Natabiri jaribio lolote la kubadilisha Katiba na ukomo wa Rais litaibua mazito

Unaweza kumhukumu Magufuli leo kwamba atamuua Mbowe 2025?
 
Jambo muhimu ni kuutunza huu uzi mpaka 2025. Tukijaliwa tuurejee.

Magufuli asipoongeza muda utafanya nini?

Hizi habari watu wamesema tangu enzi za Kikwete angalau.
 
Mmeporwa kura mchana kweupe mmetuliza Mbupu sembuse kuongeza muda? Tulieni mchezee kichapo...
 
Mmeporwa kura mchana kweupe mmetuliza Mbupu sembuse kuongeza muda? Tulieni mchezee kichapo...
Hawa watu wanawayawaya tu.

Nimeuliza swali mara kadhaa hapa.

Wakiweza kumzuia Magufuli asiongeze muda, au Magufuli mwenyewe akiamua kutoongeza muda, halafu Magufuli akapachika kibaraka wake awe rais, na Magufuli aendelee kuendeleza sera zake kwa remote control, watafurahia kwamba wamemtoa Magufuli?

Mpaka sasa sijaona jibu.
 
Leadership style Magufuli imeshajikita mizizi sana. Hakuna atakaye m-challenge wala la kukataa wala wa kumbishia tena hata akitaka saa saba mchana sote tuwe vitandani mwetu tumelala.
 
Leadership style Magufuli imeshajikita mizizi sana. Hakuna atakaye m-challenge wala la kukataa wala wa kumbishia tena hata akitaka saa saba mchana sote tuwe vitandani mwetu tumelala.
Watu ambao wameshindwa kutekeleza majukumu yao ya msingi, mara nyingi hujitungia vikazi kazi vya uongo na kweli vya kijingajinga ili waonekane wako busy.

Hiki ndicho kinachofanyika katika hoja hii.

Upinzani Tanzania umeshindwa mambo ya msingi.

1. Kuleta mabadiliko ya katiba.
2. Kuleta tume huru ya uchaguzi
3. Kuhakikisha kura haziibiwi
4. Kuhakikisha madaraka ya rais yanapunguzwa na haki za kikatiba kama za kuandamana na kukutana hazivunjwi.
5. Kuelimisha umma wa Tanzania na kuushirikisha kwenye kudai yote ya hapo juu.

Upinzani umeshindwa katika hayo matano ya muhimu yote.

Yani hata wizi wa kura wa 2020 umeshasahaulika.

Watu wanatutengenezea vita ya kijinga kuhusu mambo yatakayofanyika 2025.

Ni habari za kipumbavu sana.
 
.

Yani hata wizi wa kura wa 2020 umeshasahaulika.

.

Sio tu umesahaulika, Wapinzani wanalambishwa madaraka na fedha(Ruzuku). Huku kwetu tukio la akina Halima litakufa tu na watapeleka wabunge watake wasitake. Kule Zanzibar tamaa ya kuwa mkubwa na kukimbizwa na ving'ora imetamalaki, any time mzee mzima anageukia Quibla.

Hatuna upinzani Tanzania
 
Unaweza kumhukumu Magufuli leo kwamba atamuua Mbowe 2025?
Wewe unajua hawezi kufanya hivyo? Au ni lini ulisikia akitamka hawezi kufanya hivyo; na hata angetamka, kwa tabia zake alizokwishaonyesha ni watu kama wewe pekee ndio wangeamini anayosema.

Usitake kulazimisha watu wengine waamini unavyoamini wewe, hata ikiwa ni kwa sababu uzijuazo peke yako, au kwa utetezi tu usiokuwa na ushahidi wowote.
 
Umesikia lini akisema hatamuua? Hilo ndilo jibu.
Kwa hiyo Magufuli akiwa hajasema hatamuua maana yake ni kwamba atamuua?

Na akisema hatamuua je, maana yake nini?
 
Kwa hoja zao hizi zisizo na kichwa wala mguu, wanaweza kuburuzwa mpaka 2035 angalau.

Kama si zaidi.
 
Kwa hiyo Magufuli akiwa hajasema hatamuua maana yake ni kwamba atamuua?

Na akisema hatamuua je, maana yake nini?
Mtu anapojulikana ni mwongo na hawezi kuaminika kwa lolote asemalo, na kukiwa na mifano ya aliyofanya kinyume na matakwa hata ya katiba, unazo sababu zipi kuonyesha kuwa hatafanya unalomtetea kuwa hatalifanya.

Umezua hili la Mbowe, kwa sababu zipi, kwa sababu hata kukana kuwa hatafanya hivyo hajawahi, kama alivyolaghai kuwa hataongeza muda.

Kama unataka mfano wako huo tuujadili kama tunavyojadili swala la kuongeza muda, basi kamwambie akane kuwa "Hatamuua Mbowe; halafu tutaanzia hapo kujadili hilo swala jipya.
 
Kwa hoja zao hizi zisizo na kichwa wala mguu, wanaweza kuburuzwa mpaka 2035 angalau.

Kama si zaidi.
Unajionyesha kutokuwa makini.
Maswala ya katiba na hayo unayoshikiia wapinzani wanayasahau kwa vile tu hawaamini kuwa Magufuli haaminiki kwa kudai hataongeza muda, ni maswala ya wananchi wote na wala siyo ya wapinzani peke yake. Hata CCM wanalo jukumu hilo. Kwa nini unalifanya lionekane ni la wapinzani peke yao?
 
Wananchi wengine na CCM wamewasusia hizi habari wapinzani.

Na wapinzani mnatapatapa.

Hamjui hata hoja ya kuanza nayo.

Mnarukia vioja vya kuzua kesi za makosa mnayobashiri yatafanyika 2025.

Kama vile hakuna makosa yaliyokwishafanyika 2020.

Just ridiculous.
 
Akikanusha utamuamini?
 
Tanzania kuna wafanyabiashara wa siasa na sio wanasiasa.
 
Sijui maana yako ya 'wapinzani' ni ipi hasa katika mjadala huu. Unanijibu mimi unajua niko kwenye chama gani cha upinzani?

Ni wananchi wapi hasa waliowasusia hao unaowaita wapinzani? Wewe huoni wananchi hao na wapinzani, na hata CCM wenyewe ni mateka wa mtu unayemtetea?

Wewe unadhani wananchi hawaoni makosa yaliyokwishafanyika 2020?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…