Natafuta mganga wa kienyeji konki

Ni kweli ila lazima ashughulikiwe. Mtu atakuoneaji hivi hivi nyakati hizi?
Nilisimuliwa story moja hivi. Jamaa mmoja alipata mwanamke wa Kiiraq (Mbulu). Jamaa kazi zake ni hizi za vitunguu, kushona magunia na kubeba magunia ya vitunguu. Ilikuwa Karatu. Wakatoka wakaenda Arusha mjini wakapanga chumba maisha yakaendelea.
Mwanamke alipopata ujauzito jamaa akamkimbia. Kilichofuata jamaa ni marehemu sasa (Mwanamke alimuua)
Huko huko alipokuwa alitumiwa kombora na watu wakazika.
Njoo kwenye maombi; mpende adui yako kama unavyojipenda wewe
 
Hapa mcheki mshana tu
 
Kuna sehemu moja kule korogwe vijijini inaitwa Kwalukonge,kwa wale wanaoifahamu njia ya kaskazini basi unaingilia pale ilipokua hotel maarufu Liverpool...kwa mbali kuna mlima..sasa nyuma ya ule mlima kuna vijiji huko kuna wazee wana kufuru sana.

Nakumbuka miaka kadhaa nyuma kuna jamaa yangu mmoja alikuja akataka asindikizwe huko kwa madai amedhulumiwa kwenye biashara yake ya madini..anyway kupunguza maneno mengi kufika kule yule mtaalam wala hakua na maneno mengi...aliuliza tu unatakaje? Kilichofuata ndio niliamini kuna dunia zaidi ya hii tunayoijua...hizi habari zisikie tu..ila kuna wazee wanajua..nakumbuka wakati tunarudi jamaa njiani anapigiwa simu anapewa taarifa kuhusu mbaya wake..
 

Ndio hivyo haya mambo yapo...tuishi na watu vizuri,amani ni muhimu ukijifanya mjanja kuna watu hawakuachii
 
Nimegundua watanzania haya mambo wanafanya sana tu
Namba ya imma imeombwa kama njugu huko chuma binafsi
Hahahaha 🤣🤣🤣🤣🤣 msije mkasema nimewasema...sinaga tabia hizo na sitawasema.
Ila nomefurahi tu kuona watu wanaukana unafiki
 
Ndo uweke hapa makoneksheni hayo
Sema kama ni mda mrefu sana basi ukute alishafariki mganga mwenyewe
 
Usisemee mioyo ya watu,pengine na mimi nimesharogwa sana tu,usiyoyajua yasikupe shida
Hapa jambo ni moja tu na lazima likamilike hakuna ushauri wa kurudi nyuma
Dunia ndio hii na sisi ndio walimwengu
Vingapi ulivyokuwa umevipanga lazima vitimie lakini viliishia hewani?

Kwa roho hizi namshukuru sana Mungu kutohangaika na Michepuko kwa zaidi ya miaka mi4, bila shaka nanusurika na mengi sana.

Mungu nisaidie niendelee kudumu na ndoa yangu pekee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…