Natafuta mwenza (Mke) wa maisha kwa Uhusiano wa Kudumu

Natafuta mwenza (Mke) wa maisha kwa Uhusiano wa Kudumu

Halafu Shem acha utani basiiii , nasikia pande hizo ukipata "MKE" ni "WIFE MATERIAL KWELI", naamini shem utanifanya niwe mtu wa furaha siku zote za maisha yangu
Tatizo shem umekua msiri sana hautaki kabisa upande wako ujulikane yani haya mahusiano ni one way ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

Basi walau picha ya kaburi watoto tutalea tu
 
Nadhani maelezo yangu yapo very clear, and very strict: ASIWE NA MTOTO AU WATOTO.

Watu waache kuuliza maswali ku-justify matatizo yao au changamoto zao ili waweze kukubalika. They have to read between the lines and understand the criteria for assessment.
Na wewe kwa nini ulete shida zako hapa JF ya uhitaji wa mwenza?

Halafu ukihojiwa maswali unaleta zakuleta.

Kwani unafikiri wanawake wanashida yaku kukubali wewe?

Wewe si ndio mwenye shida mpaka umeandika uzi hapa?

Sasa unaulizwa maswali hujibu.

Wewe ni single Faza una mtoto mahali unataka kuficha ficha hapa.

Na utapata single mother mwenzako. Maana ndio mnaendana.
 
Basi hata photocopy ya talaka tu tuone ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
Halafu Shem acha utani basiiii , nasikia pande hizo ukipata "MKE" ni "WIFE MATERIAL KWELI", naamini shem utanifanya niwe mtu wa furaha siku zote za maisha yangu
Na wewe kwa nini ulete shida zako hapa JF ya uhitaji wa mwenza?

Halafu ukihojiwa maswali unaleta zakuleta.

Kwani unafikiri wanawake wanashida ya kukubali wewe?

Wewe si ndio mwenye shida mpaka umeandika uzi hapa?

Sasa unaulizwa maswali hujibu.

Wewe ni single Faza una mtoto mahali unataka kuficha ficha hapa.

Na utapata single mother mwenzako. Maana ndio mnaendana.
ASANTE SANA MKUU ๐Ÿ™
 
Shem wewe na mimi tumetoka mbali sana, I hope you know me well. Hivyo kama kweli mke tarajali ana kidhi vigezo nilivyobainisha mimi sina tatizo. Mengine mwenyewe shem utakazia tu maarifa.
Mpe means of communication kama nilivyoainisha hapo kwa tangazo, then tutafahamiana na kuona the way forward maana assessment criteria zitazingatiwa ili tuweze kujenga mji bora na familia bora shem wangu
Hivi kwanini mnakuja na ID za kuzuga, mnaficha nini?
 
Nadhani maelezo yangu yapo very clear, and very strict: ASIWE NA MTOTO AU WATOTO.

Watu waache kuuliza maswali ku-justify matatizo yao au changamoto zao ili waweze kukubalika. They have to read between the lines and understand the criteria for assessment.
MUNGU akupe hitaji la moyo wako
 
Mimi ni mwanaume mpole, mnyenyekevu, nipo kwenye umri wa miaka 40 ya awali (early 40s). Natafuta mwenza(mwanamke) wa maisha kwa ajili ya uhusiano wa kudumu unaoelekea kwenye ndoa. Ninathamini upendo wa kweli, uaminifu, na ukuaji wa pamoja.
Kuhusu Mimi:
  • Ni mwanaume ninayejiheshimu na pia ni mtu mwenye heshima katika jamii inayonizunguka, ni mtu mwenye malengo chanya na mwenye maadili.
  • Vile vile ni mtu mwenye maono na shauku ya kuwa na maendeleo ya kibinafsi na ya kifamilia,
  • Nina shahada ya juu kutoka Chuo kikuu
  • Nina ajira ya kudumu katika taasisi ya umma na najitegemea kifedha.
  • Nimejikita katika kujenga maisha yenye uthabiti na mafanikio.
Mwenza ninayemtafuta (Mke tarajali)

