Nasumbuliwa na harufu ambao mke wangu amekuwa akisema ni harufu ya kizee

Nasumbuliwa na harufu ambao mke wangu amekuwa akisema ni harufu ya kizee

Pelly

Senior Member
Joined
Mar 26, 2013
Posts
197
Reaction score
207
Habari zenu wana JF

Nimekula nasumbuliwa na harufu ambao mke wangu amekuwa akisema ni harufu ya kizee, nimejaribu kuitumia sabuni tofauti na perfume lakini wapi.

Kazi nikiingia kuoga nikitoka harufu mbaya sana humo ndani, nitumie dawa gani au kama kuna anayejua kutatua hii changamoto naomba msaada wenu jamani.

Asanteni
 
Habari zenu wana JF

Nimekula nasumbuliwa na harufu ambao mke wangu amekuwa akisema ni harufu ya kizee, nimejaribu kuitumia sabuni tofauti na perfume lakini wapi.

Kazi nikiingia kuoga nikitoka harufu mbaya sana humo ndani, nitumie dawa gani au kama kuna anayejua kutatua hii changamoto naomba msaada wenu jamani.

Asanteni
kiongozi tafuta pesa, shemeji yetu ndo anayeya huyo tayari 🤣
hujasema nn kinachotoa hiyo harufu ni ngozi, kinywa chako au nn hasa? hiyo harufu anaisikia mkeo tu? wew au wengine hawaisikii?
 
DAWA PEKEE NZURI NA HUTAKUJA KUJUTA NI "KUMUACHA MKEO TENA KWA KUMFUKUZA KAMA MBWA KOKO"
Huna mke hapo una mwanamke mapumbavu unayemhudumia ili siku za usoni akufanye vibaya zaidi...
Fukuza hiyo takataka oa mwanamke mwingine
 
Hiyo shida imeanza lini? Je, umewahi kujua chanzo cha tatizo? Perfume zipi umewahi kutumia na sabuni zipi?

1. Jaribu kutumia deodorant ambazo zina zinakata jasho na kukuweka ktk harufu nzuri, mfano NIVEA Silver deodorant au FA Sport deodorant. Kila ukioga, jaribu kujipaka eneo la kwapa, mgongoni chini ya shingo, pia paka eneo linalozunguka shingo na shingoni pia.

2. Tumia perfume ambazo ni zile za gharama, mfano Invictus, 212 Men ambazo bei zake ni 200,000 kwa kila moja. Ukishindwa basi tumia zile za mafuta za kupima lakini ukifka dukani mwambie muuzaji akuwekee kimiminika kinachofanya perfume ikae zaidi ktk nguo/ngozi. Perfume waweza jipulizia kwenye ngozi kama ambavyo nlivyokwambia ktk deodorant.

Jizoeze kutumia hivi vitu mara kwa mara, mwili utazoea kupokea harufu mpya na ya kale itaondoka. Upande wa sabuni jaribu kutumia za maji.
 
Hata hapa jamii forum wamekupa cheo cha senior member nao sijui wananusa hio harufu🤣🤣🤣

Mkuu utani tuweke mbali shemeji yetu ametoa sababu ya kibwege kweli akwambie ukweli tu kama hakutaki tena yaishe tu.
 
Hiyo halufu wazee wengi almost 99% wanayo tena siyo wazee ukishagonga tu 45plus. Unachotakiwa kufanya, safisha kinywa chako kwa watalaamu anagaku mara moja kila baada ya miezi sita, kunywa maji ya kutosha, tumia pia green tea kama huna pressure, fanya mazoezi. Waliokujibu hapo juu ni wajinga hawajui kitu. Pia nenda upime UTI, na vingine eg. Mkeo anakupenda sana tena mpende mno na mshirikiane kuondoa halufu. Hata wanawake hasa wanaovaa tight na suruari yaani wananuka utadhani choo hahaha. Hivyo mkeo anakupenda na usimuache mshukuru sana
 
Kama imekuja ghafla bhasi nenda tu hospitali au kaulizie dawa za asili maana unaweza kuta dawa yako ni kuogea maji ya limau au maji ya ukoko wa wali 😁😁. Natania mkuu ila mantiki ni kuwa kwenye dawa za asili, vitu vidogo vinatibu matatizo makubwa
 
Back
Top Bottom