Natafuta Partner kwenye biashara ya marudio (Uchenjuaji wa marudio ya Dhahabu)

Natafuta Partner kwenye biashara ya marudio (Uchenjuaji wa marudio ya Dhahabu)

Mkuu mm sio mgeni kwenye hii biashara....na usidhani ndo mara yangu ya kwanza kufanya...KAA KIMYA MKUU....HUJUI KITU KUHUSU BIASAHRA YA MARUDIO.
Hakuna utajiri wa makundi, ungekuwa sio mgeni wa biashara hiyo mpaka saivi usingehangaika kutafuta wawekezaji maana ungekuwa vizuri na ungefanya mwenyewe. Tetea hoja sio bla bla.
 
Wakuu habari zenu.


Nitaenda moja kwa moja kwenye mada, natafuta mtu ambaye nitashirikiana naye katika biashara ya uchenjuaji wa marudio ya dhahabu.

Marudio yapo maeneo ya Morogoro, marudio yenyewe yanasoma kati ya 1.2ppm-3.2ppm kwa hiyo average nakisia inaweza kuwa 1.8ppm ila itabidi kuyapima kwa mara nyingine ili kujiridhisha zaidi kabla hatujafanya uwekezaji wowote. Marudio yapo zaidi ya tani 600 kwa kuanzia.

Mimi nitahusika kwenye madawa ya uchenjuaji na partner ninayemtafuta atahusika kwenye manunuzi ya marudio, kwa kawaida kwa maeneo hayo marudio yanauzwa kwa trip ya gari.

Kwa trip moja ya gari la tani kumi na tano tunaweza nunua kati ya 100k na 200k, ukiweka na gharaza ya gari na upakiaji gari moja inaweza cost 300k Tsh mpaka marudio yanafika kwenye plant (VAT leaching plant).

Kimsingi mimi sina plant kwa hiyo itabidi kukodisha, gharama ya kukodi plant huwa ni maelewano kati ya mkodishaji na mwenye plant (waliofanya haya mambo wanajua).

Wale wachenjuaji mnakaribishwa.


Nimeona kuna jamaa anakuja na hesabu zake za kufikirika hapa, naomba niweke mchakato mzima wa hii issue ili kila kitu kiwe sawa.


GHARAMA ZA MADAWA
400kg Activated carbon......................................................................................................6,000,000
Pipa 8 za Sodium Cyanide@1,000,000.......................................................................8,000,000
Lime 150 bags@10,000...........................................................................................................1,500,000
Hydogen Peroxide..................................................................................................................... 120,000
Lead Nitrate......................................................................................................................................320,000 (hii sio muhimu ingawa)
Lab Reagents..................................................................................................................................500,000

MANUNUZI NA USAFIRISHAJI WA UDONGO/MARUDIO
600tons/15tons.....40trucks@300,000.............................................................................12,000,000

GHARAMA NYINGINEZO
Kupakia na kuopoa matanki....20tanks@100,000...................................................2,000,000 (kisio la juu sana)
Maji..........................................................................................................................................................2,000,000 (kisio la juu sana)
Kukodi Plant.......................................................................................................................................5,000,000
Mkemia..................................................................................................................................................1,000,000
Meals and accomodation.......................................................................................................1,000,000 (kisio la juu sana)
Gharama za elusion.....................................................................................................................1,500,000

TOTAL........................................................................................................................................................40,940,000
Contigency 5%................................................................................................................................ 2,047,000

G TOTAL..............................................................................................................42,987,000

TUJE KWENE UHALISIA SASA

600Tons@1.8g/t tukirecover 80%..............................................................864grams of Gold.
Purity ya dhahabu ni 85% (864*85%)......................................................734grams of Gold

MAUZO
Kwa bei ya leo gram moja ya gold inanunuliwa kwa 132,000Tsh baada ya kutoa commision ya muhindi

734g*132,000...................................................................................................96,940,800Tsh

KODI YA SAMIA
Hapa nitachukua 7%

96,940,800*7%..............................................................................................6,785,856

CHA MKONONI
96,940,800-6,785,856=================================90,154,944

EXPECTED FAIDA

90,154,944-42,987,000==================================47,167,944TSH

HII SIO HABA KWA KAZI YA MIEZI MIWILI JAMANI


MKUU ZERO UPO HAPO



Ujaweka gharama zifuatazo:

  • change of govt policies.
  • Risk.
  • Reality...
  • Matambiko.

Biashara sio rahisi kiwango hicho! Wote tungekuwa matajiri.
 
Mkuu mm sio mgeni kwenye hii biashara....na usidhani ndo mara yangu ya kwanza kufanya...KAA KIMYA MKUU....HUJUI KITU KUHUSU BIASAHRA YA MARUDIO.
Watu wenye tabia na ujuaji wako ndo husababisha watu honesty kuingia hasada na kufilisika.

