Natafuta Military Academy for Private Military Training

Asante sana kwa ushauri, hakika nimepata kitu. lakini ningependa nimpeleke kwenye military academy ili apate mafunzo yatayomsaidia maishani mwake. nimeshamwandaa kisaikolojia and he seems ready for it! Dunia hii inazunguka kwa kasi sana, nahisi mgambo na JKT havitoshi...otherwise, natanguliza shukrani mkuu.
 

Kauli ya kwamba Mgambo na JKT havitoshi unakosea sana na kwa kukusaidia tu basi hakuna mahala ambapo Wapiganaji hupewa Mafunzo ya nguvu na ya kufa Mtu kama hayo ya Mgambo na JKT na kama kuna Mtu hapo karibu yako ambayo anayajua ' Majeshi ' ya Tanzania na aina za Mafunzo yake muulize na atakuambia. Tena usije kushangaa huko Mgambo na JKT hao Vijana wanafunzwa ' Kimedani ' na ' Kiukakamavu ' zaidi kuliko hata huko Jeshini kwenyewe JWTZ na TMA.
 
mkuu, huenda uko sahihi. Lakini hakuna kisichokuwa na faida ulimwengu huu. hata comedians huwa wanacheka tu na mwisho wa shoo wanavuna hundred/thousands of dollars. Let me think about it...once again, thank you
 
Ila ww mwenzetu duuh!! Umedhamiria, balaa!! But I hope ni kwania njema mkuu!!

Mm mwenyewe nimesoma enzi JKT imefutwa. Majuzi wameirudisha kwa lazima nikafurahi huenda na sisi wa makazini tutalazimishwa kwenda JKT hata mwezi 1.

Nakumbuka Walimu Grade A na Form Six leavers wakawa wanalazimishwa kwenda, au usipo enda ukimaliza chuo uende kambini kwako kwa zamani kumaliza zamu lasivyo ajira hakuna.

Majuzi tu CCM wamegundua JKT inaenda kuwatoa madaraka; vyombo vya ulinzi vingekuwa vinachezea kichapo toka kwa Raia wema balaaa; yaani ya siku hizi imekuwa mdebwendo siyo tena lazima, hadi uombe. Dogo mmoja kasema yale mafunzo magumu yamepunguzwa-mkienda kule mnafunzwa hasa kulima, kuvuna, na ukakamavu tu.

Nilitaka niende kule ili angalau niwe nawapa adabu Vibaka (Kujilinda) waliojaa Tz hii. Siyo wananikuta mikono laiiiini utadhani mtoto. Kujua kutumia silaha (iwapo nitakuja kuimiliki kihalali). Pia huwa sipendi uonevu (waonevu niwe nawapa vichapo).

Jameni hivi still naweza kwenda Jeshini kuomba kuungana na wale mgambo wao (wale wa jiji na wa kulinda taasisi) na wakanikubali kujifunza?
 
mkuu, huenda uko sahihi. Lakini hakuna kisichokuwa na faida ulimwengu huu. hata comedians huwa wanacheka tu na mwisho wa shoo wanavuna hundred/thousands of dollars. Let me think about it...once again, thank you
Africa ni sehemu tofauti sana na sehemu zingine Duniani Africa mwanafunzi anasoma kwa kujua kile anachosomea kitamfaidisha vipi tofauti na wenzetu wanasomea kitu kwa ajili ya kuongeza Maarifa na Ufahamu

Kama unataka vyuo vya nje kesho nikupe mawasiliano yao then utawasiliana nao kwa hapa Option pekee ni JKT na wenzie na huko ni Military Training mafunzo ya ukakamavu na matumizi ya Silaha za Moto na Baridi tu

Mengine ya Darasani ni mpaka vyuo vya kijeshi Arusha au Dar
 
Mnaandaa terrorist siyo,au Snipers, jitambulishe vizuri wewe nano na huyo ni nani je wewe siyo takibiiiiiiiir,vyuo vipo vingi nje ya nchi ila jitambulishe tatizo hizo ID zenu.
 
ni kweli mkuu, nimedhamiria haswa na ndo sababu nikaamua ku-share na wanazuoni wa JF. Binafsi naona mbali kidogo na ndiyo maana nikamzuia kutafuta kazi kwanza mpaka tutakapofika hatima ya hili. nimeishi na jamii ya watu mbalimbali na nimeona life style zao na wengi nchini mwao walienda jeshini or wana mafunzo ya kijeshi. kama mzazi, namwandaa ili naye aje kuwaandaa wadogo zake na watoto wake atakayewazaa...
 
Imekaa vyema ndg, Pambana umpeleke JKT. Kuna kambi ya Kigoma huko ndio niliona wanafundishwa mazoezi magumu hadi kutembelea Tumbo wakiwa ndani ya wavu mrefuuuu kama m50 au m100 hivi.
 
mkuu, nitashukuru ukinipa mawasiliano yao. respect bro
 
Imekaa vyema ndg, Pambana umpeleke JKT. Kuna kambi ya Kigoma huko ndio niliona wanafundishwa mazoezi magumu hadi kutembelea Tumbo wakiwa ndani ya wavu mrefuuuu kama m50 au m100 hivi.
huko wanasoma/ ku-train mafunzo kama Land warfare: force-on-force with the use of FX Simunition pamoja na Advanced Firearms Training - Live Fire contactt Drills? kama una taarifa kamili ya kozi wanazosoma JKT ninaziomba kama hutojali...bless up
 
huko wanasoma/ ku-train mafunzo kama Land warfare: force-on-force with the use of FX Simunition pamoja na Advanced Firearms Training - Live Fire contactt Drills? kama una taarifa kamili ya kozi wanazosoma JKT ninaziomba kama hutojali...bless up
Sina mkuu.
 
Kwa maelezo yako kwann wewe mwenyewe usianzishe chuo chako cha kijeshi maana naona hadi curriculum unayo tayari...mzee wewe itakuwa commandoo unataka kumfundisha mwanao mbinu za kijeshi kuwa wawili muje kufanya mapinduzi....nahisi kina Fidel Castro wanaandaliwa kuja kufanya mapinduzi Tanzania. ...
 
mkuu, hilo la kuanzisha chuo cha kijeshi haliwezekani abadani. ila ni kwa nia njema tu nataka nimwandae dogo aje kuwa "something" kwenye jamii. najaribu kuona mbali kwa darubini kali...
 
jaribu KK security mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…