Natafuta Mwekezaji katika biashara yangu

Natafuta Mwekezaji katika biashara yangu

Inategemea na Nguvu ya mwekezaji hii biashara inahitaji kadili unavoweka pesa kubwa na faida inapanda zaidi ila kuanzia milioni 10 kwenda juu hivi ndo vizuri zaidi lakini maongezi yapo kama itakuwa ni kuweka kwa awamu
Mkuu, wewe unahitaji mtaji kuanzia 10M na kitu pekee ambacho wewe umewekeza ni hizo line za uwakala na vifaa vya ofisi tu.

Maswali yangu ni:-

1. Hizo line za uwakala & vifaa vina thamani ya hiyo 10M?

2. Kama havina thamani hiyo, ni kwa nini mwekezaji awekeze kwako wakati anaweza kufungua biashara yake mwenyewe na commission atakayoipata itakuwa ya kwake 100% na hawazi kutapeliwa hela yake?

3. Nje ya kuandikishana kwa mwanasheria, ni kitu gani ambacho utaweka dhamana kwa mwekezaji?

4. Hapo juu umesema hiyo frame ipo kwenye eneo la nyumbani kwenu kabisa. Kwa nini hujataka kuwaomba ruhusa wazazi/walezi utumie hilo jengo kama dhamana ya kupata mkopo bank?
 
Inategemea na Nguvu ya mwekezaji hii biashara inahitaji kadili unavoweka pesa kubwa na faida inapanda zaidi ila kuanzia milioni 10 kwenda juu hivi ndo vizuri zaidi lakini maongezi yapo kama itakuwa ni kuweka kwa awamu
Kwanini mtaji wako ulikata? Hapa mtu akiweka mtaji atarajie kupigwa au kuleta mgogoro mbaya sana.
Kwa kukushauri kakope benki au saccos e.t.c weka mtaji wako..

Eti kila kitu unasimamia wewe kirahisi rahisi tu wakati wewe una laini na fremu mtu aweke 10M haya masihara.Huu ni utapeli na Ukanjanja kabisa kuita mwanasheria njaa na kutengeneza fake documents au kusaini mbele ya mashaidi hakuondoi dhana kuwa ni utapeli na mara nyingi kesi za madai huwa mbaya sana.

NB; Mjini mambo mengi mtu anatumbukiza 10M from Nowhere hamfahamiani kivile alafu kesho keshokutwa anarudi pale unambiwa huyo mtu hatumjui hapa na wala hajawahi kuwa hapa( fake ofisi).Unataka mtu avae boksa kichwani e.t.c
 
Habari Zenu Wakuu, Mimi ni Mfanyabiashara wa Biashara ya UWAKALA ( Electronic Money Transactions ), nina uzoefu nayo sana toka mwaka 2018.

Ipo miamala ya simu kama; Tigo Pesa, M-Pesa, Airtel Money, T-Pesa, HaloPesa na Azam Pesa

Pia miamala ya Bank kama; CRDB, NBC, NMB, TCB, UBA, ACB, AMANA, EXIM, EQUITY, AZANIA, MKOMBOZI na STANBIC

Nachohitaji ni Mwekezaji wa Mtaji ( CASH ) ili tuweze kutengeneza faida na kugawana kwa makubaliano maalum. Fremu ya Biashara ipo Barabarani kituo cha mwendokasi, sehemu ambayo ni njia panda kwenye mzunguko mkubwa wa Biashara. Nilichokosa ni mtaji tu ila vitendea kazi vyote vipo na wateja ninao wengi sana changanya na wapita njia Kwasababu ni kitua cha abilia, lete mtaji tugawane faida na nguvu kazi mimi mwenyewe. Tunaandikishiana Mbele ya Mashahidi pande zote mbili na ikibidi mbele ya Mwanasheri, Siku unaamua kutoa Mtaji wako, unauchukua kama ulivyo haipungui hata senti moja kwasababu hii sio biashara ya kununua bidhaa.

Na Upigaji Wa Hesabu ni mwepesi kwasabu nadili na miamala tu hivyo ukiweka pesa yako inabidi isipungue bali iongezeke kutokana na kamisheni tutazotengeneza.

Faida (kamisheni) ikitoka haina kificho kwasabu wanakutumia.

ujumbe wa faida yako (Kamisheni) mwisho wa mwezi. Bahati mbaya sms imefutika, tunapiga simu mtandao husika na wanakutajia kamisheni yako.

