Hiyo shida imeanza lini? Je, umewahi kujua chanzo cha tatizo? Perfume zipi umewahi kutumia na sabuni zipi?
1. Jaribu kutumia deodorant ambazo zina zinakata jasho na kukuweka ktk harufu nzuri, mfano NIVEA Silver deodorant au FA Sport deodorant. Kila ukioga, jaribu kujipaka eneo la kwapa, mgongoni chini ya shingo, pia paka eneo linalozunguka shingo na shingoni pia.
2. Tumia perfume ambazo ni zile za gharama, mfano Invictus, 212 Men ambazo bei zake ni 200,000 kwa kila moja. Ukishindwa basi tumia zile za mafuta za kupima lakini ukifka dukani mwambie muuzaji akuwekee kimiminika kinachofanya perfume ikae zaidi ktk nguo/ngozi. Perfume waweza jipulizia kwenye ngozi kama ambavyo nlivyokwambia ktk deodorant.
Jizoeze kutumia hivi vitu mara kwa mara, mwili utazoea kupokea harufu mpya na ya kale itaondoka. Upande wa sabuni jaribu kutumia za maji.