Natafuta Audio Clip ya zaidi ya Dk 5 ambayo Rais Samia anazungumza Kiingereza

Natafuta Audio Clip ya zaidi ya Dk 5 ambayo Rais Samia anazungumza Kiingereza

Nitafurahi sana nikipata audio Clip ambayo itazidi dk 5 Rais wetu Mpendwa akichana mistari kwa kiingereza katika mahojiano au maelezo flani sehemu yoyote. Iwe imenyooka haijaungwa ungwa.

Nitafurahi sana. Tuachane na haya madai ya watu kuwa yeye huwa mara nyingi anasoma tu... Tunataka kuwaonesha watu kuwa hata amewahi hojiwa kwa English au akahutubia watu wa English.

Mpaka sasa ni Maraisi wawili tu wamewahi kuongea na Wasomi vyuoni. Mwalimu Julius K. Nyerere na Benjamini Mkapa. Hawa nimewahi wasikiliza. Kwa kweli tunahitaji miaka mingi kupata Marais Smart kama hawa wanaojiamini.

Mkapa hadi Midaharo alikuwa anakubali. Baada ya yeye hakuna ambaye amewahi kukubali midaharo.

Hii hapa [emoji1484]
 
Mambo hayaishii hapo tu Mkuu, sheria zetu ziko kwa lugha ya kigeni zaidi. Na sidhani kwamba ni kosa Lisu kumsema mwanasheria mwenzake kushindwa kuongea kiingereza, maana mengi kwenye kozi zao yanafundishwa kwa kiingereza. Sasa utashangaa alipitia tundu lipi akaukwaa uanasheria. Na si hivyo tuu, msomi ni vizuri akaupinda mgongo afahamu angalau lugha kuu mbili ikiwepo moja ya kigeni. Kwani kiingereza nani alikudanganya ni lugha ya kutisha? Watu waache uvivu. Zipo nchi ukifika unakuta watu wengi wanaongea lugha nne. Niliwahi kufika duka moja uswiss nilipokuwa naulizia bei ya kitu kwa kiingereza, mara akaingia mteja, muuzaji akaanza kuongea naye kifarannsa, mara akaingia mwingine akaanza kuongea naye Kitaliano, mara akaingi mwingine wakaanza kijerumani. Nilipouliza inawezekanaje kirahisi namna hiyo nilijibiwa kuwa nchini mwao hiyo ni kawaida watu huongea lugha nne hadi tano.
Sasa kinachotushinda kujifunza mbili tu (ukiacha ya kabila lako) ni nini?.
Tuache kujilegeza tuhimizane tusonge mbele.
Umeongea vizuri na kwa faida ya lugha upande mmoja tu.Faida kubwa ya lugha ni maendeleo.Na wataalamu wanasema ,mother tongue ndio lugha muhimu kufikisha maendeleo ya nchi.Tukitumia mother tongue ,na terminology nyingi za technology tukaziweka katika kishwahili ,tutafika mbali Sana.Tafiti nyingi zinaonyesha kuwa mother tongue zimewasaidia Sana Japan,China,Urusi ,kufika mbali kimaendeleo.Aidha nikiongelea faida uliyoitaja ya kujua lugha nyingi ,sidhani Kama unaweza kuzielewa kwa ufasaha.Lugha unaweza kuzielewa kwa ufasaha kwa kuzumgumza.Pia kujifunza lugha nyingi ni kupoteza muda.Unazuia ajira ya wakalimani.Sasa hivi kule USA,na SA wakenya wanapiga pesa nyingi Sana kwa kufundisha kiswahili.Sisi tupo kwenye key board tunaponda kiswshili na tunasifia kiingereza.Huku tunaendelea kuwa masikini.Wajameni nani alituroga watanzania????
 
