Mkuu, wewe unahitaji mtaji kuanzia 10M na kitu pekee ambacho wewe umewekeza ni hizo line za uwakala na vifaa vya ofisi tu.Inategemea na Nguvu ya mwekezaji hii biashara inahitaji kadili unavoweka pesa kubwa na faida inapanda zaidi ila kuanzia milioni 10 kwenda juu hivi ndo vizuri zaidi lakini maongezi yapo kama itakuwa ni kuweka kwa awamu
Maswali yangu ni:-
1. Hizo line za uwakala & vifaa vina thamani ya hiyo 10M?
2. Kama havina thamani hiyo, ni kwa nini mwekezaji awekeze kwako wakati anaweza kufungua biashara yake mwenyewe na commission atakayoipata itakuwa ya kwake 100% na hawazi kutapeliwa hela yake?
3. Nje ya kuandikishana kwa mwanasheria, ni kitu gani ambacho utaweka dhamana kwa mwekezaji?
4. Hapo juu umesema hiyo frame ipo kwenye eneo la nyumbani kwenu kabisa. Kwa nini hujataka kuwaomba ruhusa wazazi/walezi utumie hilo jengo kama dhamana ya kupata mkopo bank?