SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Kuna faida kubwa kwenye umoja. Makabila mengi yalianza bila vision. Mazingira tu yalipelekea watu kukutana sehemu moja na baada ya muda muingiliano, mfanano wa lugha, mila na desturi zilizojengeka ukawaunganisha. Imagine sasa haya yote uyafanye kwa makusudi na kwa kufuata vision mliyojiwekea.
Imagine kundi dogo la watu wakae chini wajenge vision moja ya aina ya watu wanaotaka kuwa halafu kwa umakini mkubwa waanze kujijenga kwa vizazi kadhaa.
Baada ya muda fulani wawe na elimu na maarifa ya hali ya juu, wawe na mila na desturi ambazo ni mpya na tofauti lakini ambazo ni modern kama siyo futuristic. Imagine uunde kabila ambalo limetapakaa dunia nzima, wawe watu wenye mamlaka katika serikali kubwa duniani, katika majeshi, taasisi za media, fedha na zingine zenye ushawishi kabla hata hilo kabila halijajulikana au kutambulika rasmi.
Hilo ndiyo nakusudia kufanya na najua kwa uvumilivu linawezekana. Sitakuwepo wakati hilo limestawi ila nitajivunia kupanda mbegu hiyo.
Napokea ushauri, ukosoaji na pia wale wanaotaka kushiriki katika mwanzo huu mpya mnakaribishwa. 😎