Mambo hayaishii hapo tu Mkuu, sheria zetu ziko kwa lugha ya kigeni zaidi. Na sidhani kwamba ni kosa Lisu kumsema mwanasheria mwenzake kushindwa kuongea kiingereza, maana mengi kwenye kozi zao yanafundishwa kwa kiingereza. Sasa utashangaa alipitia tundu lipi akaukwaa uanasheria. Na si hivyo tuu, msomi ni vizuri akaupinda mgongo afahamu angalau lugha kuu mbili ikiwepo moja ya kigeni. Kwani kiingereza nani alikudanganya ni lugha ya kutisha? Watu waache uvivu. Zipo nchi ukifika unakuta watu wengi wanaongea lugha nne. Niliwahi kufika duka moja uswiss nilipokuwa naulizia bei ya kitu kwa kiingereza, mara akaingia mteja, muuzaji akaanza kuongea naye kifarannsa, mara akaingia mwingine akaanza kuongea naye Kitaliano, mara akaingi mwingine wakaanza kijerumani. Nilipouliza inawezekanaje kirahisi namna hiyo nilijibiwa kuwa nchini mwao hiyo ni kawaida watu huongea lugha nne hadi tano.
Sasa kinachotushinda kujifunza mbili tu (ukiacha ya kabila lako) ni nini?.
Tuache kujilegeza tuhimizane tusonge mbele.