Nataka kuachana na mke tuliyezaa naye watoto watatu. Amenishinda tabia!

Mimi wangu aliondoka sasa nimerud nyumbani siku mkuta akasema kaenda msibani,nikamuuliza ni msiba gani ambao mimi siiujui???basi akaongea na dada yake eti kuna msiba sijui wa nani(sikuwaelewa)ingawaje ulikuwa msiba kweli lakini haukuwa na maana ya yeye kutoka wilaya moja kwenda nyingine na kushindwa kunipigia simu au hata kuja kazini kwangu kama sipatikani kwa simu na gari za kawe zinapatikana kariakoo.

Basi nikatoka na jibu moja nikamwambia arudi hukohuko msibani alipotoka,du huwezi amini yule mwanamke saa tano usiku akavaa akataka kuondoka kurudi kule.

Basi nikafunga mlango nikamwambia huu usiku ila kesho urud hukohuko msibani,yule mwanamke hiwezi amini ilivyofika asubuhi kaoga kaondoka huko kawe.

Nilikaa siku 11 yeye yupo tu kwa ndugu zake,siku ya 12 taraka ilimfuata hukohuko wakazikataa,mshenga karudi akanipa majibu kuwa wamekataa,hivyo wanataka yazungumzwe.

Nikawaona hawa wote hawana msaada,yaan mtoto wao kakaaa siku 11 hawakutaka tuzungumze,leo wanaona taraka tuzungumze??nikawaambia sina huo muda.

Hapo upande wa ndugu sikuwapa taarifa ndipo wao wakaona njia mbadala kupitia kwa ndugu zangu ndipo nami niliopofunguka,ingawaje walielewa sana,hivyo msimamo wangu ulikuwa uleule ni taraka tuu.

Basi hakukuwa na namna kalia kanyamaz akataka vitu tugawane,nikamwambia chukua utakavyoviweza sina muda kugawana vitu,alibeba mpaka viberiti.

Baada ya miezi 5 nikaoa mke mwingine nipo nae maisha safi tunajenga familia.

NB:UKIONA MWANAMKE KWAO ANASIKILIZWA SANA,HAKUFAI HILO NI BOMU LITALIPUKA TU.
 
Kumekucha harusi nyingine Lamomy
 
Wala hata sio ubishi,hapo huyo mwanamke anatafuta njia ya kumwendesha tu jamaa,akithubutu kumfata basi kosa dogo tu demu kwao akijua atafuatwa
ukishakuwa mwanaume epuka sana kushindana na mwanamke coz wanawake wanapenda ligi na kuvimbiana.

Sasa kwa situation ya mleta mada akifanya unavyomshauri yeye binafsi hatopata shida ila watoto watateseka sana
 

Mwanamke akiona amani imezidi atahangaika mpaka awe single maza!!
 
Kama wote mmeridhia hapo tatizo halipo na divorce mahakamani ipo tayari hapo sawa. Wasiwasi wangu mtaendelea kupeana tu. Pili mnahitaji uvumilivu kustahimili aibu hiyo maana watoto wakikuwa watajua kila kitu na watawashangaa sana
Watoto wake wameafiki watoto wa huyu wameafiki so ndugu zao wanaafiki hii ndoa
 
Watoto wake wameafiki watoto wa huyu wameafiki so ndugu zao wanaafiki hii ndoa
Kama ni hivyo kuna heri. Maana hiyo pia ni kutamadunisha ilikuwa imesahaulika kwa sababu ya usomi na kuiga tamaduni za nje ila iko sawa
 
Tungemsikia na yeye pia
 
U
Miss Natafuta utani huo sasa. Tulia kwanza issue iishe yawezekana tuka collide, sisi ni people
Mkuu umetoa ripoti polisi ya kupotelewa na mtu aliye ktk mamlaka yako? Pia kwa wazazi na ndugu kisheria sio kuenyeji? Baada ya hapo chukua hatua ya kutoa talaka na pengine kuoa mke mwingine. Endelea kwa miaka isiyopungua 5 au zaidi ili watoto wakue bila kuoa ili wapate akili zaidi za kuishi na mama wa kambo. UTAKUWA UMEWAJALI WATOTO WAKO. Kuwa na rafiki wa kike angalau mmoja kwa haja za kibinadamu kama unashindwa kuishi hivyo. Nakushauri uishi MWENYEWE ukiwatunza watoto wako. Kuoa mwanamke wa kijijini asiyesoma sana kwa sasa sio suluhisho la ndoa salama. WAKIFIKA MIJINI WANAENDA NA WAKATI MPAKA WANAKUWA 6G. UTASHANGAA KAMA YUKO NA KIDUME. UKIENDA MAHAKAMANI KUTOA TALAKA KIDUME KIMEMCHOkA ATARUDII NA KUKATAA TALAKA. NIMEONA NA KUSHUHUDIA
 
Asante mkuu kwa ushauri wako mzuri . Nitaanza taratibu za kisheria mwezi wa sita kwa sasa niko na kazi nyingi binafsi na za taasisi
 
Kuna muda ukipata shuhuda Kama hizi, hofu kubwa inatanda! kufikiria hii taasisi ndoa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…