Sognsvann
Member
- Apr 3, 2025
- 49
- 115
Mimi ni mwanaume mpole, mnyenyekevu, nipo kwenye umri wa miaka 40 ya awali (early 40s). Natafuta mwenza(mwanamke) wa maisha kwa ajili ya uhusiano wa kudumu unaoelekea kwenye ndoa. Ninathamini upendo wa kweli, uaminifu, na ukuaji wa pamoja.
Kuhusu Mimi:
Ninatafuta mwanamke mwenye maadili na malengo yanayofanana au kuelekeana na yangu; aliye tayari kwa safari ya maisha ya pamoja. Mwenza huyo anapaswa kuwa na sifa zifuatazo:
Utakaponitumia ujumbe, tafadhali naomba unielezee wewe ni nani na wajihi (sifa) wako ulionao, ikiwepo umri, dini, elimu yako, unajishughulisha na nini, unapatikana wapi na mengineyo ambayo utaona yanafaa kwa mtu kuweza kukufahamu vema.
Natarajia kukutana na mwanamke sahihi wa maisha yangu ambaye tutajenga familia bora.
Asante sana na karibuni kwa moyo mkunjufu.
Kuhusu Mimi:
- Ni mwanaume ninayejiheshimu na pia ni mtu mwenye heshima katika jamii inayonizunguka, ni mtu mwenye malengo chanya na mwenye maadili.
- Vile vile ni mtu mwenye maono na shauku ya kuwa na maendeleo ya kibinafsi na ya kifamilia,
- Nina shahada ya juu kutoka Chuo kikuu
- Nina ajira ya kudumu katika taasisi ya umma na najitegemea kifedha.
- Nimejikita katika kujenga maisha yenye uthabiti na mafanikio.
- HALI YA MAHUSIANO: Nina watoto wawili, naishi nao na dada wa kazi ndio amekuwa kama mama wa hawa watoto; hivyo kwa sasa nahitaji mwanamke ambaye atakuwa MKE na pia atakuwa na upendo na watoto wangu.
Ninatafuta mwanamke mwenye maadili na malengo yanayofanana au kuelekeana na yangu; aliye tayari kwa safari ya maisha ya pamoja. Mwenza huyo anapaswa kuwa na sifa zifuatazo:
- Imani na Tabia – Awe mcha Mungu (Mkristo au Mwislamu), mwenye umri kati ya miaka 25 hadi 35.
- HALI YA MAHUSIANO – AWE HANA MAHUSIANO MENGINE KABISA(Completely single woman); AU IKIWA ANA MTOTO BASI ASIZIDI MTOTO MMOJA.
- Elimu na Kazi – Awe na elimu ya chuo (Stashahada, Shahada, au Shahada ya Uzamili) ya fani yeyote ile, na awe anafanya kazi serikalini, sekta binafsi, au kujiajiri.
- Utayari wa Maisha ya Pamoja – Awe tayari kuhamia na kuungana nami na kujenga maisha pamoja kwa kujitoa kwa moyo mmoja na sio kujaribu maisha ya ndoa.
- Afya na Ustawi – Awe tayari kufanya vipimo vya VVU pamoja na vipimo vingine muhimu kwa ajili ya kulinda afya zetu leo na baadae.
- Mambo Mengine ya Kipaumbele – Itapendeza zaidi ikiwa atakuwa ni mtu mwenye maadili, msikivu, na aliye tayari kushirikiana katika kila hatua ya maisha.