Nasoma Business law, simuelewi vizuri mwalimu naomba nisaidiwe baadhi ya maswali

NARUDIA TENA... WEWE NI MPUMBAVU!
 
Naungana nawe mkuu.

Huyu mwanafunzi ama ni mzembe au ni kilaza wa kutupwa! Na labda haya ndiyo matunda ya elimu yetu mbovu.

Library hakuna vitabu? Mitandaoni hakuna vitabu? Google haipo? YouTube je?

Anauliza vitu basic sana ambavyo hata kwenye notice zake tu vimo. Labda kama huyo mwalimu hafundishi cho chote kabisa kabisa!

Na ndicho kizazi chetu hiki kilichopo hiki. Kila kitu kutafuniwa. Maisha ni mteremko tu. Ni kuvaa mitepesho na kukesha mitandaoni. Si boom lipo?

Profesa mmoja kutoka Marekani alikuja kufundisha hapa. Alionywa kwamba asiwe frustrated na wanafunzi wetu na asitegemee kuwa watakuwa na caliber sawa na wa US kwa kujisomea na hata kushiriki darasani na uwezo wa jumla. Alishangaa sana akauliza kwa kejeli: Ina maana wanafunzi wa ngazi ya chuo kikuu hawajisomei? Hawana critical thinking?...na matokeo yake ndo haya sasa.

Halafu eti tunategemea ndiyo hawa waende wakapambane katika soko la ajira katika ngazi ya kimataifa. Eti hawa ndiyo wakapambane na Wakenya na Wanaijeria...

Puliiiizi!
 
Muacheni mtoto wa watu na hivi hatujuani unaweza kuta hata ni ndugu yako kama sio mwanao. Yeye amejikita kwenye mambo ya biashara hayo masheria yamemchanga akili. Wewe hujawahi soma kitu hata ukaenda google huelewi ukabaki kuhaha. Kaona akija huku wanasheria watamsaidia kwa lugha nyepesi aelewe.


Nakumbuka na mimi nilisoma business law mwalimu anaingia na kitambi chake na simu tu. Hatoi notes wala nini ni story tu. Akimaliza anaaga anaondoka mnabaki kutoa macho.
 
Kuna wapuuzi wanatuona sisi tunaotoa kauli hizi hatuna busara, hekima na eti hatukwenda shule.

Nyie nyie... hamjui tu kinachoendelea๐Ÿ˜ฃ๐Ÿ˜”๐Ÿ˜”๐Ÿ˜”

Sijui tutakuwa na taifa la aina gani miaka ishirini (20) ijayo... mungu atusaidie.

Mtoto anamaliza shule kuna vitu ukizungumza nae, kumwambia au kumuuliza anashangaa! Eti ndo nini hiyo?! Au mwingine anadiriki kusema anadanganywa.

Kuna wajinga hapo juu wanatetea uozo huo๐Ÿ˜”
 
1: Kuhusu cinsideration
Cinsideration ni nini ulichoandika?

Wewe ulitakiwa kuwa mpiga debe kwenye daladala au mkulima ama muuza ashkrim .za Azam barabarani kama wa kiume kama wa kike ulitakiwa kuwa msichana wa kazi nyumbani kwa mtu sio mwanachuo

Shule sio saizi yako kama ni saizi yako concentration kwenye shule iko zero sababu ya kuwa na mambo mengi ya kichizi chizi

Shule inataka concentration ya uhakika sio mtu anasoma starehe anataka nk mshika mawili moja lazima limpokonyoke hasa la kusoma ndio hupokonyoka kwanza.Wengi hudanganyana Kwa kudanganyana ohh mimi nina akili za kuzaliwa kama unazo si ungejua business law bila kusoma ingekuwa Unazaliwa tu unazijua

Concentrate kwenye masomo acha ujinga tatizo sio mwalimu haeleweki wewe ndio hueleweki na upumbavu wako na kutokuwa serious na masomo

Na utafeli hasa ukiendekeza huo ujinga

Wanaofeli masomo wenye akili pia huwemo ila ni wale wasiotilia maanani masomo na kuendekeza starehe na ujinga

Mwisho wa siku wanashangaa aliyemuona akili hana kafaulu yeye kafeli

Kazana kusoma wewe acha ujinga
 
hicho chuo kama nakijua hivi sio cha pale kwenye kona?
 
Sawa Mrs Van lakini najua ninachokisema. Mimi ni mkereketwa wa mambo ya elimu na nina angalau fununu ya mifumo mbalimbali ya elimu huko Ulaya, Marekani, Asia na hata hapa Afrika. Nimeshafanya kazi kwenye mashirika yanayojihusisha na elimu katika nchi za Kiafrika ikiwemo Tanzania. Kuna wakati inafika unatamani ujifiche ili kukwepa aibu inapofika wakati, kwa mfano, usaili wa mwanafunzi wa Kitanzania kupatiwa scholarship. Yaani vijana wetu wako shallow ajabu na huwezi kuwalinganisha na Wakenya, Waganda na wengineo. Kwa nini wa kwetu tu ndiyo wawe hivi?

Mwanzoni nilidhani pengine ni ishu ya Kiingereza lakini baadaye niligundua kuwa ni mfumo wetu wa elimu kwa ujumla wake. Wanafunzi wetu hawatafuti maarifa. Ni kukariri kariri tu na kukopi kopi hapa na pale wanafaulu mitihani yao basi. Na mfumo wetu unaendekeza hii tabia.

Huyu amenishangaza kwa sababu mambo anayouliza ni basic sana na yapo tu mtandaoni one click away. Angekuwa anauliza mambo serious angalau...lakini pengine ni kwa vile siyo uwanja wake...

Mrs Van. Hebu rudi tena ukaangalie maswali anayouliza. Hebu jipe muda wa masaa mawili tu uzame mtandaoni kutafuta majibu. Au nenda library hapo chuoni na mitandaoni kutafuta vitabu husika. Kweli huwezi kujibu hayo maswali basic? ๐Ÿ˜ณ๐Ÿ˜ณ๐Ÿ˜ณ
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