Nataka kuacha kazi nijikite kwenye ufugaji wa samaki

Nimejaribu kupitia baadhi ya koments za watu waliokushauri wengi wameshauri kwa kuangalia angle mbalimbali ila kuna angle moja naona ama haijaguswa au kama nitakuwa narudia basi ni katika kuweka mkazo katika hilo.

Kwanza wazo la kuacha kazi na kwenda kufuga samaki si sahihi.Kwa mtazamo wangu.Kufuga samaki huitaji kuwasimamia SAA 24 kama vile unawaangalia wakicheza.Kwa hiyo, nionavyo mimi huna ulazima wa kuacha kazi kwa kufuga samaki labda kama kuna sababu nyingine.Lakini bado unaweza kuwa kazini na kufuga samaki.

Hapa unachotakiwa kuanza nacho ni kijana wa kazi utakayemtrain akufanyoe kazi huku wewe ukisimamia na kujizolea ujuzi, uzoefu,na kuangalia ratiba yako kama itakuruhusu kufanya mwenyewe ikiwa kijana hayupo.

Pili, suala la wewe kufuga samaki hujasema kama unataka kujiajiri katika sekta hiyo kama ndivyo basi ni kweli kuwa kama unataka kujikita katika uzalishaji wa samaki na kuprocess inabidi upate mafunzo pale SUA au sehemu yeyote wanayotoa mafunzo ya ufugaji bora wa samaki ili kutimiza wazo lako.

Tatu ni ushauri tu.Kwa sasa unaingiza kipato kikubwa kuliko mkeo.Heshima ipo na mambo yanaenda kama kawaida.Ila utakapofanya uamuzi wa kuacha kazi ukaingia kwenye ujasiriamali utakaokufanya kipato chako kishuke au kipotee kabisa hapo ndipo wengi wametoa angalizo changoto hizo zitakufanya ukumbuke mshahara wako wa 1m.Fanya tathmini na andaa andiko la mradi litakalokuwezesha kukupa dira na ukifanikiwa basi unakuwa umetusua.

Mwisho kufuga kambale inategemea na soko lako na mahali ulipo.Nashauri anzia sokoni ukipata soko utajua ni aina gani ya samaki ufuge.Ila wengi wanaofuga samaki wanachanganya kambale na sato ili kubalansi uzalishaji kwani Kambale wanazaliana sana na Sato pia ikiwa wanfugwa pekepeke.

Nakutakia uchaguzi mwema na mafanikio mema.
 
Yaani rahisi rahisi tu namna hii!
Mkuu, ebu fikiria project nyingine na si samaki; anguko kuu huanza namna hii kwa kutopanga mambo vizuri.
 

Kabla hujaanza hiyo biashara nakushauri soma hiki kitabu cha Mawazo 114 ya biashara na mitaji yake.
Whatsapp: 0612607426
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…