Tuna
Watanzania ,tunaonyesha ujinga na upumbafu mkubwa ,kwa kufikiria kuwa kuongea kiingereza ndio maendeleo.Huu ni ujinga mkubwa Sana.Na huu ni aina ya mbegu za ukoloni ,zilizopandikizwa vichwani mwetu.Hata Lissu siku moja nilimsikia kwenye kampeni akibwabwaja kuwa ,baadhi ya wanasheria hawajui kiingereza.Hivi tulilogwa wapi?Labda niwambie kuwa nchi zote zilizoendelea wanatumia zaidi mother tongue.Lugha zao za asili.Mfano China,Korea,Urusi,Japan,Ufaransa,Italy,Hispania.Ujinga wetu ni pale hatutaki kuitumia lugha yetu ,na tunasmini kiingereza.Eti mtu akiongea kiingereza kizuri tunamsifia Sana.Tunasema huyo ndio msomi.Mbona Kuna watu hapa bongo,wanaongea kiingereza kizuri Lakini hawana elimu kabisa.Ila tu wamekaa na waingereza muda mrefu.
..mwanasheria kutokujua Kiingereza sio sahihi.
..taaluma kama bwana kilimo sio lazima awe mahiri ktk kiingereza, lakini sio mwanasheria.