Sawa Mrs Van lakini najua ninachokisema. Mimi ni mkereketwa wa mambo ya elimu na nina angalau fununu ya mifumo mbalimbali ya elimu huko Ulaya, Marekani, Asia na hata hapa Afrika. Nimeshafanya kazi kwenye mashirika yanayojihusisha na elimu katika nchi za Kiafrika ikiwemo Tanzania. Kuna wakati inafika unatamani ujifiche ili kukwepa aibu inapofika wakati, kwa mfano, usaili wa mwanafunzi wa Kitanzania kupatiwa scholarship. Yaani vijana wetu wako shallow ajabu na huwezi kuwalinganisha na Wakenya, Waganda na wengineo. Kwa nini wa kwetu tu ndiyo wawe hivi?
Mwanzoni nilidhani pengine ni ishu ya Kiingereza lakini baadaye niligundua kuwa ni mfumo wetu wa elimu kwa ujumla wake. Wanafunzi wetu hawatafuti maarifa. Ni kukariri kariri tu na kukopi kopi hapa na pale wanafaulu mitihani yao basi. Na mfumo wetu unaendekeza hii tabia.
Huyu amenishangaza kwa sababu mambo anayouliza ni basic sana na yapo tu mtandaoni one click away. Angekuwa anauliza mambo serious angalau...lakini pengine ni kwa vile siyo uwanja wake...
Mrs Van. Hebu rudi tena ukaangalie maswali anayouliza. Hebu jipe muda wa masaa mawili tu uzame mtandaoni kutafuta majibu. Au nenda library hapo chuoni na mitandaoni kutafuta vitabu husika. Kweli huwezi kujibu hayo maswali basic? [emoji15][emoji15][emoji15]