Ila ww mwenzetu duuh!! Umedhamiria, balaa!! But I hope ni kwania njema mkuu!!
Mm mwenyewe nimesoma enzi JKT imefutwa. Majuzi wameirudisha kwa lazima nikafurahi huenda na sisi wa makazini tutalazimishwa kwenda JKT hata mwezi 1.
Nakumbuka Walimu Grade A na Form Six leavers wakawa wanalazimishwa kwenda, au usipo enda ukimaliza chuo uende kambini kwako kwa zamani kumaliza zamu lasivyo ajira hakuna.
Majuzi tu CCM wamegundua JKT inaenda kuwatoa madaraka; vyombo vya ulinzi vingekuwa vinachezea kichapo toka kwa Raia wema balaaa; yaani ya siku hizi imekuwa mdebwendo siyo tena lazima, hadi uombe. Dogo mmoja kasema yale mafunzo magumu yamepunguzwa-mkienda kule mnafunzwa hasa kulima, kuvuna, na ukakamavu tu.
Nilitaka niende kule ili angalau niwe nawapa adabu Vibaka (Kujilinda) waliojaa Tz hii. Siyo wananikuta mikono laiiiini utadhani mtoto. Kujua kutumia silaha (iwapo nitakuja kuimiliki kihalali). Pia huwa sipendi uonevu (waonevu niwe nawapa vichapo).
Jameni hivi still naweza kwenda Jeshini kuomba kuungana na wale mgambo wao (wale wa jiji na wa kulinda taasisi) na wakanikubali kujifunza?