Natafuta kazi taaluma yangu ni Bachelor of Science in Chemistry Nipo Tayari Kufanya Kazi Ndani au Nje ya Taaluma Yangu

NISIKILIZE KAKA AKO HAPA

•Achana na mambo ya kuwaza ajira kwanza.

•Kazi zipo za kutosha mtaani ila zinahitaji uweke aibu pembeni.

•Kitaa kina matatizo kibao angalia unaloweza kulitatua kwa hiyo 300k waja wakupe pesa.

UKIONA HUELEWI KABISA NJOO UKU KUSINI NIKUPE KAZI YA KUPAKIA MBAO NA KUHESABU UKU UNAJIFUNZA HII BUSINESS.
 
Mbona mapema mno? Hata madogo bado wanakuita “Kaka” tayari umeshaanza kulalamika? Subiri kidogo uanze kugombania nao vitumbua au waanze kumtongoza demu wako huku wakiwmambia huna mchongo na ulipo Mshua amepanga kukupeleka kijijini ukakae na bibi.
 
Ubarikiwe mkuu
 
Anza biashara ya umachinga.. Fungua duka uza herenj, chupi, boksa, saa nenda chimbo chukua mzigo kwa hiyo hela anza nayo faida ni nzuri
 
😀😀 Punguza ukali mkuu.
Kipindi hicho ndo utajua vitu vingine ni bidhaa.
 
Mkuu jaribu kujichanganya na watu, mtaji wako unaweza ona ni mdogo lakini kuna watu wana idea ila hawana mtaji, Jimix utakutana na watu wa aina hiyo ili uvumbue fursa mbalimbali pia.
"Usijifungie ndani WATU NI FURSA"
 
Mkuu iyo biashara mtaji wa chini kuanzia inaweza kua sh ngapi?
 
Daah! hii moment unayopitia ni ngumu ila haina jinsi jaribu uangalie fursa iliopo hapo ulipo na uifanyie kazi maana "unabarikiwa mkono ufanyao kazi"
 
Bwana mdogo mbona una lose control mapema sana, m nmemalza chuo 2016 mwanzon nlijrb kutafta shughul znazoendana na taaluma yng lkn baadae nlgundua napoteza muda, hvyo nkaamua kufanya vtu vngne kwaxx Nashukuru
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…