Natafuta Connection za kucheza mpira

Kwa bongo anapaswa kuwa kipaji tu hayo mengine atafundishwa academy
 
Nakupa Akili ambayo imewasaidia Wadogo zangu 2 wa Mtaani!

Walipanga kila mtu akatafuta mtu, kwa kutumia Simu wakawa wanashoot Mechi zote za mashindano, friend match n.k

Kama unavyojua Mechi za Ndondo zilivyo ngumu, Basi wakashoot Vipande vya kutosha...

Wakapata msaada Kwa Mtaalam wa Editing, aka edit Video zao, zikakaa kwenye mpangilio mmoja, mwanzoni madogo wanajielezea historia zao, umri, urefu n.k......
Kazi zikawa zimekamilika......

Wakaanza kuzisambaza kwenye Team za South Africa, kwa Scouts wa South Africa, wao wanasambaza tu kupitia Emails, social networks n.k.....

Baada ya week chake walinifata niwasaidie kupata Passport......

Kwa kifupi walienda South Africa, na mmoja baada ya mwaka mmoja alienda Ulaya, na mwingine ndo Yupo South Africa.....

Huyu wa Ulaya yupo kwenye Academy ya Ajax......
Huyu aliyebaki South Yupo kwenye Soccer Academy moja ina jina gumu kidogo nimesahau, waliondoka wadogo miaka 17 japo walishusha miaka 2 toka 19 mpaka 17....
Sasa Passport zao zinasoma wana miaka 19...

Walikua na Vipaji halisi Kwa kweli....

Kama nawe una Kipaji Unaweza kuwaiga Wadogo zangu hawa, huenda ikawa bahati yako.
 
Mimi ni kijana wa miaka 19, Nina kipaji kikubwa Cha kucheza mpira wa miguu, urefu wangu ni futi7 na uzito wa 73kg, npo Temboni-KIMARA.

Naombeni msaada wenu wadau
Unacheza namba ngapi mkuu Man u kuna nafasi 2
 
Asante Sana nitalifanyia kazi
 
Asante Sana nitalifanyia kazi
Sio utalifanyia kazi tu, mfwate jamaa pm akupe namba ili ukimaliza akusaidie connection zaidi.

Na kwa kuongezea ukisha chukua hizo video ziweke youtube na kwenye mitandao mingine ya kijamii kama tiktok, insta na fb na jf pia!!

Pambana jombaa!!
 
Kama kawaida ya wabongo. Yani mmeangukia kwenye umri na kilo!!

Kuna kitu kinaitwa bmi mnakijua kweli? Kwa huo urefu wake mnashangaa nini kuwa na uzito huo?
Kama kawaida ya wabongo kukurupuka...hujasoma nimemuuliza urefu wake baada ya kutaja kilo zake,na comment niliyotoa after? tupunguze kukurupuka mzee,h ujasoma vizuri una comment tu.
 
Ila huo urefu unaweza kutoka nduki kweli,unatumia mguu gani japo kwa hizo namba nahisi itakua maleft,ila kwa ushauri kazania zaidi nafasi mbili ndo usonge nazo.namba 4 na 6 .ukicheza nafasi za ulinzi itakusaidia sana ila si namba tatu.
 
Ila huo urefu unaweza kutoka nduki kweli,unatumia mguu gani japo kwa hizo namba nahisi itakua maleft,ila kwa ushauri kazania zaidi nafasi mbili ndo usonge nazo.namba 4 na 6 .ukicheza nafasi za ulinzi itakusaidia sana ila si namba tatu.
Speed ninayo ya kutosha, natumia miguu yote
 
Mkuu komaa dogo ila sio rahisi achana na hawa matapeli hapa

Mimi pia nna urefu ila umenipita kidogo
Nachezaga namba nne mtaani tu kujifurahisha Mara moja moja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…