Nataka kuachana na ualimu haraka. Nikimbilie wapi?

Nataka kuachana na ualimu haraka. Nikimbilie wapi?

Niende kwenye mada moja kwa moja

Mimi ni mwalimu kiwango cha elimu ni diploma katika masomo ya PHYSICS na BIOLOGY.

Baada ya misukosuko ya ualimu ikiwa ni pamoja na kupigwa na maisha vizuri tu,
Nimekaa na kuamua kurudi shule kusoma/kujiendeleza kielimu.

Ndugu zangu naombeni ushauri wenu naweza soma course gani nje ya ualimu ambayo itakuwa na tija kidogo kwa taifa letu (ualimu siutaki tena Mimi nimechoka).

Sifa ni diploma ya ualimu wa sayansi katika masomo niliyo taja (PHYSICS na BIOLOGY).

Japo kuna watu wamenishauri kwa cheti changu hicho cha diploma nikasomee bachelor of science in PHYSICS or bachelor of science in BIOLOGY .

Naombeni ushauri jamani ualimu umenishinda nimeinua mikono juu....

NAWASILISHA.
Kwa hiyo ni muajiriwa wa serikalini? Kasome health management , ukiikosa mzumbe ipo st John hii ukimaliza tu utahamishwa halmashaur au hospital kama katibu afya, kasome engineering ukitoka andika barua kuomba kuhamia taasis nyingine japo hata ukienda halmashaur utapata Hela kuliko walimu
 
Back
Top Bottom