Nakupa Akili ambayo imewasaidia Wadogo zangu 2 wa Mtaani!
Walipanga kila mtu akatafuta mtu, kwa kutumia Simu wakawa wanashoot Mechi zote za mashindano, friend match n.k
Kama unavyojua Mechi za Ndondo zilivyo ngumu, Basi wakashoot Vipande vya kutosha...
Wakapata msaada Kwa Mtaalam wa Editing, aka edit Video zao, zikakaa kwenye mpangilio mmoja, mwanzoni madogo wanajielezea historia zao, umri, urefu n.k......
Kazi zikawa zimekamilika......
Wakaanza kuzisambaza kwenye Team za South Africa, kwa Scouts wa South Africa, wao wanasambaza tu kupitia Emails, social networks n.k.....
Baada ya week chake walinifata niwasaidie kupata Passport......
Kwa kifupi walienda South Africa, na mmoja baada ya mwaka mmoja alienda Ulaya, na mwingine ndo Yupo South Africa.....
Huyu wa Ulaya yupo kwenye Academy ya Ajax......
Huyu aliyebaki South Yupo kwenye Soccer Academy moja ina jina gumu kidogo nimesahau, waliondoka wadogo miaka 17 japo walishusha miaka 2 toka 19 mpaka 17....
Sasa Passport zao zinasoma wana miaka 19...
Walikua na Vipaji halisi Kwa kweli....
Kama nawe una Kipaji Unaweza kuwaiga Wadogo zangu hawa, huenda ikawa bahati yako.