Natafuta Audio Clip ya zaidi ya Dk 5 ambayo Rais Samia anazungumza Kiingereza

Putin hajui kingereza hata kimoja lakini anaitikisa dunia
Ni kweli kabisa. Ninapata ugumu kuelewa hivi kiingereza kinaweza kusignify elimu ya watu? Je kujua kuongea kiingereza ndiyo kuwa na elimu bora? Kwa maoni yangu tunakosea sana kuwaza hivyo. Putin kweli hajui kiingereza na dunia inamtambua. Lakini kutokujua kwake kiingereza hakuna maana kama hakuelimika. Mataifa mengi ya dunia hii wananchi wake hawajui kiingereza lakini tazama maendeleo ya China,Korea,Japan etc. Tunaweza kujilinganisha nao? Tuache kuamini kuwa elimu ni kujua kiingereza!
 
Mbona hujamtaja Alhaji Mwinyi
Sikupata intevriew ya ana kwa ana. Ninajua kuwa alipohutubia Baraza la Umoja wa Mataifa alikisoma hotuba, alitamka jina la katibu Mkuu wakati huo kuwa "Javia" Perezi de "Kuela" kwa kusoma Javier Perez de Cueller badala ya kutamka "Havia Perez de Cueya"
 
Alitakiwa kusema = i am thankful being here
Ha ha ha. Wadanganyika bwana!! Nawe unaona umepatia na unajua Kiingereza sana. Hapa anazungumzia appreciation na sio thanks ingawa inaweza kuwa ni synonym. Nilitarajia ungesema "Alitakiwa kusema = I really appreciate being here" ungekuwa umemsahihisha, ila ndio JF kila mmoja anajiona anajua na mwenziwe hajui.
 
Hayati B.W
Mkapa alikuwa mwamahabari by professional hivyo kwake midahalo ilikuwa ni sehemu ya maisha; ni tofauti na mtu kama hayati JPM ambae by professional alikuwa anashinda maabara. Ila lugha sidhani kama ni kipaumbele sana wapo marais wa mataifa makubwa duniani hawaongei "English" la hawajui kabisa na bado dunia haishangai huu ulimbukeni tunao sisi tu.
 
Reactions: Tui
Hilo halina mjadala siyo kwamba kila anayekiongea amesoma, lakini kama alivyoeleza mchangiaji mmoja hapo juu tunafahamu wa TZ wengi sana walioshindwa kwenye interview za kazi za maana sana, siyo kwa sababu hawakusoma ila walishindwa kujitetea kwa kujibu maswali kwa usahihi. Matokeo yake majirani zetu wanazichukua fursa zilizoko ndani ya nchi yetu.
Yaani hakuna hata haja ya kwenda mbali sana, tembelea maeneo ya kitalii na mahoteli ya kitalii utauona ukweli wa tunayoongelea. Hatusemi kwamba tuidharau lugha yetu, bali tujiweke tayari tuwe na vifaa vyote. Unapokwenda shamba unachukua vifaa vya kutosha kuhakikisha linakuwa tayari kupanda mbegu na hatimaye kuvuna kama vile shoka, jembe, panga, sururu nk. nk.
Watanzania wenzangu tuache uvivu wa kujisifu na lugha moja.
 
Msipende kujidanganya. waTanzania tunahitaji sana kujua lugha kubwa za kimataifa. Huwezi kujilinganisha na say mjapan au mkorea eti nao wanatumia kilugha chao. Sisi ni nchi changamasikini, (msisitizo: Tanzania ni nchi changamasikini, masikini sana). Tunahitaji kujifunza kwa wenzetu waliokwishaendelea, tupate maarifa ya sayansi na teknolojia. Sasa Kama hatujui lugha yao tutawezaje kuiba teknolojia kwao?
Na pia 'wanyonge' wanapaswa kufahamu kwamba wakati wanasiasa wanawahubiria kiswahili ni lugha adhimu na kuwahimiza kuienzi/kuijivunia, wao watoto wao wanawasomesha English medium schools hapa nchini au Kenya, Uganda, South Africa au Ulaya na America.. etc.
 
Wivu tu huo. Mtakufa na vijiba vya roho mkifuatilia madhaifu ya Rais Samia. Samia yuko vizuri sana kwenye English
 
Uongo. Hayuko vizuri.
Huko USA kwenye UNGA, Paris kwenye COP 26 na Dubai anatumia lugha gani?

Unayo clip ambayo ameshindwa kujieleza au ameongea broken?
.
WAPINZANI wa Samia kuleni sementi tu, lakini Samia anaupiga mwingi
 
Wivu tu huo. Mtakufa na vijiba vya roho mkifuatilia madhaifu ya Rais Samia. Samia yuko vizuri sana kwenye English
Kumbe wewe hujui kiingereza. Unakuja tetea ujinga? Hujui kiingereza kabisa. Bora ungenyamaza
 
Chawa wamekariri, wanadhani Put-in hajui English!
 
Kuna WAHUNI wanaamini kujua lugha moja tu ya Kiswahili ndo uzalendo. Bure kabisa!
 
Kumbe wewe hujui kiingereza. Unakuja tetea ujinga? Hujui kiingereza kabisa. Bora ungenyamaza
Wewe unayejua Kiingereza kuliko Mimi mbona unaandika kwa kiswahili hapa? Hebu leteni issues achaneni na mambo ya jikoni hapa JF
 
Wewe unayejua Kiingereza kuliko Mimi mbona unaandika kwa kiswahili hapa? Hebu leteni issues achaneni na mambo ya jikoni hapa JF
Mbona kama una makasiriko sana sister? Kwani kuna ubaya gani mtu kutaka kusikia kitu anachopenda? You want me to write in English? Well, i have written now. Tell me what else do you want madam? You shouldnt be that much negative. We socialize here and share some experience. Why are you so bitter? Relax. Life aint that much tough. Smile my dear sister....you dont wanna get old so early. Do you?
 
Waliomwalika ndio walipaswa kumwambia we appreciate your being here na sio yeye aseme i appreciate being here.
 
Waliomwalika ndio walipaswa kumwambia we appreciate your being here na sio yeye aseme i appreciate being

Waliomwalika ndio walipaswa kumwambia we appreciate your being here na sio yeye aseme i appreciate being here.
Ni mawazo yako. Uko huru kutoa mawazo. Nadhani umeona nilikuwa natoa mawazo kuhusu nini. Kwa mujibu wa online dictionary moja ya maana ya appreciate ni "be grateful"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…