Nataka kuachana na ualimu haraka. Nikimbilie wapi?

Mshikaji wangu alikuwa mwalimu shule ya msingi. Akaupiga chini akaenda kusoma diploma medicine akamaliza akapiga degree medicine sasa hivi ni doctor.
Wakati aliacha kazi ilikuwa kama masihara. Mwisho alitoboa.
Sio kila njia aliyopita mtu na mwingine anaweza kupita.

Tungepata na background ya huyo Dokta aliyepiga chini Ualimu ili tuweze kumshawishi na huyu vizuri
 
Sio kila njia aliyopita mtu na mwingine anaweza kupita.

Tungepata na background ya huyo Dokta aliyepiga chini Ualimu ili tuweze kumshawishi na huyu vizuri
Mshikaji nilisoma naye Primary na sekondary, hakupata ufaulu mzuri akaenda Ualim Certificate alifanya kazi kama miaka mitano tu. Akaacha akaenda kusoma diploma ya medicine. Baba yake mzazi alikuwa mchungaji wa Kanisa. Walikuwa na maisha yakawaida sana kama unavyojua kijijini.
 
Ahsante kaka na nitaubeba ushauri wako...pia naomba niulize swali , ni vp endapo nitaenda kusoma bachelor ya biology ama physics pasipo ualimu ? Inaweza niletea shida kwa mwajiri?
Naungana na jamaa aliyekushauri kuwa ukasome Bachelor ya Ualimu tena halafu baadae ukasome Master ya kitu kingine e.g Master of Business Administration then utaweza kupata wigo wa kuhamia taasisi zingine.

NB: Usisahau pia umri unakimbia, kwa bongo umri ukikimbia halafu huna msingi wa uchumi ni risk sana.
 
Upo sahihi .... mshahara umetoka jana lakin leo sina kitu na gas inaelekea ukingoni , na ndugu na wadogo zangu wanaomba chochote, wanaamini nnakaz nna pesa kumbe taabu tupu
Halafu enzi nasoma primary Walimu nilikuwa nawaona maisha mazuri sana.

Kuna Mwl alikuwa amezaa watoto wengi(7+) huku akiendelea kuzaa, halafu hana source nyingine ya income isipokuwa mshahara tu.

Mke ni mama wa nyumbani, watoto wake wakubwa wa kwanza na wa pili alikuwa anawasomesha sekondari shule za private, halafu maisha yalikuwa yanaenda vizuri tu. Sijui siku hizi kwanini haya mambo yanashindikana hata kama mambo yanabadilika.
 
Kwa ufupi alikuwa na support wakati anasoma Diploma ya Medicine.

Kwa mtu ambaye hana support ni vigumu, isipokuwa kama anajiweza mwenyewe kujihudumia
 
Bro maeneo niliyopo hayan support kabisa npo Tanga ndan ndan
 
Hao wapo ndio lakin utakuta unapata 1 kwa 100 au labda walio mjin ....Mimi hapa kituon kwangu hamna kitu ata kula wanakula vibaya tena chakula cha watoto wa hostel
 
Acha kujidhalilisha mwalimu acha dhalilisha walimu kama shida zako ni wewe usiwapake matokeo walimu nyie ndio mnatakiwa kufukuzwa kazi maanq hamjitambui
Bro kua mtulivu kaka, hamna anaeweza nifukuza kazi kisa nimesema ukweli kua maisha ni magumu, najua ata wew unatambua lkn nashangaa kwanini unakua mkali
 
Shukran kaka
 
Badala ukawe MC unarudi tena kupoteza hela?
 
Bro alaf waalimu wa msingi nimefuatilia nimegundua Wana maisha mazuri kuliko sisi wa secondary, sijui mchawi wetu nani
 
Maneno makavu kabisa haya bila kumuwazia mtaji atapata wapi

Niliajiriwa nikiwa Afisa kata wa fani X
Baada ya kufanya Kazi mwaka nikarudi chuo kusoma fani Y (Nilidanganya kwa DED naenda kusoma X ila nikaenda kusoma Y).

Na kibaya/kizuri zaidi nikaunga kabisaa mpaka masters ya Y.

Kurudi kazini (baada ya kutoka chuo) nikawasilisha cheti.
Baada ya miezi kadhaa nikafayiwa recategorization na kwenda kwenye hiyo Idara ya Y, nikafanya Kazi miezi 8 nikapata shavu la KUKAIMU MKUU WA IDARA.

The point is Amoc thefdon unaweza kusoma chochote na kufanya Kazi yoyote.

Ukirudi kazini ukakuta HR anazingua Kuna fursa kibaoo...
1. Kuhamia ofisi nyengine ya serikali (transfer)
2. Kuomba Kazi upya kupitia Ajira.go.tz

#YNWA
 
Naongezea Mkuu, Kuna rafiki yangu somebody Felicia shimbewangoso alikuwa na ujuaji wa hapa na pale, aliingia Kama mwalimu wa krashi programu kwa enzi hizo miaka 2016/2017, Basi bwana kapiga kazi,muda ulipoenda akaenda kusomea bachelor ya mazingira sijui na Nini huko wlipohitimu alirudi kazini Kama kawaida,maana enzi hizo ufuatiliaji ulikuwa duni,hivyo aliendelea kupiga kazi Kama kawaida na bachelor yake hiyo.

Mwaka 2016 kwenye uhakiki wa watumishi hewa si akaombwa apeleke cheti Cha taaluma ,akitoe wapi ,maana bachelor yake alisoma vitu tofauti na ualimu,mwisho wa siku akapigwa chini ,Sasa hivi hata Mia Hana,kapauka sana ,anajutia uamuzi wake.

Mwisho wa siku kwako mtoa mada, usijifunze kwa walioshindwa, fanya kile moyo wako unakutuma kufanya, Mimi pia nampango wa kusoma mambo ya community development niachane na fani ya ualimu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…