Natafuta system ya mziki mixer, spiker nk

computer Mkuu na generator
 
Asanteni sana vijana wenzangu kwa michango mizuri. Nami ninahitaji kujilipua kwenye biashara hii ya muziki na nimeshakusanya pesa zinazokaribika kama 10M hivi kwa ajili ya kununua vifaa hivyo. Sasa ninaomba mnishauri nianzie wapi, I mean duka zuri ambalo linauza vifaa genuine, aina za speakers katika levels zote tatu (Bass (double), Midi na Highs), aina na idadi ya booster, crossover, DBX, Equalizer na Mixer. Vitu ambavyo nimekuwa nikifuatilia so far ni PC (ninapenda sana windows pc) so nimeona HP Envy 8GB RAM 1TB Hard Disk inaweza kufaa kuanzia, pia DJ Console (DJ Controller) katika utafiti wangu nikaona Pioneer XDJ-RX itaweza kufaa. Pamoja na hayo ningeomba nipate maelekezo ya namna ya kupanga equipment katika DJ Kit, yaani kifaa kipi kikae juu ya mwenzake. Ninaombeni mnishauri katika hayo na msisite kunikosoa au kunirekebisha pale ambapo nitakuwa nimefanya machaguo ambayo sio. Ninatanguliza shukrani.
 
Sio vibaya kufuta kauli, sasa hivi ninafuta kauli. Fidek toleo jipya ni mziki mwingine, zile spika zinatema balaa.
 
Mimi Mkuu ni DJ kanisani, sijapiga vyombo vikubwa saaana ila wastani.

Upande wa Spika Mkuu kanunue FIDEK, kkoo kuna duka linaitwa Bethlehem, nenda hapo utapata hizo Spika. Zinatema balaa, ninaposema zinatema yaani namaanisha zinatema kwelikweli. Hapa nazungumzia Speaker za Mid na sio Bass.

Bass kamuone mnyama mmoja anaitwa Oprah, nunua single bass ziwe mbili, zinatosha kabisa Mkuu.

Mic kanunue walau ziwe 4, nunua ambazo ni UHF na sio VHF, ni vema kunanunua na Betr za Sony ambazo ni rechargable pamoja na Charger flani hivi, nikipata muda nitakuwekea na picha zake.

Mixer kanunue YAMAHA, wana wakala wao pale njia ya Uhuru, Mixer ya njia 16 inatosha kabisa maana mziki wako sio wa Kanisani.

Nitaendelea.....
 
Ninashukuru sana ndugu yangu Aleyn ...nipo hapa ninasubiri muendelezo, sitoki[emoji144]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mwenye kujua bei ya vifaa vya mziki, mixer ya njia tatu, spiker,amplyfire, na nyaya zake nataka nianze biashara ya disco na matangazo. pia kama kuna zaidi ya vifaa nilivyo orodhesha anisaidie
Mkuu usihangaike na hivyo vitu kwa hapa Bongo utaishia kununua vitu feki tuu...kwa msaada zaidi chungulia link hiyo..kama huwezi namna ya kuagiza nicheki PM ntakusaidia fuatilia link hii Complete DJ System | eBay
 
Mkuu hapa sijakuelewa, yani hapa ni achague kimoja wapo, au izo zote awe nazo?
 
Nimependezwa mada hii,nahitaji vyombo vya mziki kanisani,naomba msaada wako
 
ENZI ZETU UKITAKA KUFUNGA SYSTEM KALI
YA MZIKI TULIKUWA TUNAMUONA,NIKAS
MWAMBA ALIKUWA MKALI
VIJANA SAHV WANACHEZA TU

ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…