Nataka kuacha kazi niwe mjasiriamali, naombeni ushauri

Nataka kuacha kazi niwe mjasiriamali, naombeni ushauri

wadanganyika kwa uoga, mimi niliacha kazi ya take home laki 4 kama wewe nikajiajiri, sasa nina miaka 2 uraiani sijawahi jutia uamuzi wangu. We endelea kukomalia laki nne huku dereva wako anakulamba laki 8 kwa mwezi bila wewe kujua
 
Nina miaka sita toka niajiriwe kwenye kampuni flani,
Mshahara wangu ni tsh 800000 kwa mwezi ambao ukikatwa na makato pamoja na marejesho ya mkopo napokea tsh 421000 kwa mwezi

Familia yangu ni ya watu watatu yani mama,baba,na mtoto mmoja

Nimebahatika kununua Noah mbili ambazo nazifanyia biashara kila moja inanipatia tsh 40000 kwa siku ni sawa na 80000 kwa noah zote mbili

Kwa mwezi ni sawa na 2400000,kiasi ambacho ni Mara tatu ya basic ya mshahara wangu

Nina leseni ya udereva na wakati mwingine naendesha mwenyewe,

Sasa nataka niache kazi ya kuajiriwa ili nijikite zaidi kwenye biashara maana naona inalipa zaidi

Naombeni ushauri

Piga chini,watakuja huku watakuambia usubiri lkn km nafsi yako inakwambia uko tyr piga chini,eti ujipange mpk biz ikue,nakwambia utakua unajiambia hivyohivyo na kwa sababu uko bize na biashara ya mtu mwingine yako inakua inasuasua,hayo masaa labda 8 unayotumia kujenga biashara ya mtu imagine ungeyatumia kujenga biashara yako.
 
Hii sauti "usijaribu hata kidogo, utafilisika, mtu flani alijaribu akashindwa" hii sauti ya kukatisha tamaa na kukujengea hofu siku zote ndio inayowafelisha watu.... UMASKINI NI UOGA WAKO".... Watanzania tuko hivo, na bado tutamsikilizia Mzee Magu atufanyie maamuzi ya maisha yetu. Tunasubiri atuajiri, asipotuajiri basi tena. Hatuna uthubutu hata kidogo... Ila ni wachezaji wazuri saana wa kamari.
Hivi unatafuta nn katika maisha yako kama c pesa? Kazi hata ya kwako ni kazi jamani Kwann tu waoga sana?
Mkuu, maandiko yanasema "Usiombe ushauri wa kupigana vita kwa mtu mwoga '' say Yes, and do it.... Usiiruhusu hiyo sauti ya upande wa pili na utafanya... Impossible is possible.
 
Pamoja na ushauri mzuri unaopewa humu, mwenye jibu sahihi la swala hilo ni wewe mwenyewe. Heshimu hisia zako , songa mbele kwa hilo utakaloamua!!!
 
Waswahili husema
uwoga wao ndio umasikini wako.
Kuna mtu anaitwa Michael Shirima,alikuwa ni rubani analipwa uzuuri tu.
Lakini aliamua kuacha kazi na kuuza mbao.
Leo hii ndiye anayemiliki ndege za precision
Jaribu kuangalia wenye mafanikio je? wameajiriwa au wamejiajiri?
Kama leo Mzee Mengi angekuwa ameajiriwa unadhani angefika hapi alipo leo?
MUHIMU SIKILIZA SAUTI YAKO YA NDANI..KAMA INASEMA ACHA KAZI .ACHA FANYA BIZNEZ
 
Hizi ndio mentality za Watanzania wengi. Yuko radhi kung'ang'ania ajira ya laki 7 ila anaogopa kuchukua risk ya biashara inayoweza kumuingizia 3m
omba_yasikukute_mimi_ni_chui_niliyejeruliwa_am_speaking_through_my_experience
 
nakushauri endelea na kazi kwanza angalau hizo noah zifike 5 then kiroho safi achana na kazi za watu,hizo noah zitatosha sana kukupa mtaji wa kufanya biashara nyingine na kujipanua zaidi kibiashara
 
nakushauri usiache kazi mkuu cha kufanya ongeza biashara ingine ambayo si ya magari ya moto ikusaidie
 
Usiache kazi endelea nayo na wekeza hela kwenye mradi mwingine uwe na miradi miwili unayopambana nayo pamoja na kazi mkuu.
 
omba_yasikukute_mimi_ni_chui_niliyejeruliwa_am_speaking_through_my_experience
Kwahio bad experience yako ndio rule kwa wengine? Kuanguka kupo, ukianguka unainuka unaangalia umejikwaa wapi....sio ku-give up.
 
Nina miaka sita toka niajiriwe kwenye kampuni flani,
Mshahara wangu ni tsh 800000 kwa mwezi ambao ukikatwa na makato pamoja na marejesho ya mkopo napokea tsh 421000 kwa mwezi

Familia yangu ni ya watu watatu yani mama,baba,na mtoto mmoja

Nimebahatika kununua Noah mbili ambazo nazifanyia biashara kila moja inanipatia tsh 40000 kwa siku ni sawa na 80000 kwa noah zote mbili

Kwa mwezi ni sawa na 2400000,kiasi ambacho ni Mara tatu ya basic ya mshahara wangu

Nina leseni ya udereva na wakati mwingine naendesha mwenyewe,

Sasa nataka niache kazi ya kuajiriwa ili nijikite zaidi kwenye biashara maana naona inalipa zaidi

Naombeni ushauri
Mbona tayari jibu unalo? Compare your net salary and income from your Noah's ambazo nazo unapigwa si chini ya asilimia 40 ya unacholetewa
 
Kama ww ni mwanafunzi au mtu yeyote asiye na ajira au mwenye mshahara mdogo tafadhali bonyeza link ifuatayo uweze kutengeneza hadi dollar 500 sawa na shilingi milioni moja na laki mbili za kitanzania kwa siku.kujiunga ni bure kabisa.Anza sasa kulipwa kutokana na kutumia muda wako kwenye internet.Kwa ufafanuzi ukishindwa kujiunga nitafute 0718115516.unaweza kunitumia meseji wasap au kwa njia ya kawaida.bonyeza sasa link hii
TheJobTasks.com - Earn from Your Home, Earning website for Students, Job-less people
 
Jobless Na wanafunzi changamkieni fursa,but be very careful
 
ktk mambo ambayo ni uamuzi mgumu ni pamoja na kuacha kazi mkuu ktk watanzania 100 utakaowaomba ushauri sidhani kama hata 10 watafika wakao kupa moyo juu ya uamuzi wako zaid sana ni vitisho tuu nothing else

Mkuu kuendelea kung"ang'ani kuajiriwa ni kukaribisha umaskini nyumbani kwako kwa speed ya 4G haiwezekani ukomae kulinda ajira yenye basic ya 800k uache kuisimamia kazi inayokuingizia 2.4ml punguza uoga mkuu fanya uamuzi sahihi otherwise hata hizo noa zako zitapote cha msingi kuwa makini tu all the best mkuu
 
Nimekupata vema mkuu
 
Endelea na kazi na uendelee kuwekeza zaidi kwanza
 
Back
Top Bottom