MjasiriamaliElimu
Senior Member
- Nov 21, 2013
- 117
- 69
Nimejaribu kupitia baadhi ya koments za watu waliokushauri wengi wameshauri kwa kuangalia angle mbalimbali ila kuna angle moja naona ama haijaguswa au kama nitakuwa narudia basi ni katika kuweka mkazo katika hilo.Heshima kwenu wakuu, mimi ni mwajiriwa wa Serikali, mshahara wangu ni kima cha kati kama milioni hivi kwa mwezi, actually unanitosha kwa kula tu. Nina mtoto mmoja. Mrs. Pia ni mwajiriwa serikalini, mshahara wake ni kima cha chini, Kwa miaka almost 6 nimekuwa nikiishi kwa kukopa bank hivo niliishi kwa robo tu ya mshahara wangu.
Tayari nina kwangu, Ninataka nikope tena 15mil niwekeze kwenye ufugaji wa kambare. I hope sitafeli maana nitawekeza nusu ya hela kwenye samaki, na nusu ingine natumia kujilipia ada ya kusoma udsm, hapo nitakuwa nalipwa mshahara na baada ya 3yrs nitakuwa nimemaliza deni na biashara ya samaki itakuwa na mwelekeo, hapo ndo nitaamua kuacha ama kuendelea na kazi.
Ushauri wenu wajuzi wa maneno.
Kwanza wazo la kuacha kazi na kwenda kufuga samaki si sahihi.Kwa mtazamo wangu.Kufuga samaki huitaji kuwasimamia SAA 24 kama vile unawaangalia wakicheza.Kwa hiyo, nionavyo mimi huna ulazima wa kuacha kazi kwa kufuga samaki labda kama kuna sababu nyingine.Lakini bado unaweza kuwa kazini na kufuga samaki.
Hapa unachotakiwa kuanza nacho ni kijana wa kazi utakayemtrain akufanyoe kazi huku wewe ukisimamia na kujizolea ujuzi, uzoefu,na kuangalia ratiba yako kama itakuruhusu kufanya mwenyewe ikiwa kijana hayupo.
Pili, suala la wewe kufuga samaki hujasema kama unataka kujiajiri katika sekta hiyo kama ndivyo basi ni kweli kuwa kama unataka kujikita katika uzalishaji wa samaki na kuprocess inabidi upate mafunzo pale SUA au sehemu yeyote wanayotoa mafunzo ya ufugaji bora wa samaki ili kutimiza wazo lako.
Tatu ni ushauri tu.Kwa sasa unaingiza kipato kikubwa kuliko mkeo.Heshima ipo na mambo yanaenda kama kawaida.Ila utakapofanya uamuzi wa kuacha kazi ukaingia kwenye ujasiriamali utakaokufanya kipato chako kishuke au kipotee kabisa hapo ndipo wengi wametoa angalizo changoto hizo zitakufanya ukumbuke mshahara wako wa 1m.Fanya tathmini na andaa andiko la mradi litakalokuwezesha kukupa dira na ukifanikiwa basi unakuwa umetusua.
Mwisho kufuga kambale inategemea na soko lako na mahali ulipo.Nashauri anzia sokoni ukipata soko utajua ni aina gani ya samaki ufuge.Ila wengi wanaofuga samaki wanachanganya kambale na sato ili kubalansi uzalishaji kwani Kambale wanazaliana sana na Sato pia ikiwa wanfugwa pekepeke.
Nakutakia uchaguzi mwema na mafanikio mema.