Nasumbuliwa na fangasi sehemu za siri, hamna dawa ambayo sijatumia

Nasumbuliwa na fangasi sehemu za siri, hamna dawa ambayo sijatumia

muyakb24

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2018
Posts
412
Reaction score
290
Wakuu mnisamehe bure mwandiko wangu sio mzuri sana, mwenye Lengo la kunisadia anisaidie tu kama Kanielewa.

Ni hivi wakuu? Eti wapi Chimbuko La dawa za asili yaani ni sehemu gani mkoa gani au ni kijiji gani ambako Ni kuna wataalamu wa Dawa za asili Nikiwapata hao Tatizo Langu Linaweza Likaisha maana hospital nimechemka.

Wakuu nasumbuliwa na Fangasi Sehemu za siri yaani ni muwasho Kukauka kwa ngozi ya Korodani, muwasho wa mapajani Yaani ni muwasho Usio wa kawaida. Hamna dawa ambayo sijatumia kama ni hospital nishaenda zaidi ya Kumi tena Kubwa.
 
Tafuta dawa za fungus za kumeza, mara nyingi wenye kuzifahamu vizuri hizi ni dermatologists. Hakikisha na mwenza wako anatibiwa na ikiwezekana acheni sex kipindi cha matibabu.

Jikaushe vizuri baada ya kuoga na taulo ulianike juani. Ikiwezekana ukipona nunua mataulo na boxers mpya.
 
Dawa kuu ya fungus ni kuacha tabia inayosababisha hao fungus. Mfano kama hao fungus wanasababishwa na matumizi ya maji fulani basi unaacha kutumia hayo maji.

Pia tumia dozi ya vidonge pamoja na dozi ya kupaka kwa wakati mmoja wa hii dawa kisha utarudi hapa bila shuruti kunishukuru.

073236.jpg
073254.jpg
 
Nakupa dawa bure hapa siku mbili tu uje unipe mrejesho ni uhakika asilimia 90,tafuta jani la alovera jipake ile juice yake sehemu husika asubuhi na jioni siku mbili tu uje ushukuru hapa
Nishafanya hii kitu hamna majibu yoyote
 
Wakuu mnisamehe bure mwandiko wangu sio mzuri sana, mwenye Lengo la kunisadia anisaidie tu kama Kanielewa...
Pole kwa maswahibu. Kama unahitaji dawa ya kienyeji, chukua punje 10 za kitunguu swaumu vitwangwe na weka chumvi kidogo na maji ya vuguvugu kijko kimoja au viwili. Changanya then kunywa kwa siku 5 asubuhi na jioni. Visipokauka uchawi upo.

Unaweza paka hiyo alovera wakati unatumia swaumu.

Pia uwe unabadili boxer. Mtu boxer moja siku 2 khaaa... Na ukilala achia mbupu hizo zipate hewa.

Tahadhari: Kama una presha ya kushuka usitumie vitunguu swaumu utakufa.

Nipe mrejesho next week 28/07/2021.
 
Nishafanya hii kitu amna majibu yoyote
Mkuu nakuja pm kukuelekeza namna ya kupona hiyo fangasi kwa kutumia Wild neem, mafuta ya Nazi na Alovera hakika utapona na kusahau tatizo hilo. KUNA JAMBO 1 WENGI HAWALITEKELEZI KATIKA KUJIBU FANGAS FUATANA NA MIMI PM MKUU
 
Wakuu mnisamehe bure mwandiko wangu sio mzuri sana, mwenye Lengo la kunisadia anisaidie tu kama Kanielewa.

Ni hivi wakuu? Eti wapi Chimbuko La dawa za asili yaani ni sehemu gani mkoa gani au ni kijiji gani ambako Ni kuna wataalamu wa Dawa za asili Nikiwapata hao Tatizo Langu Linaweza Likaisha maana hospital nimechemka...
Kunywa fluconazol na dawa ya kupaka hile scaboma
 
Back
Top Bottom