Mawasiliano 0768 828082, hii Namba ina WhatsApp pia
Daah hongera mkuu
 
Mtagawana faida pekee..hasara vipi, hasara ya chums ulete, matapeli na wizi. Hiyo biashara unaweza tengeza faida ya laki ukaibiwa milioni.
Hapo sasa ndo watu watatoana roho! Hili jambo nimeliangalia kiroho kama ni lenye kuleta amani. Moyo umegoma kabisa...hapo watu watachinjana na kurogana kabisa...
Mtu una 10M si unafanya biashara yako kabisa kwani Inagharimu kiasi gani laini za simu, ofisi na vifaa. Labda huyo mtu asiwe mjasiliamali.
 
Biashara ya mmoja kuweka pesa na mwengine kuweka maneno haijawahi kuwa na mwisho mzuri 😁
Anaweka maneno na Laini zake pamoja na eti location kwamba kuna flow ya watu nzuri tena karibu na mwendokasi mbona mtaji wake ulikata kama angekua anatengeneza faida?. Hii ni ngumu kumeza hata mwenye mtaji akiweka apimwe vizur akili.

Kasema kila kitu atakua anasimamia yeye wakati mara ya kwanza biashara imekufa..jamaa janja sana huyu..unajikuta mtu kaweka 10M faida ya miamala yote anambiwa 400k na maneno kibao sijui chuma ulete, sijui kaja mtu kutoa kumbe n mwizi, mara kuna shoti imeingia.
Hapo mtu anaweza geuka mbogo!
 
Haya sasa mtu anawekeza 10M wiki haifiki ujambazi unatokea mtu anaporwa tena.Si mtu utajua kabisa huyu jmaa kahusika moja kwa moja..Kinachofuata hapo ni nini...kama sio mauaji na kuharibiana maisha.
Wengi wanaachiwa roho zao ila ukianza kujifanya mjuaji upambane nao, chuma kinakuhusu
Maana wanakuja wamejipanga kwa lolote hata kupambana na polisi
Yaani unakufa kisa hela bora kuifunga tu
 
Uaminifu ni kipengele mno kwa sisi wabongo.
Chief mi binafsi yashanikuta kuna dogo wa kitaani alinifuata niwekeze kwenye biashara yake ya kuingiza nyimbo ( kipindi kile ipo hot) kwa makubaliano ya kunipa elfu kumi kila siku.

Fremu ilikuwa ni ya nyumbani kwao kwa io mi kazi yangu ilikuwa kununua vifaa vya ofisini ikiwemo kompyuta, spika na vitu vinginevyo

Huwezi amini yule dogo alinipa hela miezi miwili ya mwanzoni baada ya hapo alikuwa ananipiga sound ilhali ofisi ilikuwa busy vibaya sana yaani hyo elfu kumi kwake haikuwa ishu coz alikuwa ana wateja wengi sana

Mwisho wa siku tuligombana ugomvi mpaka polisi baada ya kuniporomeshea matusi ya nguoni mbele ya wateja.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
wewe ni mimi. hizi kenge za kuitwa watanzania siwezi kufanya nao biashara tena. humuhumu kuna nyau 2 zililala mbele. moja ni lisukuma linajiongelesha kifalafala alikua muaminifu miezi 3 tu baada ya hapo vumbi.
mimi ndio maana hela zangu nawekeza tu kwa govts bonds sitaki shida na matanzania.
 
Chief mi binafsi yashanikuta kuna dogo wa kitaani alinifuata niwekeze kwenye biashara yake ya kuingiza nyimbo ( kipindi kile ipo hot) kwa makubaliano ya kunipa elfu kumi kila siku.

Fremu ilikuwa ni ya nyumbani kwao kwa io mi kazi yangu ilikuwa kununua vifaa vya ofisini ikiwemo kompyuta, spika na vitu vinginevyo

Huwezi amini yule dogo alinipa hela miezi miwili ya mwanzoni baada ya hapo alikuwa ananipiga sound ilhali ofisi ilikuwa busy vibaya sana yaani hyo elfu kumi kwake haikuwa ishu coz alikuwa ana wateja wengi sana

Mwisho wa siku tuligombana ugomvi mpaka polisi baada ya kuniporomeshea matusi ya nguoni mbele ya wateja.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
Maana aliona kama anakupa hela bure eeh
 
Back
Top Bottom