Ni ujinga wa Hali ya mwisho kusifia kisicho chako.Hao wazungu,wanaongea Kiswahili wakihutubia?Wanatumia lugha zao,mswedeni(kiswidish)Muamerika(ana Englishi yake),Muingereza(ana Englishi yake),Mkanada(ana English yake)Ireland(ana English yake)mjerumani(Kijerumani),Muitalia (kitaliano),mfaransa(kifaransa)nk.Wataalamu wa lugha wanasema English ina lahaja 60 tofauti,wewe sijui utasema ipi Kati ya hizo 60,au utachanganya changanya.Jivunie Kiswahili chako,penda chako,achana na cha wengine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeongea vizuri na kwa faida ya lugha upande mmoja tu.Faida kubwa ya lugha ni maendeleo.Na wataalamu wanasema ,mother tongue ndio lugha muhimu kufikisha maendeleo ya nchi.Tukitumia mother tongue ,na terminology nyingi za technology tukaziweka katika kishwahili ,tutafika mbali Sana.Tafiti nyingi zinaonyesha kuwa mother tongue zimewasaidia Sana Japan,China,Urusi ,kufika mbali kimaendeleo.Aidha nikiongelea faida uliyoitaja ya kujua lugha nyingi ,sidhani Kama unaweza kuzielewa kwa ufasaha.Lugha unaweza kuzielewa kwa ufasaha kwa kuzumgumza.Pia kujifunza lugha nyingi ni kupoteza muda.Unazuia ajira ya wakalimani.Sasa hivi kule USA,na SA wakenya wanapiga pesa nyingi Sana kwa kufundisha kiswahili.Sisi tupo kwenye key board tunaponda kiswshili na tunasifia kiingereza.Huku tunaendelea kuwa masikini.Wajameni nani alituroga watanzania????
Umenikumbusha jambo zuri sana. Nakuhakikishia huo ndiyo uvivu tulio nao haswaa. Hao wakenya wanaofundisha kiswahili US na AK ni wale waliopinda mgongo wakajifunza kiswahili fasaha, siku hizi wanajua kiswahili kuliko watazania, kalisha wanafunzi 10 wa ki TZ na 10 wa Kikenya uwape mtihani wa kiswahili utashangaa matokeo ya fasihi. Na kwa taarifa yako hao wa Kei wanaofundisha kiswahili huko US na AK pia wanaongea kiingereza safi kabisa. Usiukubali udhaifu wala kuuhalalisha katika karne hii.
 
Labda kwa kuuza au kubinafsisha viwanda karibu 400 alivyoviacha mwalimu JK NYERERE, Pia kwa kuuza Bank ya taifa kwa bei chee !! Lakini pia yapo mazuri aliyoyafanya !! Apumzike kwa Amani !
 
Tuna

Watanzania ,tunaonyesha ujinga na upumbafu mkubwa ,kwa kufikiria kuwa kuongea kiingereza ndio maendeleo.Huu ni ujinga mkubwa Sana.Na huu ni aina ya mbegu za ukoloni ,zilizopandikizwa vichwani mwetu.Hata Lissu siku moja nilimsikia kwenye kampeni akibwabwaja kuwa ,baadhi ya wanasheria hawajui kiingereza.Hivi tulilogwa wapi?Labda niwambie kuwa nchi zote zilizoendelea wanatumia zaidi mother tongue.Lugha zao za asili.Mfano China,Korea,Urusi,Japan,Ufaransa,Italy,Hispania.Ujinga wetu ni pale hatutaki kuitumia lugha yetu ,na tunasmini kiingereza.Eti mtu akiongea kiingereza kizuri tunamsifia Sana.Tunasema huyo ndio msomi.Mbona Kuna watu hapa bongo,wanaongea kiingereza kizuri Lakini hawana elimu kabisa.Ila tu wamekaa na waingereza muda mrefu.
Naunga mkono hoja.
P
 
Putin hajui kingereza hata kimoja lakini anaitikisa dunia
Kwanza si kweli ,Putin anajua English,pili Russia hujifunza darasani jwa lugha yao sasa hawa wetu wamejifunza English tangu darasa la tatu hadi Phd ila hata kutamka neno enterpreneur hawezi
 
Samia hata maneno ya kawaida tu ya Kiingereza hajui kuyatamka vizuri.

Hata akiwa anasoma bado anashindwa kuyatamka.

Ni wa kawaida sana kwenye hiyo lugha.

Na hayuko vizuri kwenye kuongea.

Ukiona mtu anadai Samia yuko vizuri kwenye Kiingereza basi jua mtu huyo naye hiyo lugha inampiga chenga.

Unaweza mlinganisha na mwendazake???
Afadhali yeye alitumia lugha ya taifa. Kusemaukweli mama anachapia sana jinsi anavyotamka hata wakati wa kusoma. Sijui anatumia old english? Halafu akigundua amekosea kuna kakikohozi fulani hivi anakatupia!😀🙌
 
Samia hata maneno ya kawaida tu ya Kiingereza hajui kuyatamka vizuri.

Hata akiwa anasoma bado anashindwa kuyatamka.

Ni wa kawaida sana kwenye hiyo lugha.

Na hayuko vizuri kwenye kuongea.