Ninatafuta mwanamke mwenye maadili na malengo yanayofanana au kuelekeana na yangu; aliye tayari kwa safari ya maisha ya pamoja. Mwenza huyo anapaswa kuwa na sifa zifuatazo:
  1. Imani na Tabia โ€“ Awe mcha Mungu (Mkristo au Mwislamu), mwenye umri kati ya miaka 25 hadi 35.
  2. Hali ya Mahusiano โ€“ Asiwe amewahi kuolewa wala kuwa na mtoto au watoto.
  3. Elimu na Kazi โ€“ Awe na elimu ya chuo (Stashahada, Shahada, au Shahada ya Uzamili) ya fani yeyote ile, na awe anafanya kazi serikalini, sekta binafsi, au kujiajiri.
  4. Utayari wa Maisha ya Pamoja โ€“ Awe tayari kuhamia na kuungana nami na kujenga maisha pamoja kwa kujitoa kwa moyo mmoja na sio kujaribu maisha ya ndoa.
  5. Afya na Ustawi โ€“ Awe tayari kufanya vipimo vya VVU pamoja na vipimo vingine muhimu kwa ajili ya kulinda afya zetu leo na baadae.
  6. Mambo Mengine ya Kipaumbele โ€“ Itapendeza zaidi ikiwa atakuwa ni mtu mwenye maadili, msikivu, na aliye tayari kushirikiana katika kila hatua ya maisha.
Sihitaji uhusiano wa muda mfupi au wa kupita. Kama upo tayari kwa uhusiano wa kweli unaolenga maisha ya pamoja na kuanzisha familia, tafadhali nitumie ujumbe binafsi kupitia barua pepe: [email protected] au unaweza kunitumia ujumbe kupitia Jf.

Utakaponitumia ujumbe, tafadhali naomba unielezee wewe ni nani na wajihi (sifa) wako ulionao, ikiwepo umri, dini, elimu yako, unajishughulisha na nini, unapatikana wapi na mengineyo ambayo utaona yanafaa kwa mtu kuweza kukufahamu vema.

Natarajia kukutana na mwanamke sahihi wa maisha yangu ambaye tutajenga familia bora.

Asante sana na karibuni kwa moyo mkunjufu.
iNaonekana huna experience ya ndoa ww Binti mwenye shahada wa miaka 25 katakusumbua mpaka ...
 
iNaonekana huna experience ya ndoa ww Binti mwenye shahada wa miaka 25 katakusumbua mpaka ...
Kuna kitu kinaitwa moral values, kama ni binti aliyelelewa na wazazi katika maadili mema na kujua umuhimu wa kuolewa na kuwa mke na kujenga familia bora basi hilo ulisemalo halitakuwepo, na ikiwa ni wale wasichana wasiojielewa na kuona mwanaume kama kitega uchumi na kumtimizia shida zake za dunia huyo hatofika mbali kwa sababu criteria za assessment zitamtupa nje mapema sana na kujikuta yupo nje ya uwanja.

NB: Nipo makini katika hili jambo na wala sipo kufanya majaribio.
 
Asante sana ndugu, nia sio kuwa mbishi HAPANA, nilikuwa na nia njema tu kwa kumaanisha uhusiano wa kudumu ni NDOA ambayo inaanzia katika kuwasiliana na kufahamiana hatimaye wahusika wakishaelewana vema na kuwa na common vision, then wanafunga ndoa na hiyo ndio nilimaanisha dhana ya kuwa na uhusiano wa kudumu.

I am sorry kama utakuwa umekwazika lakini sikuwa na nia mbaya katika kulifafanua hilo jambo.
No need to apologize, kila mtu ana mtazamo wake. Fuatilia wako
 
Sema kama una mtoto au watoto ,chukua tu single mother hakuna kitu umepoteza...Kikubwa heshima maana ya dunia ni mengi.

Behind the scene ,hawa single mother wengi walidanganywa ndoa na matarajio yao yalikuwa ndoa...Elewa udhaifu wa kiasili wa mwanamke mbele ya mwanaume ,hii upelekea kudanganywa sana mwishoe kukimbiwa.
 
Back
Top Bottom