Nataka kuachana na mke wangu ambaye nimeishi naye miaka 2

Wanaoachana Huwa hawasemi
 
Nenda mahakama ya temeke

Hawana mbambamba


Si umehamua kumuacha mkeo bila sababu za msingi
 
Hilo swala kunyima unyumba ni jambo la kikatili sawa na mtu ulipe ada then unaambiwa usifanye mtihani.
 
Habari yako ,binafsi nakuunga mkono umuache haraka,ila tutumie mbinu unipe namba nimtongoze nimpige miti halafu utumie kama kigezo cha kumuacha,unaona aje hiyo?
 
Ukisikia Kuna watu wanazungumzia ukubwa jua sio namba ya umri ni namna gan utakabiliana na changamoto zinazokuja kweny maisha yako.pole sana
 
Je mnasali pamoja
Je mna Biblia na vitabu vya Sara
Je Umewai kukusanya familia yako mka sali pamoja kabla ya kwenda kulala
Je Umewai kwenda pamoja kanisani au msikitini
Kama amfanyi hivi basi kwanza mkaribisheni Yesu mambo yatakwisha,
 
USIMUACHE BADILI TABIA!

1.Kama anakunyima unyumba ni kwasababu Unamuomba,usiombe unyumba kama hataki tafuta mwanamke nje!!ukimpata lala nae mzungu wa nne!

2.Tunza uchumi wako mfukoni mnunulie ya msingi tu pesa usimpe kabisa ,pesa apate Toka kwa mpenzi wake mpya kama anae!!

3.Jenga dhana ya kutoachana Bali kusitisha uhusiano nankufanya kuwa domarnt tu,kuachana ni ushamba hasa kama mna watoto mmezaa!!

Mwanamke anaetumia unyumba kama silaha kwako Huwa anahisi bila yeye huwezi ishi kana kwamba utakifa vile!!madem kibao mtaani Tena hawana Hela ya kula wanaunga unga TU unakosaje man!!?

Acha kulia Lia ,usipoiomba TU hata wiki atashtuka na kuanza kuhisi unatoka nje akikuuliza mwambie wewe sio padri ukininyima naipata nje na wewe endelea na wako!!
 
Nakupa ushauri wa kiume Tena ufanyie kazi haraka.Kwanza kabisa hakikisha umempandisha cheo anakuwa mke mkubwa ila hakikisha mke mdogo anakuwa mzalendo Kwa maana Hana hata tabia moja kati hizo then Fanya uwezavyo ajue kuwa umeoa mke mwingine ili uone atabadili tabia asipo badili faster mpe Talaka na Wala usiangalie nyuma ama kuwaza jamii itakufikiriaje Kwa kuwa kwenye hili wewe ndio mhanga mkubwa
 
Rudi nyuma kidogo,hilo linaongeleka,peleka hiyo issue kwa wazazi wako na wa kwake,ikishindikana peleka kwa kanisa au msikiti,ikishindikana sasa unaweza kuamua lolote...
 
Ongezeko la single Maza hebu fanya kusamehe mara 70 dunian tunaishi Kwa mda mfupi Kaa furahia na mke na mtoto wenu kila mtu anamapungufu yake ingekua poa tungesikia na mkeo anasemaje pia
 
Mambo ya ndoa magumu sana, Ijumaa jioni wiki hii alikuja binti mmoja kwa mke wangu, walikaa more than three hrs wanaongea, anamuomba akaongee na mama yake mlezi kuhusu jambo linalomkabili nyumbani kwake kwamba anataka kuondoka kwa mumewe kwasababu wamekuwa hawana mahusiano mazuri kwa muda mrefu hadi ikafikia amezaa mtoto mmoja asiye wa mumewe, hivyo anataka aondoke ndoani akalee huyo mtoto akiwa nje ya hapo.
 
Uamuzi sahihi, tena kama huna Mali fanya faster
 
Naona kwisha wadau wanakusakama kwa uamuzi unayotaka kuchukua. Haha asee pole sana.

Skia, ukiachilia mbali ups and downs za ndoa kitu kimoja kinachowatesa wote wawili ni UBINAFSI. Wewe unataka mkeo afanye kitu ili ufurahi na mkeo nae Kuna namna anatarajia ufanye mambo fulani ili afurahi.

Hakuna ambaye yupo tayari kufanya jambo kumfurahisha mwenzie. Yaani kila mtu anajiangalia yeye.

Kaka sikusimangi, ila swali....ukiachana na mkeo vipi mustakabari wa mtoto wenu mwenye miezi 7?

Hilo kaka wewe hujali sio. Furaha ya mtoto kutoka kwenye malezi ya wazazi wote wawili Hilo kaka kwako sio kipaumbele au vipi, na si ajabu na mkeo nae Hilo halimsumbui kichwa maana anasubiri umtoe out kama realMamy alivyoshauri ndio penzi linoge kaka.

Kaka Jitahidi kuwa chanzo Cha furaha kwa unaowapenda nasio utegemee furaha kutoka kwao. Hata huyo mamaa mshauri, Acheni UBINAFSI. Naelewa wanawake wanaongoza ktk hili. Najua hapo ladies mtaona nawananga.

Wake up brother. Ukiona kitu hakikufurahishi usinune na kukaa kimya. Mwambie mwanamke wako Nini hupendi Nini unapenda. Usisahau huyo sio demu wako kwamba unaogopa ukimkalipia atakataa kuileta geto. Huyo ni mkeo, Ongea kama kichwa Cha familia.

Otherwise jitahidi kuwa muumini wa kujenga zaidi na sio kubomoa. All the best kwisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…