Natafuta mwenza (Mke) wa maisha kwa Uhusiano wa Kudumu

In case na wewe umewahi kuwa na watoto na unaficha ficha hapa. Basi usitegemee mwanamke ambaye hana watoto aje aungane na wewe.

Kama na wewe una mtoto mahali, komaa na huyohuyo uliyemzalisha.

Unataka kutafuta mwanamke asiye na watoto wakati wewe mwenyewe una mtoto.

NB: This is in case you have a child.

Kama huna mtoto kabisa then you are good to go.
Kwa kweli, 😂😂😂😂
 
Na wewe kwa nini ulete shida zako hapa JF ya uhitaji wa mwenza?

Halafu ukihojiwa maswali unaleta zakuleta.

Kwani unafikiri wanawake wanashida yaku kukubali wewe?

Wewe si ndio mwenye shida mpaka umeandika uzi hapa?

Sasa unaulizwa maswali hujibu.

Wewe ni single Faza una mtoto mahali unataka kuficha ficha hapa.

Na utapata single mother mwenzako. Maana ndio mnaendana.
😂😂😂😂😂
 
nime-update tangazo langu shem
Hapo imekaa sawa hadi namie nimetamani nijiweke sema tu kigezo kimoja kinaniondoa......

Kwahiyo shem kaburi lipo? Au ndo watu mpo zenu romantic mmepandishiana miguu mnalishana zabibu mara mama watoto anapiga simu anataka kuongea na watoto.
 
Mimi ni mwanaume mpole, mnyenyekevu, nipo kwenye umri wa miaka 40 ya awali (early 40s). Natafuta mwenza(mwanamke) wa maisha kwa ajili ya uhusiano wa kudumu unaoelekea kwenye ndoa. Ninathamini upendo wa kweli, uaminifu, na ukuaji wa pamoja.
Kuhusu Mimi:
  • Ni mwanaume ninayejiheshimu na pia ni mtu mwenye heshima katika jamii inayonizunguka, ni mtu mwenye malengo chanya na mwenye maadili.
  • Vile vile ni mtu mwenye maono na shauku ya kuwa na maendeleo ya kibinafsi na ya kifamilia,
  • Nina shahada ya juu kutoka Chuo kikuu
  • Nina ajira ya kudumu katika taasisi ya umma na najitegemea kifedha.
  • Nimejikita katika kujenga maisha yenye uthabiti na mafanikio.
  • HALI YA MAHUSIANO: Nina watoto wawili, naishi nao na dada wa kazi ndio amekuwa kama mama wa hawa watoto; hivyo kwa sasa nahitaji mwanamke ambaye atakuwa MKE na pia atakuwa na upendo na watoto wangu.
Mwenza ninayemtafuta (Mke tarajali)

Ninatafuta mwanamke mwenye maadili na malengo yanayofanana au kuelekeana na yangu; aliye tayari kwa safari ya maisha ya pamoja. Mwenza huyo anapaswa kuwa na sifa zifuatazo:
  1. Imani na Tabia – Awe mcha Mungu (Mkristo au Mwislamu), mwenye umri kati ya miaka 25 hadi 35.
  2. HALI YA MAHUSIANO – AWE HANA MAHUSIANO MENGINE KABISA(Completely single woman); AU IKIWA ANA MTOTO BASI ASIZIDI MTOTO MMOJA.
  3. Elimu na Kazi – Awe na elimu ya chuo (Stashahada, Shahada, au Shahada ya Uzamili) ya fani yeyote ile, na awe anafanya kazi serikalini, sekta binafsi, au kujiajiri.
  4. Utayari wa Maisha ya Pamoja – Awe tayari kuhamia na kuungana nami na kujenga maisha pamoja kwa kujitoa kwa moyo mmoja na sio kujaribu maisha ya ndoa.
  5. Afya na Ustawi – Awe tayari kufanya vipimo vya VVU pamoja na vipimo vingine muhimu kwa ajili ya kulinda afya zetu leo na baadae.
  6. Mambo Mengine ya Kipaumbele – Itapendeza zaidi ikiwa atakuwa ni mtu mwenye maadili, msikivu, na aliye tayari kushirikiana katika kila hatua ya maisha.
Sihitaji uhusiano wa muda mfupi au wa kupita. Kama upo tayari kwa uhusiano wa kweli unaolenga maisha ya pamoja na kuanzisha familia, tafadhali nitumie ujumbe binafsi kupitia barua pepe: [email protected] au unaweza kunitumia ujumbe kupitia Jf.

Utakaponitumia ujumbe, tafadhali naomba unielezee wewe ni nani na wajihi (sifa) wako ulionao, ikiwepo umri, dini, elimu yako, unajishughulisha na nini, unapatikana wapi na mengineyo ambayo utaona yanafaa kwa mtu kuweza kukufahamu vema.

Natarajia kukutana na mwanamke sahihi wa maisha yangu ambaye tutajenga familia bora.

Asante sana na karibuni kwa moyo mkunjufu.
Ndugu yetu upo sawa kiakili kweli?
 
Nimesoma andiko lako vizuri sana.Mimi naweza kukusaidia kumpata mtu atakayekufaa.Ukiona wazo langu linafaa njoo inbox utafurahi
 
Back
Top Bottom