Natafakari nini cha kumfanya...

Lugha ya mjini wewe ni danga huna zaidi ya hilonau zamani buzi la kuchunwa
 
Mkuu naona kuna mahali umeuliza kosa lako nini.....kosa lako ni moja tu mkuu HAKUPENDI hilo ndo kosa lako kubwa sanaaaa
 
Daaah mwanangu unakosea sana usirudie tena huu upuuzi ndugu yangu kumpenda sana mwanamke na kujitoa aimaanish ndo anakupenda sana jifunze kufanya vitu kwa kiasi
 
Nakubaliana na wewe kabsa sema niko kwenye kipindi kigumu sana cha kujiuliza kosa liko wapi au hawa viumbe ndio walivo hivi au nimekosea chaguo.
1. Mwanamke yeyote ambaye shida ndiyo iliyomleta kwako, huyo usimuamini kuwa ni wako milele, kaa nae chonjo.

2. Mwanamke yeyote ambaye pesa ndiyo ushawishi mkubwa kwake, yaani anakuona mwanaume pale tu unapomtumia pesa na huo muda ndio anaokupenda zaidi ila ukikosa pesa tu kidogo anabadilika na hakupendi wala kukutia moyo hata kwa kuonyesha kujali hali yako kwa wakati huo ambao huna, huyo naye kaa naye makini.


3. Mwanaume ukiona mwanamke huelewi matendo yake na hakuweki wazi kwa maamuzi baadhi anayofanya, jiongeze acha kupoteza muda.

4. Mapenzi ya kukutana mjini na kujuana miezi mitatu, sita au mwaka tu kisha kuanza kuaminiana na kupanga ndoa, huko ni kudanganyana kama hujajiandaa kustahimili matukio mazito.

5. Usimuamini mwanamke kiasi cha hisia zako kuingia kwa asilimia 100, yaani namaanisha wewe mwanaume achana na masuala ya kupenda kwa moyo, wewe unapaswa kupenda kwa akili. Siyo mwanaume unapenda mpaka unakuwa mtu wa kuendeshwa, onyesha uanaume wako kwa kutotoa mwanya wa hisia zako kutawaliwa. Kiongozi lazima kutumia akili na hisia kiasi, siyo kwa asilimia 100 unatumia hisia kufanya maamuzi, utaumia.


6. Naomba kusisitiza hili mwanaume acha kutanguliza pesa na kutoatoa vitu hovyo kwa mwanamke. Wanawake hawa wana akili sana tu ukionekana wewe mapenzi yako yanalindwa na fedha basi atakutumia vilivyo, jenga mazingira ya mwanamke kukupenda kiuhalisia na siyo kwa kupitia pesa na sina maana ya usimpe, hapana ila USIENDEKEZE.

Miezi 6 umepoteza 10M mwamba hukushtuka kuelewa unawekeza wapi??

Mwisho ni kwamba, ebu tanguliza malengo fulani katika maisha yako na malengo hayo yawe na uzito kuliko chochote kile, kwa mfano binafsi namuomba Mungu baada ya miaka kadhaa walau nijenge nyumba za kusaidia wahitaji hata mbili tu kubwa na waweze kupata huduma zote BURE, na malengo mengine yenye kuendana na hili. Kuna wakati nikiwaza mahusiano kuniharibia baraka na alama ambayo nitaiacha hapa duniani naona mahusiano kwani kitu gani ?? Hivyo kutobabaishwa na chochote maana najua kuna ambacho naweza tengea muda na kikanipa furaha zaidi hata kuliko mahusiano hayo. Nadhani ndiyo maana wife hajawai nipandia kichwani, huwa namueleza wazi kabisa kuna ya msingi kuliko yeye na familia hivyo akizingua anakaa pembeni mda wowote watu tuache legacy za maana na kukumbukwa milele.
 
Binadamu huwa anafundishwa zaidi pale yanapomkuta,, so amini kuanzia leo utakuwa mwalimu mzuri sana kwenye huu ulingo wa malavidavi
 
Haya mambo yanaumiza sana,kama una roho ndogo unaweza kumdhuru mtu kwa namna yeyote ila ndio haina budi kuyapotezea
 
Kitakachoponya moyo wako ni kuvunja uhusiano na ukaribu na yeye.

Kwa sasa una migogoro miwili, wewe na nafsi yako, wewe na yeye yaani unajutia upendo wako kwake halafu unamchuki kwanini ulimpenda na kufanya yote kwaajili yake kitu ambacho si kosa...

Katika hali yako usifikirie kufanya kisasi bali angalia unawezaje kuponya nafsi yako, move on and break soul ties ili siku huyo binti akili ikimkaa sawa na akajirudi kwako, wewe uwe imara kumkataa...
 
Nimeshafanya hayp maamuzi na nimemweleza kuwa alichofanya kunitumia sio ubinadamu angesema shida yake kwangu kulikp kupotezeana mda na resources,kwa jinsi alivo mjeuri akulijibu ilo so i wished her the best in life lakini atanikumbuka siku na ata kutana na mtu aliyejitoa kama mimi kwake atachezea D. U. D. U kwenda mbele tu.

Sent from my 601SO using JamiiForums mobile app
 
Aisee!
Hebu tulia kwanza!
Haya mambo haya yasikie tu kwa mtu!
 
Nakubaliana na wewe kabsa sema niko kwenye kipindi kigumu sana cha kujiuliza kosa liko wapi au hawa viumbe ndio walivo hivi au nimekosea chaguo.
Unafikiri mtu akiamua kukufanyia mambo yake unakuwa na kosa?
Yashatukuta wengi tu,lkn hatuwezi kuhukumu wanaume,wanawake kwa kosa la mtu mmoja!
 
You may be looking on the same direction, yet differ on what you see.

Wewe unaona mapenzi kati yenu. Ila yeye anaona fursa. Hapo ni maji na mafuta broh.
 
You may be looking on the same direction, yet differ on what you see.

Wewe unaona mapenzi kati yenu. Ila yeye anaona fursa. Hapo ni maji na mafuta broh.
Well said brother, kama unavosema. I hope she gets what she deserves. Sema hawa watu ni hatari sana

Sent from my 601SO using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…