua kisa cha Jemedari Mkuu kujizatiti huko Chato home town for 45 days nao wanahitaji majibu pia.
Kwanini wanahitaji majibu kwa kuwa Raisi anawajibika kwa wananchi wake na hiyo ndio katiba yetu ilivyo.
 
Yani watu mnaongea sana vitu vingi visivyo na maana kiasi mnaacha na mambo yenu ya maingi kwa umbea na laana zenu tu.

Kila kitu ni kulalamika tu utadhani matoto madogo, kila mtu ni wa MUNGU na MUNGU anamjua, huwapa watu wote karama. Ridhiki kadri ya atakavyo, nyie mnadhani Magufuli yupo tu kajiweka bila MUNGU kujua!!

Kutwa kumsema RAIS wa nchi sijui mmebeba wehu vichwani mwenu! Tafuteni na nyinyi kwenda Ikulu kwa hekima na kumtegemea MUNGU, maana historia ya mzee mnaijua safari nzima ya uongozi wake ila mnapotezea tu vichwani mwenu kwa sababu ya uroho wa mamlaka

JAH Rastafari Morning Africa.Trust JAH respect nature
Wewe ndio mwehu kabisa, kiongozi yeyote anachaguliwa kutatua changamoto za anao waongoza.
Pia utambue kiongozi anachaguliwa kulinda masilahi ya wengi sio ya wachache, na kingine binadamu kusemwa ni kawaida kwani akisemwa anapungukiwa nn?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha Pombe wewe.. Analalamikiwa mwingine unachanganya vingine, kwani umeambiwa huyo Raisi Ni wa CCM peke yake.. ushangai hata COVID-19 inaua wabunge na Viongozi wa CCM peke ake..

Kuna siku CCM itangoka pia na mizizi yake, Alafu Mali zetu Watanzania tutazirudisha hata Kama kutoka kwa Vitukuu vyenu.. Vizazi vyenu vitaishi kwa aibu na Makaburi yenu yatasahaulika Kama ya Wanyanganyi na Wevi.
Watumishi wa umma imekula kwenu! Ile ahadi mliyopewa ya kuongezewa mishahara kabla ya kipindi cha miaka 5 kwisha imeota mbawa! Hii recession itachukua miaka mingine 5 kufufuka. Fanyeni uamuzi sahihi 2020!
 
Tumchague nani Sasa Mkuu, babaako ama?
Mbna mna kashfa nyingi kuliko maneno ya kujenga.. Na ndio maana hata Upinzani unaonekana Kama vile hauna Vijana wachapakazi kumbe Umefukiwa na wachache wenye visasi na mfumo tawala na njaa za madaraka.
 
Serikali haina vipaumbele vya Taifa. Yaani nn tunahitaji kwa sasa. Mf badala ya kukimbilia kununua ndege tungeanza na viwanda vyenye kuzalisha ajira kwa wingi na faida kwa Serikali. Kisha faida ile itumike baadae kununua ndege. Badala kukimbilia kujenga ukata kule Mirerani tungefufua kiwanda cha magurudumu kilichoko kule kule Arusha. Au kingine kipya popote pale nchini. Faida ile pia tukazungushe ukuta kule Mirerani.

Sent using Jamii Forums mobile app
Utajengaje viwanda wakati huzalishi umeme wa kutosha? Je utashindanishaje bidhaa inayozalishwa na umeme unaonunuliwa kwa unit moja kwa 136 tsh na ile inayozalishwa kwa unit moja kwa 20 tsh? na hiyo ndo sababu kubwa ya kufa kwa viwanda vikubwa kama Mutex, G/tires nk. Wawekezaji wengi hushindwa kutokana na bidhaa zinazozalishwa kishindwa kushindana na zilizopo sokoni kwa bei.

Mpaka kuwe na sustainable sources of Energy mfano endapo bwawa la kufua umeme la Nyerere kule Rufiji labda ndo linaweza kutoa suruhisho la hayo yote.

Pia Ikiwa tumeamua kufufua shirika la ndege na likawa advertised kama mashirika mengine mf Ethiopia huenda tukapata another source of national income na si lazima hizo ndege apande Wewe au bibi yako.
 
Watu wanashangaa kwanini anahamisha makazi ya Rais kwenda anakotaka yeye anajibu" kwani nikifa nitazikwa wapi?”

Yani majibu kama haya ni ya dharau sana kwa watu makini! Anasahau kwamba sisi hatuna shida na maiti yake akishakufa tunaweza kumtupa hata baharini samaki wapate chakula.

