Nataka kuachana na ualimu haraka. Nikimbilie wapi?

Nataka kuachana na ualimu haraka. Nikimbilie wapi?

amoc thedon

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2016
Posts
345
Reaction score
531
Niende kwenye mada moja kwa moja

Mimi ni mwalimu kiwango cha elimu ni diploma katika masomo ya PHYSICS na BIOLOGY.

Baada ya misukosuko ya ualimu ikiwa ni pamoja na kupigwa na maisha vizuri tu,
Nimekaa na kuamua kurudi shule kusoma/kujiendeleza kielimu.

Ndugu zangu naombeni ushauri wenu naweza soma course gani nje ya ualimu ambayo itakuwa na tija kidogo kwa taifa letu (ualimu siutaki tena Mimi nimechoka).

Sifa ni diploma ya ualimu wa sayansi katika masomo niliyo taja (PHYSICS na BIOLOGY).

Japo kuna watu wamenishauri kwa cheti changu hicho cha diploma nikasomee bachelor of science in PHYSICS or bachelor of science in BIOLOGY .

Naombeni ushauri jamani ualimu umenishinda nimeinua mikono juu....

NAWASILISHA.
 
Kuosha magari Posta-Dar.

Kuosha magari Posta, gari moja ni Tshs 5000 kwa siku unaosha gari 10 kwa wastani utapata 1.5 milioni kwa mwezi ambayo haikatwi kodi wala haina TOZO za MWIGULU wa SINGIDA ALL STARS. sasa Singida big Stars, Esther Luxury .

Watu wa SENSA wakija unawaambia huna kazi, hulipi kodi, unakula kwa mama lishe ugali wa 1500 kwa mchana na jioni unamwagilia moyo kwa bwashee.

Utapata hela nyingi kuliko bank Teller wa CRDB Ushirika tower Dar anayelipwa 1.5 m p.m na makato kibao! ..
 
kuosha magari posta.
kuosha magari Posta, gari moja ni Tshs 5000 , kwa siki unaosha 10 kwa wastani utapata 1.5 milioni kwa mwezi ambayo haikatwi kodi wala haina TOZO za MWIGULU wa SINGIDA ALL STARS.
Utapata hela nyingi kuliko bank Telleer wa CRDB
Nilivyoanza kusoma hii comment nilijua unamdhihaki ila dah kweli town hapa mipango tuu.. 🙌
 
kuosha magari posta.
kuosha magari Posta, gari moja ni Tshs 5000 , kwa siki unaosha 10 kwa wastani utapata 1.5 milioni kwa mwezi ambayo haikatwi kodi wala haina TOZO za MWIGULU wa SINGIDA ALL STARS.
Utapata hela nyingi kuliko bank Telleer wa CRDB
Nyie motivation speakers huwa mnaongea tu.nani akupe elfu 5 kwa siku kwa kuosha magari tu?kwanza hayo magari 10 unayosema ya kuosha unayapata wapi kila siku?
 
Nyie motivation speakers huwa mnaongea tu.nani akupe elfu 5 kwa siku kwa kuosha magari tu?kwanza hayo magari 10 unayosema ya kuosha unayapata wapi kila siku?
Mkuu usipende kuwa negative, utanisamehe kama ntakukera.. ila yuko sahihi eneo lolote mjini mfano Posta, Mnazi, Livingstone, Mwenge (Mlimani kwa madalali), na kwingine kwenye parking hukosi waosha magari.. Nna miezi sijaosha gari town bei ilikuwa 3000 labda itakuwa imepanda, kulifuta tu vumbi gari 1500 mpaka 2000.

Gari ni nyingi sana mjini mkuu na nyingi zinapark na kutoka so hii ni fursa japo inaweza isifike 1M kama alivyosema maana kuna gharama ya sabuni ya unga na maji..ila jiulize mtu kaingia town saa 2 asubuhi mpaka saa 12 jion. Mbona gari 10 easy tu tuseme kila saa ana gari 1... hata akipata magari 6 kwa siku bado si haba kuliko mzunguka na mavyeti moka imepaukaaa kutwa kuomba nauli!
 
Nashukuru ndugu, sina chanzo chochote cha uchumi lakini nikitaka nibadili fani nikiwa bado mwalimu
Late 2009 kuna Mwl mmoja alifanya uamuzi kama huu unaoutaka wewe, yeye alisoma kozi fupi ya Ualimu wa Sekondari mwaka 2006 kipindi Shule za kata zimeanzishwa. Sasa alimua kwenda kusoma Degree ila aliamua kubadili kozi ya kwenda kusoma chuo, alichagua Accountancy na alifanikiwa kudahiliwa UDOM.

Wakati anaomba ruhusa kwa mwajiri wake(DED) alidanganya kuwa anaenda kusoma Ualimu akapewa ruhusa.

Baada ya kumaliza Chuo akiwa na Degree ya Accountancy akashindwa kurejea kwa mwajiri ili aendelee na kazi maana alidanganya tangu mwanzo. Akaamua kuingia mtaani ili atafute kazi. Aisee mambo yakawa magumu sana akafanya Application nyingi za kazi bila kuitwa hata Interview moja, stress si ikapiga hodi akakondeana hatari maana mwanzoni alikuwa bonge. Wenzio ambao hawakudanganya wakarejea kazini(Ualimu) bila usumbufu wowote tena wengine waliopata GPA kubwa walipangiwa Vyuo vya Ualimu kwenda kufundisha, yeye akaanza kujutia uamuzi wake.

Sasa hivi sijui yuko wapi maana mara ya mwisho nilikutana naye mwaka 2015.

Kwa hiyo binafsi nashauri kama hauna chanzo kingine cha ugali, usiache ualimu ukakimbilia kusoma kozi nyingine tofauti na hiyo Ualimu, imagine walimu wamejaa mtaani wenye degree na wanatamani wakafundishe hata Primary angalau wapate hela ya kusogeza siku.
 
Mkuu sijasoma chemistry advance naweza pata ? Maana Mimi cheti nilicho nacho ni hiko cha diploma ya physics na biology
Advance umesoma kombi gani na je matokeo yakoje
Hakuna kazi yeyote ya kuajiriwa utakayofurahia,ukifurahia maisha kwa kuajiriwa kada yeyote tena serikalini niite MBWA nimekaa paleeee.
Karibia kila kazi ya kuajiriwa usitegemee kufurahia
 
Back
Top Bottom