Natafuta Mshirika wa Biashara ya Chips Tabata Kinyerezi

kuna watu bado tuna uaminifu(na mimi najiwekamo kwa sababu najijua)

ninaweza kusimamia vizuri biashara ya mtu bila kumpiga shida inakuja kwenye malipo, akijipendelea tu matatizo yanaanzia hapo
Nakubali waaminifu wapo ila ni wachache sana, lakini haiondoi ukweli kuwa biashara inamuhtaji sana mmiliki wake kwa ukaribu.
 
JAMANI NDUGU JAMAA NA MARAFIKI BADO SIJAPATA WA KUINGIA NAE MKATABA WA KISHERIA JUU YA BIASHARA YA CHIPS NA MBUZI CHOMA HAPA TABATA KINYEREZI SENTA JUU YA ENEO NILILO NALO.
 
Kirahisi rahisi hivyo?
 
Kwa waafrika bado sana, anaweza kukimbia na kila kitu, au akakuroga uchawi wa "kiatu" ukajikuta bila ufahamu wako unaondoka tu Dar ,na hela yako hutaifuatilia, anakufunga kabisa akili, au anakufanya zezeta.

Fanya mwenyewe au na mtu wako wa karibu saaana, au simamia mwenyewe.

Mwafrika ni kiumbe hatari sana
 
Mkuu Gerald huwenda kweli una nia nzuri ya kushirikiana na mtu katika wazo lako hilo, ni jambo zuri sana. Changamoto hapa ni uaminifu tu, sio rahisi watu mmekutana humu kwa haraka tu mkafanya jambo lenu. Wengine uaminifu bado tunao, hebu niaminishe kuhusu wewe. Niko tayari tupige kazi.
 
Huyu jamaa kwa maandishi yake sidhani kama ana utimamu wa akili
 
Yaani wewe unataka upate mtaji kupitia mtu/mshirika wako baadae mje muanze kusumbuana..mimi nikajua unamuuzia kieneo hicho jamaa afanye biashara. Sasa kumbe unataka mambo ya % na ilihali jamaa kanunua mahitaji.Alafu ukishapata mtaji uanze kumzingua mtu.

Hii ni ngumu sana.Kama umeshindwa kuendesha biashara kutokana na mtaji huna muuzie mtu eneo afanye biashara yeye kama yeye.
Vinginevyo utazua ugomvi wa kimaslahi. Hilo nimeliangalia Kwa jicho la Tatu (Kiroho zaidi)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…