Rais Magufuli nilikuwa nampenda sana ila anachokifanya kuongoza nchi utadhani ni mali ya familia yake nimetokea kumchukia sana.

Anawatesa watumishi wa umma, anawatesa wapinzani wake, anaamua atakacho kwa sababu anajua Watanzania ni wanyonge kama anavyowaita.

Mungu wapiganie Watanzania, wanaburuzwa, mwenye nguvu anawatesa sana. Rais Magufuli nakuombea ubadilike, wewe ni binadamu siyo Mungu
Magufuli anajiamimi yeyeye ni super human kuwa hakosei. Lakini maamuzi yake yote aliyokwisha fanya maishani ni FAILURES tu. Mfano kidogo huu hapa;
1. Kushika Meli ya wavuvi wa Thailand kulikosababisha tukashindwa kesi
2.Ununuzi wa kivuko cha MV Bagamoyo ambacho kilipaswa kiwe kinasafiri kwa Dak 45 kutoka DSM- Bagamoyo instead kikawa kinatumia masaa 2
3. Uuzaji wa nyumba za Serikali hadi kumuuzia mdogo wake Musa Magufuli na kimada wake
4. Kuwakamata wauzaji wa sukari mwaka 2016 kwa kisingizio cha ukwepaji kodi. Mpaka sasa Sukari imetoka kwenye Tsh 1,800 kwa kilo mwaka 2015 hadi Tsh 3,800 na haipatikani
5. Kuvuruga biashara ya korosho mwaka 2016 kwa kisingizio cha kwamba makampuni yanawanyonya wakulima. Korosho bado haijatengamaa

Haya ni machache tu lakini Magufuli hashauriki na mtu wala hana muda wa kushauriwa. Kimsingi kichwa chake hakina nafasi ya kutunza ushauri. Yeye akiamua anakuwa ndiyo ameamua kwa hiyo akipotea anapotea kweli kweli.
 
Yani watu mnaongea sana vitu vingi visivyo na maana kiasi mnaacha na mambo yenu ya maingi kwa umbea na laana zenu tu.

Kila kitu ni kulalamika tu utadhani matoto madogo, kila mtu ni wa MUNGU na MUNGU anamjua, huwapa watu wote karama. Ridhiki kadri ya atakavyo, nyie mnadhani Magufuli yupo tu kajiweka bila MUNGU kujua!!

Kutwa kumsema RAIS wa nchi sijui mmebeba wehu vichwani mwenu! Tafuteni na nyinyi kwenda Ikulu kwa hekima na kumtegemea MUNGU, maana historia ya mzee mnaijua safari nzima ya uongozi wake ila mnapotezea tu vichwani mwenu kwa sababu ya uroho wa mamlaka

JAH Rastafari Morning Africa.Trust JAH respect nature
Umetumwa sio bure

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Magufuli anajiamimi yeyeye ni super human kuwa hakosei. Lakini maamuzi yake yote aliyokwisha fanya maishani ni FAILURES tu. Mfano kidogo huu hapa;
1. Kushika Meli ya wavuvi wa Thailand kulikosababisha tukashindwa kesi
2.Ununuzi wa kivuko cha MV Bagamoyo ambacho kilipaswa kiwe kinasafiri kwa Dak 45 kutoka DSM- Bagamoyo instead kikawa kinatumia masaa 2
3. Uuzaji wa nyumba za Serikali hadi kumuuzia mdogo wake Musa Magufuli na kimada wake
4. Kuwakamata wauzaji wa sukari mwaka 2016 kwa kisingizio cha ukwepaji kodi. Mpaka sasa Sukari imetoka kwenye Tsh 1,800 kwa kilo mwaka 2015 hadi Tsh 3,800 na haipatikani
5. Kuvuruga biashara ya korosho mwaka 2016 kwa kisingizio cha kwamba makampuni yanawanyonya wakulima. Korosho bado haijatengamaa

Haya ni machache tu lakini Magufuli hashauriki na mtu wala hana muda wa kushauriwa. Kimsingi kichwa chake hakina nafasi ya kutunza ushauri. Yeye akiamua anakuwa ndiyo ameamua kwa hiyo akipotea anapotea kweli kweli.
Acha uongo sikiliza wazee wa Machame wamechachamaa na Mwenyekiti wako wa maisha Mh. Mbowe Mugabe.

Back
Top Bottom