Hakuna mfanya biashara timamu mwenye assurance kama zako! Uwekezaji ni jambo serious.
 
Sio mtaalam wa biashara za madini

Ila Kuna mwamba katoa Uzi wake wa majuto ya biashara ya madini,

Wengi wametoa comments zao naona zimekaa vibaya vibaya,zinatisha.

Binafs
Nakutakia kila la heri mkuu[emoji120]
 
Ujaweka gharama zifuatazo:

  • change of govt policies.
  • Risk.
  • Reality...
  • Matambiko.

Biashara sio rahisi kiwango hicho! Wote tungekuwa matajiri.
hahahahaaaaa
 
Sio mtaalam wa biashara za madini

Ila Kuna mwamba katoa Uzi wake wa majuto ya biashara ya madini,

Wengi wametoa comments zao naona zimekaa vibaya vibaya,zinatisha.

Binafs
Nakutakia kila la heri mkuu[emoji120]
Sawa mkuu...kila heri kwako pia katika shughuli zako
 
Watu wenye tabia na ujuaji wako ndo husababisha watu honesty kuingia hasada na kufilisika.

Hakuna mfanya biashara timamu mwenye assurance kama zako! Uwekezaji ni jambo serious.
Hya bwana
 
Ujaweka gharama zifuatazo:

  • change of govt policies.
  • Risk.
  • Reality...
  • Matambiko.

Biashara sio rahisi kiwango hicho! Wote tungekuwa matajiri.
Biashara sio ngumu kiasi hicho....ndo maana wengi ni maskini maana hatuna uthubutu....kila kitu kwetu ni UTAPOTEZA HELA
 
Sio mtaalam wa biashara za madini

Ila Kuna mwamba katoa Uzi wake wa majuto ya biashara ya madini,

Wengi wametoa comments zao naona zimekaa vibaya vibaya,zinatisha.

Binafs
Nakutakia kila la heri mkuu[emoji120]
KWenye biashara ya madini kuna watu wametusua mbaya mkuu....hukuna kitu ambacho hakina kupoteza chief...wewe kama umaeamua kuwa mfanyakazi endelea kuwa mfanyakazi...maana huku kwenye biashara sio kurahisi kiivyo...
 
Shida yako una wivu wa kike na mambo ambayo huna hata uwezo wa kuyafanya
Kwa lugha kama hizo unategemea kupata mwekezaji hauko serious, mimi nafanya hiyo kitu ila all in all hiyo biashara ni 50% 50%. Hamna mambo ya uhakika, jambo usilolijua usiliongelee mi nina uzoefu wa hiyo kazi na ninafanya hadi sasa. Maduara, plant vyote ninavyo....

98% ya wanaonunua marudio wanaangukia pua. Unabisha?
 
Biashara sio ngumu kiasi hicho....ndo maana wengi ni maskini maana hatuna uthubutu....kila kitu kwetu ni UTAPOTEZA HELA

Usiseme hivyo, ni kwamba hatujuani, mimi nimefanya biashara na zero capital kuanzia, na kuna wakati sales zangu kwa mwaka zilifika 1bn.

Nataka nikueleze, biashara sio hesabu hizo hapo za karatasi, kabisa, kwenye hizo hesabu umeongelea leseni? Na gharama nyingine achana na VAT.


Biashara sio profil and loss account, haya mambo magumu sana, ukifanya masihara inaweza kukugeuka mpaka ukasahau flies ipo wapi wakati wa haja ndogo
 
Sio mtaalam wa biashara za madini

Ila Kuna mwamba katoa Uzi wake wa majuto ya biashara ya madini,

Wengi wametoa comments zao naona zimekaa vibaya vibaya,zinatisha.

Binafs
Nakutakia kila la heri mkuu[emoji120]
Shida ni gharama za uendeshaji ni kubwa mnoo kwa hiyo ukiikamia halafu ukatamanishwa mbele sijui utapata kilo 3 sijui 4 hapo utafilisika ni kuifanya mdogo mdogo
 
KWenye biashara ya madini kuna watu wametusua mbaya mkuu....hukuna kitu ambacho hakina kupoteza chief...wewe kama umaeamua kuwa mfanyakazi endelea kuwa mfanyakazi...maana huku kwenye biashara sio kurahisi kiivyo...
Nikusahihishe,
Mimi Ni mfanyabiashara wa vitu today kabisa

Ila kiukweli kwny madini Sina uzoefu wowote ule.

Ni biashara nnayoitamani,
Ndo maana nategemea rating na comments za wadau wataalam Kama nyie kuweza kuchanganua hayo mambo

Siwez kuingia uko kichwa kichwa mkuu
 
Back
Top Bottom