Nataka kuachana na ualimu haraka. Nikimbilie wapi?

Nataka kuachana na ualimu haraka. Nikimbilie wapi?

Late 2009 kuna Mwl mmoja alifanya uamuzi kama huu unaoutaka wewe, yeye alisoma kozi fupi ya Ualimu wa Sekondari mwaka 2006 kipindi Shule za kata zimeanzishwa. Sasa alimua kwenda kusoma Degree ila aliamua kubadili kozi ya kwenda kusoma chuo, alichagua Accountancy na alifanikiwa kudahiliwa UDOM.

Wakati anaomba ruhusa kwa mwajiri wake(DED) alidanganya kuwa anaenda kusoma Ualimu akapewa ruhusa.

Baada ya kumaliza Chuo akiwa na Degree ya Accountancy akashindwa kurejea kwa mwajiri ili aendelee na kazi maana alidanganya tangu mwanzo. Akaamua kuingia mtaani ili atafute kazi. Aisee mambo yakawa magumu sana akafanya Application nyingi za kazi bila kuitwa hata Interview moja, stress si ikapiga hodi akakondeana hatari maana mwanzoni alikuwa bonge. Wenzio ambao hawakudanganya wakarejea kazini(Ualimu) bila usumbufu wowote tena wengine waliopata GPA kubwa walipangiwa Vyuo vya Ualimu kwenda kufundisha, yeye akaanza kujutia uamuzi wake.

Sasa hivi sijui yuko wapi maana mara ya mwisho nilikutana naye mwaka 2015.

Kwa hiyo binafsi nashauri kama hauna chanzo kingine cha ugali, usiache ualimu ukakimbilia kusoma kozi nyingine tofauti na hiyo Ualimu, imagine walimu wamejaa mtaani wenye degree na wanatamani wakafundishe hata Primary angalau wapate hela ya kusogeza siku
Angerudi Kwa kisingizio kwamba alidisco chuoni angeendelea na kazi . Watu wengi wamesomea vitu tofauti na ualimu na hawajatolewa kwenye ajira zao chamsingi unaaga unaenda kusomea ualimu pia uwe na joining instructions ya kwamba umechaguliwa kusomea education. Ila unasoma Chuo kingine at the end unarudi kuendelea kufundisha huku unatafuta namna ya kufanyiwa recategorization ili ubadilishe muundo wa kazi yako.
 
still unapoteza muda mkuu kwanza muajiri wako haitambui hiyo course, ingekua enzi za Kikwete ungeweza enda kusoma hata Mass Communication ukae chuo hata miaka 10 hakuna wakuzuia mshahara au kukuuliza mbon hurudi kazin...
Kwasasa nenda kasome Bachelor ya ualimu bahat nzuri una masomo ya sayansi, ukitoka chuo rudi kazini fight kutoka ktk ualimu uhamie taasisi nyingine za serikali NECTA TET UKAGUZI TMDA TBS ukihangaika nao hawa ndani ya 2yrs wanakuhamishia kwao unalamba pesa nzuri, shida yenu walimu hamhangaiki kuuliza taasisi au wizara ambazo unaweza kuhamia... Asikudanganye mtu sasa hivi ajira hazipo otherwise kama una undugu na kiongoz mkubwa sana ambaye akikohoa tu unapewa kazi... Zamani wabunge wakurugenz DC Rc walikua wanaweza kumtafutia kazi mtu na akapata, ila sikuhiz hata wao wenyewe watoto wao wapo nyumban hawana kazi...
Ukisomea education utaendelea kuwa mwl tuu . Labda options ya mwisho uwe lecture tuu TBS mwl anafanya nini kule TBS kuna specialist Kwa kila Kitu options ni kusomea kitu tofauti na ualimu basi . Ruhusa ya kwenda shule zipo Ila
 
Niende kwenye mada moja kwa moja

Mimi ni mwalimu kiwango cha elimu ni diploma katika masomo ya PHYSICS na BIOLOGY,,,

Baada ya misuko suko ya ualimu ikiwa ni pamoja na kupigwa na maisha vizuri tu,
Nimekaa na kuamua kurudi shule kusoma / kujiendeleza kielimu.

Ndugu zangu naombeni ushauri wenu naweza soma course gani nje ya ualimu ambayo itakua na tija kidogo kwa taifa letu (ualimu siutaki tena Mimi nimechoka),

Sifa ni diploma ya ualimu wa sayansi katika masomo niliyo taja (PHYSICS na BIOLOGY).

Japo kuna watu wamenishauli kwa chet changu hicho cha diploma nikasomee bacherol of science in PHYSICS or bacherol of science in BIOLOGY .

Naombeni ushauri jamani ualimu umenishinda nimeinua mikono juu....

