Natabiri hili kutokea kwenye mikutano ya CHAUMMA

Ukipata connection kuhusu washangiliaji mimi nipo mkuu, bei zangu ni rafiki hatutashindwana na chauma.
Nina uwezo wa kushangilia masaa 12 bila kuchoka.
Pia nina crew yangu ya ushangiliaji, tupeni tenda jamani.
 
Kuna clip inatembea youtube ambayo vijana wanajadili kuwa wamedhulumiwa pesa walioahidiwa wakihudhuria mkutano wa CHAUMA.
Wanaeleza kuwa nauli walitumiwa na Wenje na ndiye aliyeratibu safari ya washiriki wa kutoka Mwanza.Lakini wanadai kuwa kwenye mkutano wa Mwanza wa tarehe 30 watawaaibisha CHAUMA kwa kuwaumbua kupitia vyombo vya habari.
Mambo yameshaanza kuharibika.
Mimi naamini kuwa pesa akipewa mchaga agawe haiwezi kufika yote.
 
Chama kwa bara kimebaki Tunduru,na Kigoma mjini
 
Hizi ni mbinu za kulaghai wapuuzi, wajinga na wapumbavu, waaerevu wanang'amu na kuona ni hila za kuikomoa chadema yenye upinzani wa kweli
Wabongo si wa kuwaamini..Wengi akili zao wanazijua wenyewe.

Tukiacha wasomi na wengine angalau wanaofanikiwa kupata taarifa mitandaoni mbumbumbu ni wengi ambao ndio mtaji wa wanasiasa matapeli.
 
Watu

Watu watapigwa mawe na zomeazomea mpaka wakome
Na ndiyo dawa iliyobaki..Wanasiasa matapeli ni wakati wa kuwaonesha kwamba hii ni karne ya 21 na si karne ya 19 na za huko nyuma kama wanavyodhani.
 
Chama kwa bara kimebaki Tunduru,na Kigoma mjini
Hata hawa wachumia tumbo wangeelekezwa waende ACT kuipa nguvu..
Ila nadhani changamoto ni mbili.
1.Bwana mkubwa mstaafu wa Upinzani na wafuasi wake wasingeweza kukubali kwenda kwenye chama cha mtu waliyemfurusha kwa aibu.

2.Dola ina wasiwasi wa ACT kupewa nguvu italeta usumbufu Zanzibar kama ilivyokua nyakati za CUF na Maalim Seif yake.
 

Nina mashaka makubwa na sustainability yake, mwekezaji anahitaji mtaji mkubwa sana kwa hii biashara anyway! Ataweza kuifanya hadi uchaguzi ufike? Kumbuka watu wote wa chama hiki ni wageni na wana njaa kali! Alikua Rungwe tu na mwanae (tena kwa kujitolea) sasa payroll imekwenda juu sana probababy by 1m% au zaidi tena ghafla!
 
Hakuna kinachoshindikana..Hii nchi ina pesa za kutosha.Na pia kumbuka huyo tycoon wa upinzani anachangia pia mbali na pesa za mfumo.

Na uzuri zaidi watawala wala hawaogopi kufuja pesa za umma as long as hakuna wa kuhoji na pia zitawasaidia kuendelea kutawala kwa amani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…