Natafuta muwekezaji

Natafuta muwekezaji

Mkuu unatafuta muwekezaji JE,Muwekezaji atakuwa MMILIKI?Atamiliki percent ngapi?Je kama sio mmiliki utakuwa ni mkopo?Mkopo wa muda gani na masharti gani?Kusema tu ela itakuwa mara mbili haitoshi.Kuhusu mikatabansio tatizo tatizo ni masharti ya huo mkataba.

Mimi naweza kukupatia kiasi hicho cha PESA kwa makataba wa Mwezi mmoja dhamana iwe asset kama vile gari au kiwanja au nyumba na nitahitaji faida ya 10% kwa mwezi sio zaidi.Vipi Utayaweza hayo masharti?
Kongole kwa maswali mazuri mkuu, niseme tu kwamba kuna mambo naepuka kuyaanisha hapa kwa sababu za maslahi lakini nitajaribu kukujibu kiufasaha hapa na pia nitajongea PM tuzungumze zaidi.
1.Naona umejikita zaidi kwenye mkataba na nikutoe hofu tu kwamba kama kutaonekana kuna haja ya kubadili, kuongeza ama kupungza kipengele chochote kwenye mkataba basi hakutakuwa na budi ya kufanya hivyo.
2.Muwekezaji anakuwa mmiliki ambae atakuwa na baadhi ya haki.
3.Kuhusu asilimia ni kwamba anakuwa anamiliki asilimia 46(46%) lakini hofu ipo kwa wasimamizi wa mkataba(serikali) kwa maana kwamba yawezekana suala la asilimia likawa na ukakasi kwao kwa sababu ya kukosa uzoefu ama uelewa wa kutosha na hivyo basi kiasi utakacho kuwa unakipata kama muwekezaji kitakuwa hakibadiliki(fixed) mfano wa mikataba ya boda boda na bajaj ilivo.
4.Kuhusu suala la mkopo ni kwamba kama kiasi hicho kinapatikana kwa mkupuo na masharti ni yenye ahueni basi naweza weka pembeni suala la uwekezaji na kwenda na mkopo.
 
Mzeya chukua mkopo huo
 
Unaweza elezea zaidi boss
Investor anaangalia kufanya pesa yake iwe mara 10 zaidi na kuendelea. Wewe unatoa ofa ya kuifanya iwe mara mbili tu. Kwa kiwango cha 3.5 million si investor unatafuta bali unatafuta mkopo. Unaweza kwenda kwenye taasisi ya mikopo ya karibu na wanaweza kukusaidia zaidi.
 
1.Suala la mara ngapi investor (muwekezaji) anataka pesa yake iwe ni jambo moja lakini jambo jingine ni kwamba mrejesho wa pesa ya muwekezaji unaisha/kuiva(mature) lini ndo haswa lenye uzito kwa sababu inawezekana pesa yako ikawa mara mbili ya kiasi ulichowekeza ndani ya muda mfupi sana ama ikawa mara 10 au hata mara 20 ndani ya muda mrefu.
2.Suala la kiasi cha pesa nadhani hapa ndipo madhara ya ukoloni yanapoonekana kwa maana kwamba tunadhani muwekezaji ni yule anayeweka mabilioni ya fedha katika biashara au mradi na wengine huwa wanaenda mbali kudhani kwamba inabidi awe mtu toka magharibi au masahriki ya kati na Uchina.
 
Yawezekana Simon999 hauko peke yako kudhani kwamba hili ninalolifanya ni jambo jipya ama siko sahihi na ndio maana unashauri mambo ya mkopo.
Kwa faida yako wewe binafsi na wengine wenye mtazamo kama wako ni kwamba ninaemtafuta hapa kwa kimombo anaitwa "angel investor" na hawa wamekuwako kwa miaka mingi katika nchi zilizoendelea.
 
Mzeya chukua mkopo huo
kama anapata 35,000 kwa siku inamaana kwa mwezi ni million 1 na 50k
kwaio mkopo wa mwezi mmoja hautomtosha na hapo kumbuka ajajilipa, ajanunua vitu vinavyohitajika katika uzalishaji.

Hio hela ili irudi tupigie 6 month
 
Fatilia hizi comments mtu anayekuja kucomment coment ya 19 mng’ang’anie anayo pesa na yupo radhi kuwekeza.. nakusisitiza usimuache mkuu akikoment tu mfate inbox moja kwa moja.. akikoment vyovyote vilee muendee inbox
Naona uliamua kututambulisha ID yako nyingine
 
Wazo zuri ila watanzania kuwekeza ni wagumu sana

Ila kuwa mvumilivu watakuja wenye nia
Watanzania wamechoshwa na watu wanaokuja na lugha nzuri za kuvutia uwekezaji ukishaweka hela zako zinafuata dana dana mfano Mr Kuku QNet Jatu etc kwa hiyo sio kuwa ni wagumu Wana woga wa kupigwa
 
Back
Top Bottom