Kuna watu wanafanya kazi wakitoa nauli ya kwenda na kurudi kazini, hela ya chai na lunch na dinner kwa mwezi mzima hapakiwi hata na elfu 50 ya akiba.
Sasa unakuta mdada huyu anaishi, anakula, ananunuliwa nguo, akiumwa anapelekwa hospital, family ikiwa na mitoko na yeye anatolewa out nk. Mwezi mzima ameishi na bado ana 60k yake haijaguswa, mbona hainw shida?
Btw wapo watu ninaowajua wanalipa wadada wao 100k+ lakini hao wadada wanafanya kazi kama punda. Na hamna cha nguo wala kutibiwa wala kula vizuri.