Nataka kuachana na ualimu haraka. Nikimbilie wapi?


Kwanini asingefanyiwa RECATEGORIZATION?

#YNWA
 
Hii tunaita kujiongeza,wengi wanateseka kwa kukosa uwezo wa kujiongeza yaani wanakuwa rigid wanakosa flexibility.
Mtu anasoma halafu utakuta amerelax tu anangoja makaratasi yake ndio yamuokoe.
 
Kwenye maisha usiige mtu,kila mtu ana timing zake.
Hata kama kwao maisha ni ya kawaida huwezi kujua alifanya connection gani hadi akatoboa,siri ya mtu ni kichaka.
 
Eti afisa uvuvi wachache [emoji1787]

Kabla ya kufanyiwa recategirization unajua mara ya mwisho ajira zao walitangaza lini ? Unaongea kana kwamba kuna uhitaji kwenye idara hiyo

Nimemaliza na wanangu wengi tu wa aquaculture hapo Sua bado ngoma ni bila bila


Mtoa mada siku hizi ajira ngumu baki huko huko ulipo ila tu ji upgrade ongeza elimu yako kwenye kada yako siku hizi ajira ni ngumu kila sehemu kila sekta
 
Bachelor of science in Physics, Chemistry....Ili iwaje sasa?

Ni bora ujiendeleze Ualimu.

Au soma kozi za Afya.
 
Nenda kasome kozi za mazingira badae rahisi kukubalishia kwa sbb ya masomo yko na kuwa afisa mazingira 🙏
 
Ajira za uvuvi zimetoka chache kipind cha hapo nyuma.
 
Akisoma CPA akiwa chuo itamlazimu kuanzia ATEC I mpaka aje kumaliza inawezekana na chuo chenyewe kikawa kimeisha na Bado asiipate hiyo CPA kwa sababu Hana msingi kwenye Uhasibu.

Bado hujamshauri
Na ikiwa mtu ana bachelor of science, say, education, then akaongezea na CPA. Akirudi halmashauri anaweza kufanyiwa recategorization kwa kwa cheti cha CPA?

Msaada mkuu kama una uelewa na hili.
 
Kwanini asingefanyiwa RECATEGORIZATION?

#YNWA
Na ikiwa mtu ana bachelor of science, say, education, then akaongezea na CPA. Akirudi halmashauri anaweza kufanyiwa recategorization kwa kwa cheti cha CPA?

Msaada mkuu kama una uelewa na hili.
 
Vocha ya elfu 10 hyo hapo,umejitahidi sana kuelezea ukweli
3457 467 345 2345
 

Inawezekana kufanyiwa recategorization. Hakuna Idara yenye watumishi "waliotosha"
Unachotakiwa kufanya ni kutafuta halmashauri yenye upungufu halafu unahamia huko.

Usitake ufanyiwe recategorization hapohapo halmashauri yako.

Cha kufanya hapo ni kuhama halmashauri kwa kutafuta halmashauri yenye upungufu.

Mfano: Halmashauri yetu ilikuwa na Afisa tehama mmoja tu.

Juzi tulipokea mwana katokea halmashauri ya mjini na kuhamia kwetu.
Aliajiriwa huko mjini kama mwalimu ma diploma.
Kaenda kusoma IT.

Kurudi kakuta ma-IT wengii halmashauri kwao huko mjini.

Akaanza kutafuta Chaka, akalifumania halmashauri yetu.

Basi amehamia sasa, kwahiyo hapo tegemea bajeti ijayo anatoboa na kuwa full IT.

#YNWA
 
Na ikiwa mtu ana bachelor of science, say, education, then akaongezea na CPA. Akirudi halmashauri anaweza kufanyiwa recategorization kwa kwa cheti cha CPA?

Msaada mkuu kama una uelewa na hili.
Unaweza ila kuna maafisa utumishi wengi hawajui kusoma muundo pale unatakiwa ubadilishiwe kwa kutumia statement of result ya intermediate ndio wanaiterm kama degree au foundation wanaiterm kama certificate ila kuna baadhi ya maafisa utumishi hawajui muundo basi ni shida wanasumbua watu mno
 
Shukran sana tena sana mkuu mrsmau , huu mrejesho mzuri kwangu.
Hayo mengine tutaeleweshana tu kama mdogo mdogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…