NAWASILISHA.
Huku mtaani ni kisanga kama haujajipanga aisee komaa na ualimu wako. Ukibisha acha kazi njoo mtaani uhustle 🤣🤣🤣 miez 3 mingi unarudi tena hapa kulia kia
 
Late 2009 kuna Mwl mmoja alifanya uamuzi kama huu unaoutaka wewe, yeye alisoma kozi fupi ya Ualimu wa Sekondari mwaka 2006 kipindi Shule za kata zimeanzishwa. Sasa alimua kwenda kusoma Degree ila aliamua kubadili kozi ya kwenda kusoma chuo, alichagua Accountancy na alifanikiwa kudahiliwa UDOM.

Wakati anaomba ruhusa kwa mwajiri wake(DED) alidanganya kuwa anaenda kusoma Ualimu akapewa ruhusa.

Baada ya kumaliza Chuo akiwa na Degree ya Accountancy akashindwa kurejea kwa mwajiri ili aendelee na kazi maana alidanganya tangu mwanzo. Akaamua kuingia mtaani ili atafute kazi. Aisee mambo yakawa magumu sana akafanya Application nyingi za kazi bila kuitwa hata Interview moja, stress si ikapiga hodi akakondeana hatari maana mwanzoni alikuwa bonge. Wenzio ambao hawakudanganya wakarejea kazini(Ualimu) bila usumbufu wowote tena wengine waliopata GPA kubwa walipangiwa Vyuo vya Ualimu kwenda kufundisha, yeye akaanza kujutia uamuzi wake.

Sasa hivi sijui yuko wapi maana mara ya mwisho nilikutana naye mwaka 2015.

Kwa hiyo binafsi nashauri kama hauna chanzo kingine cha ugali, usiache ualimu ukakimbilia kusoma kozi nyingine tofauti na hiyo Ualimu, imagine walimu wamejaa mtaani wenye degree na wanatamani wakafundishe hata Primary angalau wapate hela ya kusogeza siku
Ujinga alioufanya ni kutorudi kazini hata kama alidanganya... angerudi na kama wangemzingua angepambana ahame halmashauri..
 
Nilivoanza kusoma hii comment nilijua unamdhihaki ila dah kweli town apa mipango tuu.. 🙌
rest assured , hapa mahakamani wanaotuoshea ma- V-* XLR 2022 tunawalipa 10,000 kwa siku, sasa anaosha gazi zake 5 kwa siku, maji anachukua mahakamani au kwenye AC za ofisi jirani, hawalipi kodi wala hawana TIN , maisha ni mpangilio tu
 
Nyie motivation speakers huwa mnaongea tu.nani akupe elfu 5 kwa siku kwa kuosha magari tu?kwanza hayo magari 10 unayosema ya kuosha unayapata wapi kila siku?
acha dhihaka njoo field hapa Posta, njoo IFM ma-bos wa BOT wana
Nyie motivation speakers huwa mnaongea tu.nani akupe elfu 5 kwa siku kwa kuosha magari tu?kwanza hayo magari 10 unayosema ya kuosha unayapata wapi kila siku?
njoo field uncle , mjini mipango wenzio mtaji ni kitambaa , sponji na sabuni FOMA, jioni anafunga 50,000/-
wewe endelea na white collar job.
 
Kasome fani unayoipenda ukimaliza uombe kufanyiwa recategorization

Mfano inayofaaa kwako
Dentist ina soko na watu ni wachache

Ila usiache, mana kurudi kwenye system utaweza tena
 
Kasome fani unayoipenda ukimaliza uombe kufanyiwa recategorization

Mfano inayofaaa kwako
Dentist ina soko na watu ni wachache

Ila usiache, mana kurudi kwenye system utaweza tena
 
Mkuu vipi hukupata tena ajira ya ualimu [emoji22]. Kama ulipata hongera ila kama hukupata pole sana najiskia maumivu makali kuliko anaechomwa na moto wa petrol. Umefight sana kiongozi wangu Mungu yupo
NASHUKURU sana ndugu yangu....siku bahatika kupata...kwakweli iliniuma sana nilikesha usiku kucha nikashinda mchana kutwa takribani wiki 2...za kupambania kombe bila mafanikio...
 
Ukisomea education utaendelea kuwa mwl tuu . Labda options ya mwisho uwe lecture tuu TBS mwl anafanya nini kule TBS kuna specialist Kwa kila Kitu options ni kusomea kitu tofauti na ualimu basi . Ruhusa ya kwenda shule zipo Ila
Brother ume lack exposure tuu, hii dunia huwez kuambiwa kilakitu, walimu wameajiriwa hadi MSD, TMDA sembuse TBS..? Tena ni walimu waliosomea masomo ya Arts, hii dunia ukikosa exposure utajikuta umebaki kwenye kiofisi kimoja hadi unazeeka...
 
Back
Top Bottom