Kuna siki Nzalendo akivuna korosho zake anashuka nondo za maana.Si wote wenye uwezo wa kuingia show room.
na mtu mwenye akili timamu ya utafutaji hawezi kuweka
more than 7m on the road.(labda ni limbukeni wa magari)
au kutafuta sifa,mashindano n.k.
millioni 5 shuka chini ndio akili nzuri ya ku invest kwenye motokari.
Gari dawa yake ni service tu.
Kuna sehemu magari ya toka 1930,40's,50's,60'sna 70's bado yanafanya kazi uzuuuri.
nakupeni mifano.
Iringa... Roka Taxi---Peugeot 404 inadunda barabarani mpaka leo.(ina zidi ya miaka 50 on the road)
Mwanza...Tanganyika bus wanamiliki Royle royce ina umri sawa na jina Tanzania.
Moshi...Thame trader ni aina ya malori yapo zaidi ya 5 yanabeba magogo,kabla ya uhuru mpaka leo.
Pia kuna Land rover zinapanda milima ya Tela zipo toka enzi ya Mkoloni.
Arusha ...peogeot 403 lipo maeneo ya kijenge ni pick up linadunda mpaka leo ni gari ya miaka ya 40's
Tabora...Ford anglia ya mzee mmoja bonge bonge anakaa mitaa ya bachu na cheyo.
Consolata sisters Iringa ...wana benz ya miaka ya sitini macho panzi ni kama mpya,pia wana peugeot 404 pick up wameijengea bodi.
Hii yote nataka nimfundisheni kuhusu gari unaweza lifufua likawa jipya ukalitunza likadumu daima.
Ahh Frank upoo?nilijua uzi kama huu huwezi kukosa.Katika maisha yangu nimetumia gari mbili tofauti, gari ya kwanza nilinunua 2.6m na gari ya pili nikanunua 2.3m tena sikuwahi kwenda kwa fundi zaidi ya kuweka mafuta, oil na maji tu kwahivyo mtu akisema kuwa hauwezi kupata gar kwa 2.5m ni mpumbavu na anataka kuleta ligi humu wakat tumeishatembelea gari za 2.5m bila matatizo, acheni ubishi na ujuaji na acheni kukatisha watu tamaa humu ndani wanaotafuta magari ya bei rahis!
Mkuu si Vibaya kulumbana
manake hapa tuko kwa ajili ya kusaidiana.
kwa kifupi sana.
Ilala Amana kuna gari safi kabisa kwa bei hiyo zinatembea.
Gari si issue mkuu
ila ukienda kichwa mkuki lazima ulie.
Magari ya hiyo bei yapo sana tu na Mimi nimeshayauza na niliowauzia wote hakuna hata mmoja alienilalamikia, utapata tu mkuu
mkuu nakupatia vw beetle
made in germany.
Gari ni chuma mtupu.''chuma ya mjerumani.''
Kama unakwenda Gongo la mbotoMkuu upo serious?. Mi nayapenda sana hayo yaan sijui kwann. Hvi kweli yanapatikan?
pWatu wanasumbuliwa na kutokujua. Kuna chaser nzuri saina niliinunua muda mrefu milioni tatu tena kwa insalments kama tano hivi nikaibadilisha starter (50,000/-) kwa wanaochinja na compressor ya AC (120,000/-) ina miaka mitano sasa na nikiwa na safari ndefu hiyo ndio chombo yangu. Ukikosa gari kwa 2.5 huna bahati
p
niambie chesa cc 1800 linakulaje fuel.naka nilichukue