Kulea mwenyewe sio ujanja dada,ungejua taabu na madhara wanayokuwa nayo hawa watoto wa kulelewa na mzazi mmoja usingetamani kumwingiza mwanao mpendwa kwenye aina hiyo ya maisha,iwe bahati mbaya jamani si kupanga kama utakavyo. Kuna teenager namfahamu amelelewa vizuri ana kila kitu muhimu lakini ukikaa naye siku zoote mkitulia akawaona watoto wako na wazazi wao wawili anaumia saaana, ana maswali mengi sana juu ya babayake alipo,anasema baba yangu angekuwepo ningempenda sana,mara ..hao watoto wana raha sana wako na baba yao.Jamani wanawake msipende kuiga maisha ambayo hayako kwenye mpango wa Mungu.