Ukiona mtu anadai Samia yuko vizuri kwenye Kiingereza basi jua mtu huyo naye hiyo lugha inampiga chenga.
Ningefurahi sana kusikia cha kwako angalau dakika tano.
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Alisoma kiingereza Makerere hivyo alikuwa Mtaalamu wa hicho ki-malkia.
Kumbe alikuwa mtaalamu kabisa, basi si sahihi kumtumia kama mfano kwa kulinganisha na wengine ambao si wataalamu.
 
Afadhali yeye alitumia lugha ya taifa. Kusemaukweli mama anachapia sana jinsi anavyotamka hata wakati wa kusoma. Sijui anatumia old english? Halafu akigundua amekosea kuna kakikohozi fulani hivi anakatupia!😀🙌
Utakuwa unachuki binafsi na yeye,accent yake nzuri anawashinda viongozi wengi kama kina Museven, na anauwezo mkubwa tu,huwezi mfananisha na mtu kama Magu hata robo hamuingii,wakenya walimsifia sana wewe kaa na chukizako.
 
Lakini hashobokei Kiingereza kama wabongo malimbukeni wafanyavyo.
Kawaida hii Mufti,English ni lugha ya Dunia usitudanganye,wanaeijuwa wana haki ya kujidai,wewe nenda posta halafu Ongea ngelee uone watakavokuangalia,
 
Utakuwa unachuki binafsi na yeye,accent yake nzuri anawashinda viongozi wengi kama kina Museven, na anauwezo mkubwa tu,huwezi mfananisha na mtu kama Magu hata robo hamuingii,wakenya walimsifia sana wewe kaa na chukizako.
Wakenya wenyewe accent yao ni kama 'kiluo' waganda ndio kabisaa, ukimsikiliza waziri mkuu wao akiongea kiingereza utacheka hadi mbavu ziume!

Kwa upande wangu huwa sijali sana kuhusu kujua au kutojua kiingereza. Ila tatizo ni pale baadhi ya watu wanapodhani kwamba lugha ni kipimo cha maarifa. Lugha ya kiingereza ina lafudhi tofauti tofauti kama zilivyo lugha nyingine kutegemea na mahali, hadhi ya wazungumzaji nk. Mama hata kiswahili chake tu ni mtihani kwa sisi watanganyika tushazoea kusema jambo jingine, mama yeye husema 'jengine' nk

Kwahiyo ni matamshi tu. Na wanaotumia RP (received pronunciation) ndio tunasema wanatamka maneno ya kiingereza kwa ufasaha. Mfn BBC. Hivyo ndg, hapo hakuna chuki kabisaaaa ni mtazamo tu!
 
Samia hata maneno ya kawaida tu ya Kiingereza hajui kuyatamka vizuri.

Hata akiwa anasoma bado anashindwa kuyatamka.

Ni wa kawaida sana kwenye hiyo lugha.

Na hayuko vizuri kwenye kuongea.

Ukiona mtu anadai Samia yuko vizuri kwenye Kiingereza basi jua mtu huyo naye hiyo lugha inampiga chenga.
Hivi Kiingereza ndiyo maendeleo au? Ingekuwa hivyo basi China, Japani na tuseme Asia yote isingekuwa na maendeleo hata kidogo. Urusi tu ni Kirusi mtindo mmoja. V. P mwenyewe hata kama anakifahamu Kiingereza lakini haongei. Kule Falme za Kiarabu nako je?
Kifupi Kiingereza siyo Lugha yetu Tanzania. Tumeiga ukoloni. Hivyo siyo Lugha ya asili. Mfano Mimi wazazi wangu kabila tofauti. Foundation yangu ni lugha za wazazi zote mbili. Kikafuata Kiswahili na mwisho Kiingereza cha kusomea tena Mimi mhenga nilianza kusoma Kiingereza nikiwa Darasa la 4 kama si la 5 na vitabu vigumu vya Oxford. Nilitoka kapa mpaka nilipoanza Firm One ndogondogo nikaanza kukikamata cha kujibia mtihani na siyo fluent speaking. Sasa wale mliopata bahati mkazaliwa familia za Kishua na nje ya nchi mkaenda kuishi hatuwezi kulingana na nyie.
Likewise Rais wetu mfumo ni huo huo Ila ana bahati alifanya KAZI some International NGOs. So far Kiingereza chake kinatosha kabisa kuiweka Tanzania vizuri katika USO wa DUNIA.
Hongera Sana Madam President. KAZI Iendelee na Kiswahili kinakuwa Kati ya Lugha za Kimataifa. Loading!!!
 
Back
Top Bottom