Late 2009 kuna Mwl mmoja alifanya uamuzi kama huu unaoutaka wewe, yeye alisoma kozi fupi ya Ualimu wa Sekondari mwaka 2006 kipindi Shule za kata zimeanzishwa. Sasa alimua kwenda kusoma Degree ila aliamua kubadili kozi ya kwenda kusoma chuo, alichagua Accountancy na alifanikiwa kudahiliwa UDOM.
Wakati anaomba ruhusa kwa mwajiri wake(DED) alidanganya kuwa anaenda kusoma Ualimu akapewa ruhusa.
Baada ya kumaliza Chuo akiwa na Degree ya Accountancy akashindwa kurejea kwa mwajiri ili aendelee na kazi maana alidanganya tangu mwanzo. Akaamua kuingia mtaani ili atafute kazi. Aisee mambo yakawa magumu sana akafanya Application nyingi za kazi bila kuitwa hata Interview moja, stress si ikapiga hodi akakondeana hatari maana mwanzoni alikuwa bonge. Wenzio ambao hawakudanganya wakarejea kazini(Ualimu) bila usumbufu wowote tena wengine waliopata GPA kubwa walipangiwa Vyuo vya Ualimu kwenda kufundisha, yeye akaanza kujutia uamuzi wake.
Sasa hivi sijui yuko wapi maana mara ya mwisho nilikutana naye mwaka 2015.
Kwa hiyo binafsi nashauri kama hauna chanzo kingine cha ugali, usiache ualimu ukakimbilia kusoma kozi nyingine tofauti na hiyo Ualimu, imagine walimu wamejaa mtaani wenye degree na wanatamani wakafundishe hata Primary angalau wapate hela ya kusogeza siku